Maofisa NIDA mikononi mwa Takukuru Moshi

Maofisa NIDA mikononi mwa Takukuru Moshi

charles ndagulla

Senior Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
168
Reaction score
110
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru)mkoani Kilimanjaro,inawashikilia Maofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) wakituhumiwa kushirikiana na matapeli wanaowaumiza wananchi kwa kuwauzia vitambulisho hivyo ambavyo kwa kawaida vinapaswa kutolewa bure.

Kwenye mtandao huo wa matapeli,Takukuru ikafanikiwa kumnasa Mwalimu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kiusa iliyopo Kata ya Kiusa Manispaa ya Moshi,Hemed Shaaban Adinan ambaye baada ya upekuzi amekutwa na rundo la vitambulisho ambavyo vilikuwa viuzwe kwa wananchi .

Kukamatwa kwa maofisa hao kunatokana na Taarifa ya mwananchi mmoja(jina kapuni) kwenda kulalamika takukuru kuwa anadaiwa atoe rushwa ya sh,100,000 na ofisa wa NIDA ili aweze kupewa kitambulisho chake jambo mbalo ni kinyume na kifungu cha 15 cha sheria na.11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

"Mtego uliandaliwa uliopelekea kukamatwa kwa Bw.Hemed Shaaban Adinan ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni afisa wa NIDA na baada ya kupekuliwa bw,Hemed alikutwa na vitambulisho ambavyo havijawafikia walengwa",amesema Holle Makungu Mkuu wa Takukuru K'njaro katika taarifa yake kwa wanahabari.

Takukuru wanasema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini watumishi wa NIDA wanaohusika kumpa mwalimu huyo vitambulisho hivyo kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Imesema mara uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kujihusisha na uvunjaji huo wa sheria na kutoa wito kwa wananchi kutambua kwa vitambulisho hivyo vinatolewa na NIDA bureeeee.

Takukuru imesisitiza wananchi watakaodaiwa rushwa na maofisa wa NIDA ili wapatiwe vitambulisho vya uraia wa Tanzania basi wasisite kutoa taarifa ama wapige simu ya bureeeeeeeeeeeee namba 113.

Kazi kwenu wananchi mtakaoombwa pesa ili mpatiwe vitambulisho ,piga simu hiyo buree ili kuwanasa waranguzi wa vitambulisho#Rushwa ni Adui wa Haki
 
Dah hawa wajinga ndio maana tangu mwaka jana hatupati vitambulisho, kumbe wamevifungia ndani ili watupige wajinga hawa.
 
Hapo wachunguze vizuri lazima rushwa ya ngono ipo tena kwa kasi ya 4G+
Tamaa mbaya huyo mwalimu tayari ana Kazi yake lakini anajiongeza hadi kwenye vitanbulisho,sasa atanyooshwa hadi pumbu zichubuke!!
 
Kwenye mtandao huo wa matapeli,Takukuru ikafanikiwa kumnasa Mwalimu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kiusa iliyopo Kata ya Kiusa Manispaa ya Moshi,Hemed Shaaban Adinan ambaye baada ya upekuzi amekutwa na rundo la vitambulisho ambavyo vilikuwa viuzwe kwa wananchi


Miaka hii walimu wanaidhalilisha taaluma yao
 
Kisayansi mwanamume ana uwezo wa kukaa siku tano na mwanamke siku saba bila kula hadi umauti.
Huwezi kumweleza mtu huyu chakula ni buree katika siku ya mwisho ya mpaka wake na kifo. Atatoa rushwa ili kupata hicho chakula cha bure.
Ninachomaanisha ni kwamba serikali ndio iliyoandalia mazingira ya rushwa katika vitambisho vya taifa.
Havijatengenezwa toka mwaka juzi kwa sababu ya ukata. Ref riport ya CAG Kwa mamlaka ya NIDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watanzania wengi wanazungushwa mpaka sasa kupata hivi vitambulisho kumbe kina sisi tumevikamata na kuviuza kwa bei ya juu,Takukuru msiwaachie hao mpaka wataje mtandao wao woteeee
 
Report ya CAG imetaja MOJA ya hasara serikali imepata in kuhusu ununuzi wa machine ya BVR feki tens hawa mapimbi wanafanya ujinga wa kuwauzia watanzania dah hatar sana
 
Mh Raisi Dkt. John Pombe Magufuli ninajua unapitia kwenye mitandao hii,Heshima yako,au una watu wako,wanaopitia naomba utusaidie wakazi wa moshi, ofisi za nida kwa kweli zimekuwa ni mwiba kwa wananchi,tunaomba utubadilishie watumishi hawa wasio waaminifu, dar vitambulisho mwezi mmoja tuu mtu anapata, huku ni zaidi ya mwaka,miaka 2, kila kitu kimekamilika kila ukienda wanakuambia baada ya miezi 3 njoo, ucheki,ikipita miezi 3 wanakuambia tena njoo baada ya miezi mitatu, wengine tunakwama kupata TIN bamba kwa ajili ya biashara, tunashindwa anzisha biashara sababu ya kitambulisho cha taifa,tunakuomba sana uingilie kati, au utoe tamko ninajua hawawezi kuwajibika mpaka wewe uingilie kati. mpiga kura wako.
 
Mh Raisi Dkt. John Pombe Magufuli ninajua unapitia kwenye mitandao hii,Heshima yako,au una watu wako,wanaopitia naomba utusaidie wakazi wa moshi, ofisi za nida kwa kweli zimekuwa ni mwiba kwa wananchi,tunaomba utubadilishie watumishi hawa wasio waaminifu, dar vitambulisho mwezi mmoja tuu mtu anapata, huku ni zaidi ya mwaka,miaka 2, kila kitu kimekamilika kila ukienda wanakuambia baada ya miezi 3 njoo, ucheki,ikipita miezi 3 wanakuambia tena njoo baada ya miezi mitatu, wengine tunakwama kupata TIN kwa ajili ya leseni,tunakosa Ajira sababu ya vitambulisho havitoki,kumbe kuna rushwa,moshi kunatatizo Dr. tunashindwa fanya maendeleo sababu ya kukwamishwa na kitambulisho cha taifa na watumishi wako,tunakuomba sana mzee uingilie kati, au utoe tamko ninajua hawawezi kuwajibika mpaka wewe uingilie kati. mpiga kura wako.
 
Back
Top Bottom