Manzese ni moja kati ya kata za kitambo sana, 1975 tayari ilikuwa ni kata kamili yenye miundombinu inayoekeweka, ndio eneo la kwanza Tanzania kuwa na Daraja la wavuka Kwa miguu ambalo liligeuka kuwa kivutio enzi zile, Kwa miaka mingi manzese imekuwa kitovu cha biashara, burudani Na soko kubwa la unga wa mahindi.
Ajabu ni kuwa hii kata bado ni fukara sana, makazi yake ni duni sana, ukizunguka kwenye mitaa yake kuna ufukara wa kutupwa, mitumba kama sidilia ndiyo inauzika mno eneo hili. Shida iko wapi?
Manzese imebadikika sana ndg, mahoteli ya ghorofa kibao, inaenda kuipiku Magomeni mapipa, maduka makubwa usiseme, barabara za lami na mitaro ipo Kila sehemu, sijui unazungumzia manzese ya mwaka Gani? Pita na kagua tena, utaamini nikiongeacho ndg.
kuna guest nililala hapo,chumba kina kunguni na taa nyekund kuwaua huwez nikabak kujipapasa usiku kucha bila usingiz,chumba kina hewa nzito mixer yale ma-perfume yale kama dawa ya mbuu huku nikiwaza watu wamekulana humu siku nzima.
Nashangaa jamaa sijui anazungumzia manzese ipi? Kuanzia Argentina, Tiptop hadi kwa mfuga mbwa magorofa yanaporomoshwa balaa labda manzese ya midizini kule ndio bado.