Manzese darajani Dar es salaam 2015

Dah...siamini macho yangu hapa lazima niitafute imani ya Tomaso
 
Hapo ni kama Thailand, mabango yake yana maandishi ya kithai!
 
bila shaka hii itakuwa mwaka 2050 coz hayo mzingira hayawezi kutengenezwa kwa mwaka mmoja.pia hakuna nafasi ya kutosha pale kuweka hizo mbwembwe zenu kwa kila upande wa barabara.
 
Usiniambie kutakuwa hakuna bajaji na bodaboda ?????????????
 
Lazima kuwe na mifuko ya rambo imetapakaa kila kona ndo Manzese inakamilika.
 
Hii lazima itakuwa moja ya sehemu isiyo salama kuanzia saa 1 usiku. Watu watakula sana kabari hapo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwenye ufisadi huwezi kupata kitu cha aina hiyo!
 
Yaani sisi Wabongo tulivyo vilaza na umbulula, pale Manzese tayari zile pavements na side blocks zimeshaanza kubomoka.
Wenye maguta, bodaboda, bajaj na wengineo wamezitimba kiasi kwamba sasa hivi vile vitofali vipo tu chali chini kama havikujengwa vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…