Manyigu na nyuki: Shairi-Chombo chenda mrama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manyigu na nyuki: Shairi-Chombo chenda mrama

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Senior Bachelor, Jun 24, 2011.

 1. S

  Senior Bachelor Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chombo kii baharini, mawimbi yasukasuka
  Waloshika usukani, manahodha moja hulka
  Walikitoa ufukweni, baharini 'kiingika
  Abiria mehamaki, chombo chaenda mrama!

  Ilipoanza safari, kutapika walihisi
  Kwa woga wayo bahari, majiye kuyaakisi
  Taratibu wakakiri, hawakuwa nayo jinsi
  Nahodha kawatuliza, kuikabili safari.

  Injiniye yachemka, nahodhaye chamshinda
  Abiria wanamaka, wamehisi kinapinda
  Tobo 'megundulika, 'lotoboa sio kinda
  Manahodha moja hulka, chombo chenda mrama.

  Aloshika usukani, Cheka Jino mpole
  Litia na tumaini, chombo lipopokea
  'Biria lipata amani, wakidhani si gobole
  lo! Kama walotangulia, huyu pia limbukeni!

  Limbukeni 'jisifia, ajigamba yu mweledi
  Jama namhurumia, ajifanya maridadi
  Chombo kinajinukia, hata akipiga dobi
  Ukubwani kaingia, ndevuze hazichomozi!

  Mashauriano afanya, ya akidi na unywaji
  Kila wakiyamaliza, wajipamba kwa uaridi
  Maji ya vikao vyao, machozi ya abiria
  Ndio! chombo ki baharini, maji chumvi hayanyweki!

  Vya wengine vyaelea, bahari haivitishi
  Matobo meyamendea, maji hayawaangushi
  Makasia 'jipigia, kama bwana maangushi
  Chetu kinajizamia, manahodha tubadili.

  Toka kiwe baharini, nchi kavu kijaona
  Kama vile harusini, manahodha hawaj'ona
  Wisiki wazitamani, wa'giza bila amana
  Machoziye abiria, ni kinywaji chao bora!

  Abiria amkeni, kusanyeni zana zenu
  Machoziyo hayanyeshi, hata mchicha wa menge
  Tafuteni nazo nyundo, zibeni hayo matobo
  Manahodha fukuzeni, mchukue usukani.

  Kwa majigu jifunzeni, na kwa nyuki vilevile
  Nyuki wao wafaidi, kwa asali ya sukari
  'Nyigu mwisho ni masega, hivi asali wawezi?
  Lakini kiwasikia, wajiita nao nyuki!


   
 2. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  1. Chomboni kuna matundu, japo bado twaelea,
  Ni kama tunalo gundu, nahodha anapwelea,
  Nahodha hana utundu, hana cha kuelezea,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  2. Chombo si kama shilingi, ama sivyo tungezama,
  Sio ndoto wala bangi, ufukwe nautazama,
  Nahodha huyu mhangi, mpeni njia kina mama,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  3. Tukifika ufukweni, tumpe ridhaa makini,
  Hawezi tuweka poni, bayana yake thamani,
  Apandapo jukwaani, ni vitendo bila ghani,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  4. Kwa unahodha ameiva, tayari kwa kuongoza,
  Jamani mpeni ridhaa, ili safari kuanza,
  Magwanda ameshavaa, nuru kote kuangaza,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  5. Kosa lilofanya jana, kesho katu sirudie,
  Takao kuwa vijana, kwa mdomo washuhudie,
  Ni sherehe ya kufana, kwa sasa tuvumilie,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  6. Tujipe uvumilivu, tupeane taarifa,
  Subira yetu ya mbivu, tazifikia tarafa,
  Hatutakubali mbovu, tatumia maarifa,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

  7. Mpeni ulinzi nahodha, huyo wetu mtarajiwa,
  Changia hata kwa fedha, shughuli kufadhiliwa,
  Shima tuondoe adha, nahodha wetu akitajwa,
  Japo twaelekea kuzama, mbele naona nuru.

   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  nimekikosa kitufe cha thanks naongezea heko!!!!
   
 4. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Heko MSEJA MWANDAMIZI!badili jina kaka kukienzi kiswahili.na kwani hutaki oa?
  Ndoa jama ni tamu,kimpata muadhamu.
  Ndoa mashamshamu,pendo likiwa timamu.
  Ndoa mithili ya ndimu,mchuzi kunogesha hamu.
  Ndoa siyo jahanamu,pendo kishika hatamu.
   
 5. S

  Senior Bachelor Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pangu Pakavu,

  Ulosema yote poa, moyoni yamenipenya
  Japo naitaka ndoa, bado nafsi naifinya
  Walo ndani waniboa, hasa kwa wanachofanya
  Ndoa wazitia doa, utadhani ni mapanya.

  Utafiti nimefanya, kuzihusu hizo ndoa
  Walo ndani wanaminya, nje kujichomozea
  Walo nje wanahenya, ndani kupakimbilia
  Sitaiga tembo kunya, mwandamizi nabakia.
   
Loading...