Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 11,798
- 18,037
Miaka 63 iliyopita, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliandika kijitabu Tujisahihishe, akionya tabia ya kutafuta mchawi nje ya nchi kila tukipatwa na matatizo tuliyoyasababisha sisi wenyewe.
Mwalimu alisema ni rahisi kulaumu “mabeberu” au “watu kutoka nje” kuliko kujitazama na kukiri ukweli kwamba chanzo cha matatizo yetu ni uamuzi na mifumo tunayoitengeneza.
Mwalimu alisema, “Kuna tabia imekita mizizi katika siasa na jamii ya Tanganyika [Tanzania]—tabia ya kutafuta mchawi nje ya mipaka ya nchi yetu kila tunapokutana na matatizo tuliyoyazalisha sisi wenyewe. Ni rahisi sana kulaumu ‘mabeberu,’ ‘makaburu,’ au ‘watu kutoka nje,’ lakini ni vigumu sana kujikagua, kujiangalia kwenye kioo na kusema, ‘Tatizo ni sisi.’
Leo, zaidi ya nusu karne baadaye, ukweli wa maneno hayo unajidhihirisha. Matatizo mengi ya Tanzania, kuanzia KATIBA dhaifu, mfumo mbovu wa uongozi, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ubaguzi kwenye elimu, misafara ya kifahari, hadi tume za uchaguzi zisizoaminika, si maagizo ya mabeberu. Beberu gani ameagiza vyombo vya habari viminywe? Ni uamuzi wa viongozi wetu wa CCM na mfumo walioujenga kwa mikono yao wenyewe.
Sasa baada ya UDINI kukwama, tunahamasishwa tuamini kuwa madhila yetu yanasababishwa na MA BEBERU ! Kama yapo, ni kidogo sana. Mengi ni matokeo ya kazi ya akili, matamanio na ubinafsi wa watawala wetu CCM...
Katiba tuliyonayo haikuandikwa Ulaya. Hakuna mzungu aliyeweka vifungu vinavyompa Rais mamlaka makubwa au vinavyokataza wananchi kuhoji matokeo ya uchaguzi mahakamani. CCM wenyewe walikataa mchakato wa KATIBA MPYA kwa UBINAFSI wao wenyewe na Raisi wa wakati ule Jakaya Mrisho KIKWETE...
Vile vile, sheria ya mafao kwa wenza wa viongozi, ukubwa wa Bunge, ongezeko la posho na safari, na matumizi makubwa ya magari ya kifahari; vyote hivi ni uamuzi wa watawala wetu CCM. Wananchi wakilalamika, wanaambiwa wametumwa na mabeberu. Huku ni kukwepa UWAJIBIKAJI kwa CCM.
Hata ubaguzi wa elimu—watoto wa viongozi kusoma shule bora na watoto wa wananchi kusukumwa kwenye shule za kata zisizo na miundombinu, si maagizo ya nje. Ni mfumo uliojengwa na CCM , unaochochea hasira na kukatisha tamaa vijana. Vivyo hivyo, tume ya uchaguzi iliyojaa shaka, misafara mikubwa ya viongozi, barabara kufungwa ili mkubwa wa CCM apite, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola si kazi ya mataifa ya nje. Ni CCM walioamua kuunda utamaduni wa kuwatukuza viongozi kuliko nchi yao.
Kwa miaka mingi, rushwa imeota mizizi kuanzia juu hadi chini. Hakuna mkoloni aliyeagiza tuibe asilimia 10 kwenye miradi ya serikali, tuidhinishe mikataba mibovu, au tuoneane aibu tunapopaswa kuwajibishana. Huu ni udhaifu wa CCM na taasisi zake ilizoziunda, si njama za nje wala mabeberu..
Aidha, MAUAJI , UTESAJI , watu KUTEKWA na KUPOTEA, yamekuwa majeraha ya taifa LETU, yaliyosababishwa na CCM bila kushinikizwa na taifa lolote kubwa. Hakuna beberu aliyeagiza polisi wawapige raia wanaodai haki au waue watu kana kwamba wanaua nzige shambani.
Maafa ya Oktoba 29 hayakupangwa na mabeberu. Bunduki zilizoangamiza Watanzania zilishikwa na Watanzania wenyewe; mipango ya mashambulizi ilifanywa ndani ya CCM na mfumo wao wa kihalifu. Ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, si maagizo ya nje. Tukitafuta mchawi nje, tutakuwa tunazidi kukwepa ukweli unaotakiwa kutuokoa.
Mwalimu anasema kwenye TUJISAHIHISHE..., “Sababu moja ambayo ilituzuia sisi Waafrika kuendelea ni majibu ya urahisi kwa matatizo makubwa. Shamba letu kama halikutoa mavuno ya kutosha, jibu lilikuwa wazi; au limelogwa au ni amri ya Mungu. Watoto wetu walipokuwa wagonjwa daima, jibu lilikuwa rahisi; au walilogwa au ni amri ya Mungu. Nyumba yetu ilipopigwa radi ikaanguka, jibu lilikuwa rahisi; au ni uchawi au ni amri ya Mungu. Majibu ya namna hii huzuia binadamu kupata sababu za kweli za matatizo yao, na kwa hiyo yanazuia akili kutafuta njia za kweli za kuondoa matatizo hayo.”
Kwa hiyo, tusikimbilie kuwalaumu mabeberu. Matatizo ya Tanzania yametengenezwa na Watanzania wenyewe na CCM yao.., ukombozi wake uko mikononi wetu sisi WATANZANIA, kwa kuwa wakweli, KULAZIMISHA CCM kubadili mifimo, kurekebisha tabia, na kuunda KATIBA MPYA itakayotoa majibu ya kudumu.
Tanzania mpya itapatikana siku ile ambayo VIONGOZI wa CCM watawaheshimu Watanzania wote na nchi yao Tanzania.
Kama kuna urithi mkubwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kutuachia watanzania, basi ni kutupatia KATIBA mpya, bora, shirikishi, itakayotupatia mihimili huru ya nchi, yaani BUNGE, MAHAKAMA, na SERIKALI itakayowajibika kwa watanzania.
Kwa KATIBA mpya, watanzania tutafumua na kujenga upya mifumo mibovu inayoliangamiza taifa.
Muda anao, afanye hivyo.
Manyerere J.N
Novemba 28, 2025