Manyara yaongoza kwa ukatili wa ukeketaji wanawake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa tatizo la ukatili wa ukeketaji nchini Tanzania bado ni kubwa kwani hakuna ripoti yoyote inayoonesha jamii fulani kuacha kabisa kufanya ukatili huo hivyo zinahitajika juhudi za pamoja miongoni mwa kijamii kukabiliana na ukatili huo.

Akiongea hii leo jijini Dar es salaam kuelekea siku ya ukeketaji duniani inayoadhimishwa hapo kesho kwa niaba ya waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na walemavu Ummy Mwalimu, katibu mkuu wa wizara hiyo Bi Sihaba Mkinga amesema kuwa mkoa wa Manyara unaongoza kwa kuwa na matukio mengine ya ukeketaji kwa asilimia 71 ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma kwa asilimia 64, Arusha asilimia 59 na Singida kwa asilimia 51.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto, UNICEF, linasema takribani wanawake na watoto milioni 200 wamekeketwa katika nchi thelathini duniani huku nusu yao wakifanyiwa vitendo hivyo katika nchi za Misri, Indonesia na Ethiopia.
 
Back
Top Bottom