Manufaa yatakayopatikana kupitia Mkataba wa Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DP WORLD ya Nchini Dubai

Jun 4, 2022
68
184
Ameeleza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

1. Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24. Hii itapunguza gharama za utumiaji wa Bandari yetu.

2. Kuongeza idadi ya meli zitazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33;

3. Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka siku 4.5 mpaka siku 2

4. Kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 kutokana na uboreshaji Wa mifumo yạ TEHAMA;

5. Kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka nchi za nje kwenda nchi za jirani, kwa mfano kutoka US$ 12,000 mpaka kati ya US$6,000 na US$7,000 kwa kasha linalokwenda nchi ya
Malawi, Zambia au DRC. Hii italeta Watumiaji wengi kwenye Bandari ya Dar es Salaam;

6. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka_tani milioni 18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani 47.57 mwaka 2032/33 sawa na ongezeko la asilimia 158,

7. Kuongezeka kwa Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya Forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi Trilioni 7.76 za mwaka 2021/22 hadi Shilingi Trilioni 26.70 za mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 244;

8. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 148;

9. Maboresho ya magati ya kuhudumia Majahazi na Abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitali zitakazo ongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la Taifa;

10. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer);

11. Uanzishaji wa maeneo huru ya kiuchumi na kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo: Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Utali; Viwanda na Biashara;

12. Kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; na kujenga mahusiano ya kidiplomasia.

Taifa Digital Forum
Mtazamo Halisi, Ufumbuzi wa Kweli.
10 Juni, 2022.
images (64).jpg
 
Ni manufaa mengi, nchi itakuwa kama dubai hii ilikuwa ndoto ya muda mrefu sana 🐒

 
Ni Emirates na sio dubai, ni sawa na kusema nchini Dar es Salaam au Mwanza, hiyo wrong mzee baba
 
Back
Top Bottom