Manufaa ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (Genetically Modified Organism) kwa Maendeleo ya Kilimo

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
3,023
Katika kitabu cha ‘Starved for Science, How Biotechnology is being kept out of Africa’ cha Mwandishi Robert Paarlberg kuna hoja nyingi juu ya kwanini wakulima wengi barani Afrika ni maskini kutokana na kupuuza teknolojia ya uhandisi Jeni.

Katika nchi yetu, wakulima wetu na jamii imepotoshwa kuhusu ukweli halisi wa uhandisi Jeni au Genetically Modified Organism. Hii inatokana na wananchi wengi kusikiliza hoja za upande mmoja ambazo hazina uthibitisho wa kitafiti wala kisayansi kuhusu faida za teknolojia hii. Inawezekana zipo sababu nyingi zinazosababisha hali hii zikiwemo uelewa mdogo wa wananchi kuhusu maana hasa ya teknolojia hii na uthibitisho wa kitafiti na kisayansi kuhusiana na ukweli wa teknolojia hii.Wananchi wasipoelimishwa maana na umuhimu wa teknolojia hii, inawezekana kabisa nchi yetu ikachelewa sana kufanya mapinduzi ya viwanda kupitia Tafiti,Sayansi na Teknolojia katika kilimo chetu.

Kwa muda sasa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia majukwaa mbalimbali yakiwemo Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania(OFAB) pamoja na wadau mbalimbali wa kilimo imekuwa ikifanya jitihada kuelimisha wananchi kuhusiana na faida za kutumia teknolojia ya uhandisi Jeni. COSTECH inafanya hivi kwakuwa imepewa mamlaka na Sheria No 7 ya Bunge ya Mwaka 1986 kuratibu na kuendeleza tafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu.

Pamoja na jitihada hizi za COSTECH na wadau wengine wa kilimo, changamoto inaonekana ni kubwa sana hususani kwa baadhi ya vikundi kupotosha maana halisi ya teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) kwamba teknolojia hii ina madhara kwa afya ya Binadamu.

Mtafiti anayeheshimika sana Duniani katika masuala ya utafiti na magonjwa ya Kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Mikocheni Dr Joseph Nduguru anabainisha kuwa teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) ni teknolojia ambayo ina lengo la kuongeza mavuno kwa mkulima. Anaeleza kuwa kinachofanyika katika teknolojia hiyo ni kutengeneza kinga kwa mmea au mfugo au ili usipate Mashambulizi ya magonjwa.

“Kinachofanyika kwenye teknolojia ya uhandisi Jeni hakina tofauti sana na teknolojia inayotumika wakati wa kutengeneza dawa ya Insulini kwa ajili ya wagonjwa wa Kisukari”analeza Dr Ndunguru.

Dr Ndunguru anatoa mfano wa ugonjwa wa mihogo ujulikanao kama Bato Bato ambao ameufanyia utafiti kwa kipindi kirefu. Anasema ugonjwa huo unasababishwa na aina fulani ya Kirusi aitwaye cassava mosaic virus ambaye huyafikia majani ya muhogo kupitia inzi wadogo weupe. Akizungumzia jinsi teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) inavyofanyika kwenye mihogo, Dr Ndunguru anasema kuwa kinachofanyika ni kuchukua mbegu ya muhogo na kuipandikizia aina ile ile ya kirusi ambayo huuathiri muhogo. Baada ya mchakato huo muhogo uliopandikiziwa ile DNA ya kile kirusi huwa na kinga na haiwezi tena kushambuliwa na aina ile ya Kirusi. Kwa maneno mengine muhogo ule uliofanyiwa uhandisi Jeni huwa imara kukabilina na aina ile ya ugonjwa wa Bato bato.

Teknolojia ya uhandisi Jeni ambayo imefanyiwa majaribio mengi katika Taasisi ya Kilimo ya Mikocheni ikihusisha wataalamu wengi kutoka mataifa makubwa Duniani imethibitisha kuwa mimea yote inayotokana na teknolojia hii haina madhara kwa Binadamu.

Juma Shaaban ambaye ni Mkulima wa mihogo huko Bagamoyo, Shamba lake limeathiriwa vibaya na aina hiyo ya virusi lakini hafahamu kama mihogo yake ina ugonjwa. Yeye anaamini tu kwamba majani ya mihogo yake yamekauka kutokana na ukame na ndiyo maana hupata mavuno kidogo ya mihogo.

Shina la Muhogo ulioathiriwa na virusi vya ugonjwa huo likikatwa na kupandwa sehemu nyingine bado hali ya ugonjwa huendelea kuwepo na kuambukiza eneo hilo pia.

Dr Ndunguru anaendelea kueleza kuwa virusi vinavyosababisha magonjwa ya mimea kama muhogo (cassava mosaic virus) havina madhara kwa binadamu na ndiyo maana kisamvu cha muhogo ulioathiriwa na ugonjwa wa bato bato huliwa na watu wengi bila kufahamu.

Professor Calistius Juma kutoka Chuo Kikuu cha Harvard Marekani, naye katika tafiti zake mbali mbali anaeleza kuwa teknolojia ya Uhandisi Jeni haina madhara kwa Afya ya Binadamu. Anaeleza kuwa nchi kama Afrika Kusini, Burkinafaso, Misri na Sudan zinatumia Teknolojia hii na kumekuwepo na ongezeko kubwa katika mazao.

Wakati nazungumza na mwanazuoni huyo, nilibaini kuwa nchi yetu imeweka utaratibu mzuri, tunaweza kabisa kutumia Uhandisi Jeni kwenye kilimo hususan maeneo ambayo hayana rutuba. Nchi ya India ni mfano wa mataifa ambayo yanazalisha pamba kwa wingi Duniani kuliko Tanzania pamoja na kuwa ardhi yao haina rutuba ya kutosha kama tuliyo nayo.

Watu wamekuwa wakijiuliza; kwanini teknolojia hii inapigwa vita sana na baadhi ya watu na Taasisi? Jibu ni rahisi tu, mbegu za mazao ambazo zimefanyiwa uhandisi Jeni zina kinga ambayo hustahimili magonjwa hivyo mkulima anaweza asitumie kabisa mbolea. Kwa maneno mengine, kama tukiruhusu sheria zetu zikubali moja kwa moja Uhandisi Jeni, kuna baadhi ya viwanda vitakosa soko na biashara ya baadhi ya mbolea inaweza kuharibika.

Katika baadhi ya mihadhara ambayo COSTECH ilikaribisha wataalamu kuelezea faida za Uhandisi Jeni, zimekuwa zikiibuliwa hoja ambazo hazina msingi wala ushahidi wa kisayansi. Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha umma kuwa mazao yatokanayo na uhandisi Jeni yana madhara kwa binadamu na ni mkakati wa nchi za magharibi kufanya biashara.

Hoja hizi ambazo hazina mashiko ya kitafiti wala kisayansi hazina msingi kwa kuwa hutolewa kutokana na sababu za kibiashara za kuhofia teknolojia hii inaweza kuua soko la viwanda vya pembejeo. Uhandisi Jeni ni teknolojia nzuri ambayo kama tutaitumia vizuri bila kukubali propaganda za baadhi ya vikundi vya watu vyenye matakwa yao ya kibiashara, inaweza kuharakisha zaidi maendeleo ya kilimo chetu na hatimaye kutusaidia katika mapinduzi makubwa ya viwanda na uchumi wa nchi yetu.

Teknolojia hii imekwishafanyiwa tafiti za kutosha na wataalamu wetu nchini wakiwemo wale wa Taasisi ya Kilimo ya Mikocheni. Tunaweza kabisa kufanya Uhandisi Jeni tukiwa hapa hapa nchini tena kwa kuhusisha mbegu zetu hizi hizi tulizo nazo. Uhandisi Jeni hauna maana ya kuchanganya mbegu mbili zenye asili tofauti na kuziweka pamoja ili kupata mbegu chotara. Uhandisi Jeni ni hali ya kupandikiza DNA ya kirusi cha ugonjwa flani unaoathiri mmea katika mmea husika ili kujenga kinga kwa mmea huo.
 
Week iliyopita hapa mlikuja tukawatwanga maswali mods wakawasaidia wakaikimbiza mada! poor COSTECH. MONSANTO AGENTS.

​ORGANIC IS A PASSION FOR LIFA.
 
Wito watanzania tutunze na tuendeleze mbegu zetu za asili,walitudanganya minazi mifupi matokeo yake wananchi wamekua tegemezi wa mbegu kwi miche isiyodumu
 
Mleta mada ebu pitia hiyo link hapo chini, alafu uje upya
Wa monsato and the likes hawataki kabisaa independent research juu ya long time side effects ya haya mambegu yao, wanacho ficha wanajua wao na shetani.
Kama wamekutuma wambie wawauzie wamarekani sisi watuache tuendelee na hizi hizi tulizo zizoea.

GMO Scandal: The Long Term Effects of Genetically Modified Food on Humans | Global Research

Good article mkuu! hivi unafikiri hawa wataalamu wetu vilaza wanasumbuka kutafuta facts? Wakipewa bahasha za kaki wanakurupuka kuhubiri wasiyoyajua! poor COSTECH.
 
Mleta mada ebu pitia hiyo link hapo chini, alafu uje upya
Wa monsato and the likes hawataki kabisaa independent research juu ya long time side effects ya haya mambegu yao, wanacho ficha wanajua wao na shetani.
Kama wamekutuma wambie wawauzie wamarekani sisi watuache tuendelee na hizi hizi tulizo zizoea.

GMO Scandal: The Long Term Effects of Genetically Modified Food on Humans | Global Research

Umoja wa ulaya waliokuwa wapinzani wakubwa wa matumizi ya uhandisi Jeni. Ripoti yao laya inayojuimisha miradi ya utafiti zaidi 130, iliyokuwa na lengo la kutathimini hatari/madhara yatokanayo na Mazao ya Uhandisi Jeni ( GMOs), kwa muda wa zaidi ya miaka 15 inatoa ushahidi na uthibitisho kuwa mazao ya uhandisi Jeni hayana madhara ya ziada ukilinganisha na mazao ya chakula cha kawaida. Unaweza kusoma ripoti hiyo ya Muongo wa utafiti uliofadhiliwa na umoja wa ulaya kujiridhisha kama wao walivyofanya:

EUROPA - PRESS RELEASES - Press release - Commission publishes compendium of results of EU-funded research on genetically modified crops
Since 1982, the European Commission has invested over €300 million on research on the bio safety of GMOs:

A decade of EU-funded GMO research (2001-2010):
Research - Biosociety - Library - Brochures & Reports

EC-sponsored research on Safety of Genetically Modified Organisms (1985-2000)
Research - Quality of Life - Genetically Modified Organisms - A Review of Results
 
Mkuu umeeleza sana faida,hebu tueleze japo kwa aya moja hasara za kudumu na za muda mfupi za GMO

Tafiti za kisayansi kwa bara la Marekani zilionyesha matokeo yasiyotarajiwa ya mazao ya Uhandisi Jeni (GMO) ni ya manufaa. Utafiti uliofanywa na Hutchison et al. (2010) iliyochapishwa katika jarida la Sayansi anaripoti kuwa Mahindi yaliyozalishwa kwa teknolojia ya Uhandisi Jeni, yalitumia kemikali kidogo ukilinganisha na yale yaliyozalishwa kwa teknolojia ya ya kawaida.
Areawide Suppression of European Corn Borer with Bt Maize Reaps Savings to Non-Bt Maize Growers

Nchini China ambapo wanasalisha pamba kwa iliyoimarisha kwa teknolojia ya uhandisi jeni (Bt Cotton) ulipunguza kwa kiasi kikubwa viwavi "pink bollworm" vinavyoharibu zao hilo (Wan et al., 2010). PLOS ONE: The Halo Effect: Suppression of Pink Bollworm on Non-Bt Cotton by Bt Cotton in China

Mapitio ya tathimini ya madhara ya kiafya ya mazao ya uhandisi jeni "GMO" na mazao ya kawaida na kuchapisha matokeo katika jarida la Chakula na kemikali/sumu, yalidhihirisha kuwa mazao ya GM yanayolimwa kwasasa na mazao yasiyo ya GM yana madhara sawa kwa afya ya binadamu. Kwa maneno mengine, mazao ya GM na yasiyo ya GM hayana tofauti ya kilishe na mzio " allergic" kwa mlaji ( Snell et al. 2012).
Assessment of the health impact of GM plant diets in long-term and multigenerational animal feeding trials: A literature review
 
Umoja wa ulaya waliokuwa wapinzani wakubwa wa matumizi ya uhandisi Jeni. Ripoti yao laya inayojuimisha miradi ya utafiti zaidi 130, iliyokuwa na lengo la kutathimini hatari/madhara yatokanayo na Mazao ya Uhandisi Jeni ( GMOs), kwa muda wa zaidi ya miaka 15 inatoa ushahidi na uthibitisho kuwa mazao ya uhandisi Jeni hayana madhara ya ziada ukilinganisha na mazao ya chakula cha kawaida. Unaweza kusoma ripoti hiyo ya Muongo wa utafiti uliofadhiliwa na umoja wa ulaya kujiridhisha kama wao walivyofanya:

EUROPA - PRESS RELEASES - Press release - Commission publishes compendium of results of EU-funded research on genetically modified crops

Since 1982, the European Commission has invested over €300 million on research on the bio safety of GMOs:
EUROPA - PRESS RELEASES - Press release - Commission publishes compendium of results of EU-funded research on genetically modified crops
A decade of EU-funded GMO research (2001-2010):

Research - Biosociety - Library - Brochures & Reports

EC-sponsored research on Safety of Genetically Modified Organisms (1985-2000)
Research - Quality of Life - Genetically Modified Organisms - A Review of Results

Tafiti za kisayansi kwa bara la Marekani zilionyesha matokeo yasiyotarajiwa ya mazao ya Uhandisi Jeni (GMO) ni ya manufaa. Utafiti uliofanywa na Hutchison et al. (2010) iliyochapishwa katika jarida la Sayansi anaripoti kuwa Mahindi yaliyozalishwa kwa teknolojia ya Uhandisi Jeni, yalitumia kemikali kidogo ukilinganisha na yale yaliyozalishwa kwa teknolojia ya ya kawaida.

Areawide Suppression of European Corn Borer with Bt Maize Reaps Savings to Non-Bt Maize Growers

Nchini China ambapo wanasalisha pamba kwa iliyoimarisha kwa teknolojia ya uhandisi jeni (Bt Cotton) ulipunguza kwa kiasi kikubwa viwavi “pink bollworm” vinavyoharibu zao hilo (Wan et al., 2010). PLOS ONE: The Halo Effect: Suppression of Pink Bollworm on Non-Bt Cotton by Bt Cotton in China

Mapitio ya tathimini ya madhara ya kiafya ya mazao ya uhandisi jeni “GMO” na mazao ya kawaida na kuchapisha matokeo katika jarida la Chakula na kemikali/sumu, yalidhihirisha kuwa mazao ya GM yanayolimwa kwasasa na mazao yasiyo ya GM yana madhara sawa kwa afya ya binadamu. Kwa maneno mengine, mazao ya GM na yasiyo ya GM hayana tofauti ya kilishe na mzio “ allergic” kwa mlaji ( Snell et al. 2012).

Assessment of the health impact of GM plant diets in long-term and multigenerational animal feeding trials: A literature review
 
@ banana atutakuwa watumwa wa mbegu za the so called MONSANTO. Hicho unachokisema ni kuingizana choo cha kike kwa sisi akina yae! kwa nini wao EU wameweka sheria kuwa kila product inayouzwa kwa kutumia malighafi za GMO lazima ziwe labelled ili consumer ajipime na aamue kununua after wasting a lot of that fund in research?

TAKARI!! Period
 
Mara yangu ya kwanza kusikia MOSANTO, niltafakari sana. Nilipata picha kama kuambiwa ISRAEL anakuja kukutoa roho. Niliamua kumtembelea google.. Wikipedia akaniambia vizuri mosanto ni nini. Nilshangaa sana kuona kampuni ndogo kuliko ya huyu bwana wa makompyuta "bill gate". Ni ndogo kuliko hata makampuni ya kutengeneza simu, kampuni ndogo kuliko hawa jamaa wanaotengeneza dawa tunazonunua famasi ndo imefanywa tishio. Hadi sasa sielewe kwanini mosanto imekuwa kuchaka cha kuzuia sayansi na teknolojia. Hebu tutumie mfano wa mtoa mada..Hivi kweli mosanto ana mbegu ya mihogo ya kitanzania atakayokuja kuuza kwetu? mosanto ndo analipa mishahara watafiti wa kituo cha umma cha mikocheni? Mosanto amewalipia karo vijana waliomaliza pale SUA na mlimani ambao hivi sasa ndo wanafanya utafti wa mihogo? Ndugu yangu, mikocheni inaendeshwa kwa kodi ya mkulima wa Tanzania. Watafti wote wa uhandisi jeni wa zao la mihogo wamesoma tz kwa mikopo ya umma, na wengi ni watoto wa wakulima. Mosanto hana hisa pale. Ni bora tupinge kampuni kama Nokia.. Kuliko kuzuia watanzania wenzetu kutatua matatizo ya wakulima kwa kisingizio cha mosanto.
 
@ banana atutakuwa watumwa wa mbegu za the so called MONSANTO. Hicho unachokisema ni kuingizana choo cha kike kwa sisi akina yae! kwa nini wao EU wameweka sheria kuwa kila product inayouzwa kwa kutumia malighafi za GMO lazima ziwe labelled ili consumer ajipime na aamue kununua after wasting a lot of that fund in research?

TAKARI!! Period

Suala la kuandka kuwa bidhaa hii ni matokeo ya uhandisi jeni <GMO> au la, ni suala la kidemokrasia zaidi. Linatoa uhuru kwa mlaji kuchagua anayotaka kula, kama tunavyoandika unga wa mahindi, unga wa ngano, mchele wa kyela, mchele wa kilombero, n.k. Mkulima apewe uhuru wa kulima GMO au mazao ya kawaida, na mlaji uhuru wa kujua anachokula.
 
Majuzi nilisoma gazeti moja likimnukuu Dr. Mshinda (spelling) kutoka COSTECH kuhusu haya mambo ya GMO akisema Tz hatuna policy au Act kuhusu GMO. Lakini nanenane ya mwaka huu ktk pitapita zangu niliona banda la Monsanto live bila chenga. Yani hii nchi ni kama hakuna serikali.

Ni wazi unapobadilisha vinasaba kuondoa upungufu fulani haimaanishi kua hakuna madhara, na kwa sababu makampuni yanayotengeneza vinasaba ni ya kibiashara yapo radhi kuhonga regulatory bodies ku-skip kufanya tafiti kuhusu madhara ya hizo products zao. Suala la kusema eti kuna wauza mbolea wanapiga vita GMO nadhani hiyo ni nonsense. Hata hiyo productivity wanayodai inaongezwa na matumizi ya GMOs nayo ni kiinimacho. DOI:10.1080/14735903.2013.806408
 
Mkuu Salute! Kuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa sustainable agriculture ndo njia pekee ya kulisha dunia kama hilo journal linavyojibainisha!

GM na synthetic fertilizer kama akina banana wanavyotaka kutuaminisha watashindwa!

ORGANIC IS A PASSION FOR LIFE.
 
Sikubahatika kusoma gazeti hilo. Ila kuhusu sera, sheria na kanuni, ukweli ni kwamba zipo. Kuna kanuni za usimamizi salama ya teknolojia ya uhandisi jeni ya 2009, sheria ya usimamizi wa mazingira, kifungu 69 na sera ya taifa ya mazingira ya 1997, na kuna miongozo mitatu ya kitaalam yote ya mwaka 2010.

Na suala la kuongeza tija kama ni kiini macho, basi hatuna haja ya kuogopa GMO maana wakulima watazikataa kama wanavyofanya kwa mbegu zingine zisizo na tija.
 
Ndugu Kajansi, sina sababu ya kujaribu kuhadaa watanzania kuwa kuna njia moja na ya pekee kuondoa matatizo ya uzalishaji katika sekta ya kilimo. Si hata kwa wilaya moja, achia mbali nchi na dunia kama unavyopigia debe kilimo endelevu. Wakulima wa Tanzania ni mashahidi na wanao ushahidi wa matokeo ya kilimo asili, kilimo endelevu, kilimo hai n.k. Sitaki kubeza teknolojia zingine... ila nililazimika kuchangia kwenye mada hii kutoka na ukweli kuwa kuna watu wanatumia nguvu nyingi sana kupotosha ukweli kuhusu teknolojia ya uhandisi jeni. Inashangaza unasoma gazeti, limeandika Kilimo cha GMO kimeharibi udongo Bagamoyo....wakati hakuna mahali Tanzania wanalima GMO, mara kilimo cha GMO kumeshusha uzalishaji wa pamba..... wakati Tanzania hakuna pamba ya GMO, tunaambiwa GMO inashusha uzalishaji,... wakulima wakataa GMO Tanzania...hatusemi nani kawapa au inapatikana wapi? Unakuta nukuu " Kilimo cha GMO kilipigwa marafuku Tanzania, mara tu baada ya nchi kupata uhuru". Wakati kilimo hicho kimeanza miaka ya 90, Tanzania ikiwa nchi huru. SWALI LA KUTAFAKARI NI KWANINI MTU AU KUNDI LA WATU LINALAZIMIKA KUSEMA UONGO KAMA HUU? KWA MASLAHI YA NANI?

Tuwape watanzania hasa wakulima taarifa sahihi... Tanzania hakuna GMO, majaribio ya teknolojia yapo kwenye ngazi ya maabara kwa zao la mihogo,katika kituo cha utafiti cha umma Mikocheni. Watanzania ndo wanafanya utafiti huo, waliosoma kwa mkopo wa wakulima. Na kama matokeo yakiwa mazuri na kupitia tathimini zote za uhakiki kwa afya, mazingira, ufanisi wa kupambana na magonjwa na kuongeza uzalishaji..basi wakulima wa Tanzania watapata mihogo hiyo kwa njia za kawaida kama ilivosasa.

Tuwambie teknolojia ya uhandisi jeni ni moja ya teknolojia ya kilimo ambazo wanaweza kutumia, na si teknolojia inayokuja kuondoa aina nyingine za uzalishaji, wala kuondoa mbegu za asili... kama ilivyo tunaponunua trekta hatutupi jembe. Kilimo hai au endelevu hakijaondoa kilimo cha asili...

Wakulima wanaopenda kulima GMO kipindi zitakapokuwepo Tanzania wawe huru kufanya hivo. Na pale watakapolinganisha matokeo GMO na kilimo endelevu wataamua watumia mfumo upi. Ukweli utawaweka huru..na utatuweka huru pia.:wave:
 
Asante sana banana kwa kuonyesha positivity!

Banana ni kweli hakuna GMO Tanzania lakini tunajifunza kwa wenzetu hasa India ambapo GMO seeds zimewafanya kuwa watumwa wa wazalishaji wa mbegu! Yaani uniuzie mbegu then nizalishe nitunze kwa ajili ya msimu ujao tahamaki hazifai! kweli wakulima wetu maskini wataweza?

Staki kufikiri kuwa muhogo wa Dk. Ndunguru utakuwa hivyo!!!

Mkuu sustainable Agriculture haijashindwa hapa nchni bali ni sera mbovu na ufisadi wa madaraka hapa nchini!. Nikisema ufisadi walio wengi watakimbilia kwenye kuiba pesa! NO. nazungumzia ufisadi wa watendaji eg afisa ugani ambaye awetembelei wakulima wake na kubaini matatizo yao.

Banana hivi unajua kuwa kutengeneza mbolea ya mboji (composite) ni rahisi sana kwa wakulima wetu na haitji ujuzi bali kumwelekeza mkulima tu then anafanya!

Udongo wetu hapa Tanzania hauna matatizo makubwa issue ni soil cover which can be solved by compositing basi!
Does this need ufadhili???

Hivi unafahamu nutrient intake ya GMO plants? nakuhakikishia wakulima wetu watakuwa watumwa wa synthetic fertilizer na kwa bahati mbya hapa hazizalishwi na zikizalishwa ni skendo kibao ref. MINJINGU.

Iam resting my case!
 
Mazee wanataka tuwe mawakala wa mbegu zo milele. Mimi nitajhamsicha mbegu za asili kuliko hizi.
 
Umetumwa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee aaaaaaaaacha umbuluuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuula, technologia ya GMO ni ya hali ya juu sana na haiongezi uzalishaji wa chakula tafadhali fanya utafiti wewe uliyelogwa na wazungu sijui utajikomboa lini utumwani COSTECH wanatakiwa wafanye tafiti za kitanzania katika mazingira ya kitanzania sio kuletewa technologia.
 
Back
Top Bottom