Manufaa ya kujiajiri mwenyewe

Mavoko R

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Vijana wengi, huwa tuna mawazo ya kuwa chini ya watu(kuajiriwa) tunasahau kwamba unapoajiliwa maana ake unabadilisha muda wako maarifa, na ujuzi wako kwa aliekuajili kwa sababu una produce kwa ajil ya faida yake hivo still, wewe nikama mtumwa.

Huwa najiuliza kwanini watu walioajiliwa huwa ni ngumu kuwa miongon mwa matajiri wakubwa, nikagundua , wanauza maarifa na muda wao kwa walee waliowaajiri hivo, kutengeneza nafasi kubwa ya ukandamizaji, always hakuna mtu ambae kakauajili anawez kubali uwee na mafanikio kuliko yeye so tegemea, kubaki palepale

Unapojiajiri mwenyewe, unatengeneza creative(ubunifu)kwa sababu hicho unachokifanya ndicho unataka kikunufaishe na kukutambulisha, I am sure lazima utakuwa na uchungu nacho, utambana usiku na mchana , , namn gani, kiwe bora zaidi, nakiweze kuingia kwenye viwango vya soko la kuvutia wateja wengi zaidi

Nimeandika kwa ufupi

HR
 
Hili somo huwa halieleweki kwa watanzania. Ushahidi: angalia idadi ya wachangiaji kwenye uzi huu. Uko sahihi kwa asilimia zaidi ya mia.😂
 
Naona watu wanajichanganyaga kujiajiri na kuajiiriwa. Nikiwa na maarifa ukaniajiri ivyo mtaji wangu Ni hayo maarifa ndio nimejiajiri nayo.

Mie Ni daktari ivyo yananilipa mie ama na trade maarifa yangu na money. Ukiwa na tax ama hiace una trade mtaji wako na wateja. The end product is the same. Sasa unamuongelea aliyesoma na je ambaye Ni kibarua kwa kiwanda Cha no Hana maarifa analipwa 5k per day. Unamchukuliaje ama unamsaidiaje apate angalau milioni kumi.

Inabidi ifikie hatua ukubali tofauti zetu zilizopo Mana tokea Billions of years dunia hajawahi change always Kuna matajiri wafanyakazi vibarua na watumwa.

Aliyeumba dunia ama Mana yake. Hebu mwambie mwafrika apambane amzidi mzungu kama hatakuambia kuwa namridhisha mke wangu kitandani ndio heshima pekee.
 
Hili somo huwa halieleweki kwa watanzania. Ushahidi: angalia idadi ya wachangiaji kwenye uzi huu. Uko sahihi kwa asilimia zaidi ya mia.😂
Uko sahihi, na vilevile watanzania ambao hili somo hawalielewi nao wako sahihi!

Mimi nimeshaacha kuwapa watu ushauri wa kujiajiri. Kumshauri mtu ajiajiri ilihali ana sifa za kuajiriwa ni kumpoteza kwa sababu, he wont have what it takes to be an entrepreneur.

Kujiajiri ni kazi ngumu sana, kuajiriwa ni rahisi sana, ukishaajiriwa, wewe ni kwenda tu kusaini kwenye kituo chako cha kazi, muda ukifika wa kutoka unasaini out, unasubiri mshahara mwisho wa mwezi. Huumizi kichwa, huhitaji ķuwa mbunifu wala mvumilivu, wewe ni kwenda kazini tu na kufanya ambacho bosi wako anataka, very simple. Kujiajiri ni habari nyingine.

Mimi niliacha kazi ili nijiajiri, changamoto nilizopitia nisingependa mwingine azipitie, After all, watu wengi wanaridhika akiwa na nyumba kisha akanunua na ka premio ka kuendea kazini. Kama kuajiriwa kunaweza kumpatia hayo, kwa nini aumize kichwa?, atuache tuliojitoa mhanga tupambane..

Nimejaribu kuandika kwa kifupi sababu muda ni mali, nikizingatia pia kuwa wengi hawawezi kusoma habari ndefu.

 
Mimi ni miongoni mwa watu wenye kiu kubwa sana ya kujiajiri...

Hakika.... Nimefungua hadi Business Name... Tatizo ni mitaji....


Yaani... Basi tu....

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni miongoni mwa watu wenye kiu kubwa sana ya kujiajiri...

Hakika.... Nimefungua hadi Business Name... Tatizo ni mitaji....


Yaani... Basi tu....

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Business name ya nn? Mitaji ni uanzie ulicho nacho! Kama unadham ukipata kikubwa ndo unatakiwa uanze basi nakushauri baki ajirani
 
Ni rahisi kusema kuliko kutenda,
Kujiajiri sio Sawa na kwenda mlimani city kupiga selfie!!
Vijana wengi walioajiliwa migodini,au sehemu ambapo wanalipwa,2M+ net,wengi Wana vikampuni,ambavyo na wao wameajiri watu,hii nimeiona migodini,mtu anatoka kuwa na lodge kama saba! Hata vunja bei alianziq wizarani akapiga kazi,leo amejiajiri,watu ishu za kutokea wanazijua,tatizo unaanza vipi wakati pesa hakuna,haitoshi?
Kuna kampuni za uhandisi zipo hapa mjini,BV engineering,Horizon,wanaozimiriki walianza kazi kati. Ya 1998,au 2000,lakini walikuja kuweza kujiajiri baada ya miaka 17! 2017,ni baada ya kulipwa pesa ndefu,kampuni walizokuwa wanafanya kazi zilipovunja mikataba,wakati JPM kaingia,sasa Swala la kujiajiri sio rahisi unless wewe unauhusiano na familia ya Raisi,kama kujiajiri ni rahisi,inakuaje mtu aliyekuwa Mbunge na waziri kwa miaka zaidi ya 15!akipoteza ubunge tu,anapigika balaa,mpaka mamlaka za juu,zimuonee huruma zimpe ukuu wa wilaya au mkoa,
Unaanzia wapi utoke chuo,harafu ukajiajiri,hata kama ni bodaboda,hiyo 2.5M unatoa wapi,harafu upige boda,Uzichange,ujenge nyumba upangishe,ununue ist uifanye Uber,ulime matikiti uuze ulaya,ukalime mpunga na mahindi uuze Kenya,vyote hivi uvifanye kwa vipesa vya boom!,harafu mala paap,ununue Prado na nyumba goba!
Huu utakuwa miujiza kuliko yote!!!
 
Motivesheni supika WA kibongo wanaongea kirahisi rahisi Sana , kujiajiri ni tough issue , ni ngumu hasa tena hizi nchi zetu za KiAfrica zilizo na mifumo mibovu na corruption ndio kabisa , unalima let's say Kahawa halafu unalazimidhwa uuze kwenye ushirika hapo pia unakopwa hiyo pesa ikitoka umeshajaa madeni kibao inaishia kulipa madeni Tu ,hasara kwenda mbele ,malipo usubiri miezi kadhaa ijayo yet kuna soko la uhakika nchi jirani hapo ,serikali wanakataza kuvukisha border ,

Ndio Maana kuna usemi kwamba kutoboa hasa nchi hizi za dunia ya tatu , you have got to be a crook . Kuna ukweli kiasi kikubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…