Manuel Neuer Anatarajia Kustaafu Soka Msimu Huu

Manuel Neuer Anatarajia Kustaafu Soka Msimu Huu

Jemat

Member
Joined
Nov 9, 2026
Posts
79
Reaction score
219
Kipa mkongwe na nahodha wa Bayern Munich, Manuel Neuer (40), anatarajiwa kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu wa 2026/27 mkataba wake utakapomalizika.

Kutokana na taarifa hizo ambazo zinachagizwa na jeraha la misuli ya mguu linalomkabili kwa sasa, mabingwa hao wa Ujerumani tayari wameanza mchakato wa kutafuta kipa mpya namba mbili atakayemsaidia chipukizi Jonas Urbig, ambaye anaandaliwa kurithi mikoba ya Neuer.

Neuer alisajiliwa na Bayern Munich mwaka 2011 akitokea Schalke 04, na hadi sasa ameshaitumikia timu hiyo katika mechi zaidi ya 605 za mashindano yote.

Katika kipindi chake chote klabuni hapo, amefanikiwa kubeba mataji 32, yakiwemo mataji 26 ya ndani ya Ujerumani (mataji 13 ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani ‘DFB-Pokal’ mara 6, na DFL-Supercup mara 7) pamoja na mataji 6 ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 2, UEFA Super Cup mara 2, na Klabu Bingwa ya Dunia mara 2).

Cha kushangaza, Ronaldo hajawahi kucheza Bundesliga lakini ndiye kinara wa Wafungaji dhidi ya Neuer! 😳

⚽ Wafungaji wengi dhidi ya Neuer:

🇵🇹 Cristiano Ronaldo — Magoli 10
🇩🇪 Marco Reus — Magoli 8
🇭🇷 Andrej Kramarić — Magoli 7
🇵🇱 Robert Lewandowski — Magoli 7
🇩🇪 Stefan Kießling — Magoli 6
🇦🇹 Martin Harnik — Magoli 6

🐐 Ronaldo ni mwiba kwa Neuer! 🔥😁😁
 
Sio vya kucheka mkuu, hadi kuna muda natamani kuwa pekeyangu nisiwe na watu wa karibu.
Afrika mazingira ya kusoma ramani ni bahati na connection mkuu hauko peke yako ni swala la kukubali mazingira na kuendelea kupambana sio eti ukae peke yako kisa nini..
 
Back
Top Bottom