Mantiki ya tuhuma za Sitta kuhusu CDM na mbio za Urais CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mantiki ya tuhuma za Sitta kuhusu CDM na mbio za Urais CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Sep 3, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kauli za hivi karibuni za Mh Sitta kuhusu uongozi wa CDM zinaonyesha Sitta hakukurupuka kutoa kauli zile kwani backlash yake alikua anaijua na inaonekana hakuidharau hata kidogo na ndiyo maana amejibu zile counter accusation zilizorushwa na Dr Slaa kwa mara moja. Hii yote inanipa ishara kwamba katika kuwania Urais kupitia CCM, viongozi waandamizi CCM kama Mh Sitta wanakuja na mikakati tofauti ya kuonekana wao ndiyo wanafaa kupewa ridhaa ya wana CCM kwenye chaguzi mkuu wa 2015.

  Huku Mh Lowassa akiwa anatumia muda huu kumulika kichini chini udhaifu wa JK kwa kusema stark policy objectives, Mh Sitta ambaye nae anapewa nafasi kubwa ndani ya CCM ameamua kuvuka mipaka na kuonyesha wana CCM kwamba yeye ndiye anayefaa kuchuana na mgombea wa CDM kwa kuonyesha kutokua na woga wa kukishambulia chama hiko kinachohatarisha maisha ya CCM kwenye siasa kwa sasa.

  Hii inampa nguvu Mh Sitta kuonyesha kua yeye hana cha kuficha na kama CCM inataka kuendelea kushika dola basi kati yake yeye na Mh Lowassa yeye ana nafasi zaidi ya kupita kwa wananchi kwani CDM hawatakua na la kumsema zaidi ya yale waliyoonyesha na ukiachailia hilo anaweza kwenda hatua kwa hatua na makamanda wa CDM kwa tuhuma dhidi ya tuhuma bila kuharibu image yake kisiasa tofauti na wagombea wengine ndani ya chama chake.

  Kama CDM itazidi kuongeza nguvu kwa wananchi kwa kasi kubwa kuelekea 2015 hii italazimisha uchaguzi wa ndani ya CCM kua wa kuweka mgombea anayeonekana atamshinda yule wa CDM (kwa kuweka mtu aliye maarufu, lakini mwenye vulnerability ndogo ya kutupiwa tuhuma na CDM..na hapa Mh Sitta atakua amefanyikiwa katika hili kutokana na tuhuma dhidi yake kutokua na impact haswa kwa wananchi (tuhuma za kuhamia upinzani zinaweza kua siyo mbaya kwa wapiga kura wana CCM waliokichoka chama chao, na wananchi wengi wasiokua mashabiki wa moja kwa moja wa vyama vya siasa nchini). Wagombea wengi wa CCM watashindwa kusimama na dhoruba ya tuhuma zitakazoletwa kwao toka CDM. Na hapa Sitta ameonyesha kua ni makini katika mikakati.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  sitta ana tuhuma nyingi tu:
  1.ofisi ya bunge kujengwa urambo wakati hakuna guarantee ya spika kutoka tabora miaka yote
  2.kuizima hoja ya richmond kihuni ili kulinda serikali fisadi..eti asingeizima ile hoja angenyang'anywa kadi ya ccm..rubbish
  3.kung'ang'ania nyumba ya spika wakati yeye sio spika
  4.kuasisi ccj akiwa bado ccm
  5.ni mwanamtandao,kundi moja na lowassa na jk ila alizidiwa ujanja mgao wa richmond..huwezi kuwaamini wanamtandao sababu wameshaonyesha udhaifu
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mtauana magama na uraisi!!!sasa sijui polis watamsaidia nani????naisubiri hiyio siku.tumeona bastola tunasubiti watu kuingia nec na vifaru!!!mpo juu ya sheria mnayo haki ya kuvimiliki wezi wakubwa nyie.
   
Loading...