Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,626
Mkubwa wa nchi ameshaweka makatazo mengi, in the name of kubana matumizi. Sura ya hoja hiyo wala haikua mbaya. Lakini mantiki ya ubanaji matumizi huo inaanza kupotea pale unaposhuhudia kuwa ubanaji matumizi unafanyika, kweli hela inaadimika lakini mipango yenye manufaa ya kuonyesha mantiki kwenye ubanaji huo inakosekana kwa kuingiza matumizi holela ambayo hata hayapo kwenye mipango na zaidi ni aina nyingine ya matumizi ya hovyo na holela.
Kilichonisukuma hata kuliona hili ni baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza maadhimisho ya siku ya mapinduko yakifanyika sehemu zaidi ya moja, yaani kule kwingine na kule Zenji. Sehemu zote mbili ambazo maazimisho hayo yalifanyika tumeshuhudia yakiwakilishwa na ujumbe mzito kule kwingine kwenye ule mkoa alikuwepo rais Mwenyewe Pogba, wakati kule kwingine katika viwanja visivyo na vurugu ulikuwepo ujumbe mwingine mzito sana wa wale wengine wastaafu wakiongozwa na huyu wa sasa wa jecha.
Nimejiuliza sana kuhusu ulazima wa kuongeza venue za kufanya maazimisho hayo wakati tupo katika kipindi cha ubanaji matumizi kilichosababisha mambo na taratibu nyingi kusimamishwa. Wakati wana kaya wanalia kwa sababu mbalimbali zinazoashiria dhiki walichoambulia ni masimango, na kile tunachoweza kuita 'matusi' kutoka kwa kiongozi wao. Haiingii akilini kabisa kuona matukio yale yale yaliyoonekana kuwa yanamaliza hela zetu, eti baada ya ku save sasa yanapewa uwanja mpana zaidi wa kutumia pesa na muda.
Kwa yeyote yule ambaye kwa sasa ni master mind wa mkuu anapaswa kujifikiria kama anastahili kuendelea kuwepo katika nafasi hiyo ya kumshauri mkuu. Napenda kumaliza andiko langu kwa kuwakumbusha viongozi wastaafu kwamba kwa mujibu wa nyakati tulizo nazo sasa na ushindani uliopo baina ya mataifa, watambue kuwa the parting time is over, it's a high time now they get back to business. Tuna rais anayeweza kusimamia maaumuzi yake bila ya kujali kelele za watu, sasa mumuonyeshe nini taifa linataka ili asimamie bila kujali kelele za watu badala ya kugeuza hisia zake kuwa ndiyo mahitaji na maslahi ya taifa.
Ni rais mzuri anahitaji miongozo kadhaa wa kadhaa ili aweze kuliweka taifa pamoja kwa ustawi wa muda mrefu. Kama hatushirikishani basi tunagawanywa na bila ya kushirikishana tutakuwa tunadanganyana kama ilivyo kawaida yetu. Amechaguliwa ili kusimamia ujenzi wa taifa si kwa ajili ya ujenzi wa personality yake.Huwezi ukajenga personality yako bali itajengwa na legacy.
Naomba kuwasilisha.