"MANQOBA NI KOCHA MZURI" BIN KAZUMALI

"MANQOBA NI KOCHA MZURI" BIN KAZUMALI

Joined
Oct 18, 2026
Posts
31
Reaction score
31
"Yanga SC hawako sawa, kuna sehemu ina shida binafsi sidhani shida ni Kocha wao. Nimejiuliza kama wachezaji wanapata nafasi namna hii na hawafungi Kocha unataka afanyaje?

Leo walikuwa na uwezo wa kuweka rekodi ya kushinda mabao mengi ugenini hatakama ugenini kwenyewe ingekuwa Madagascar ya Chamazi, lakini msingi ni nini kipo nyuma ya hiki kinachoonekana kwa wachezaji wa Yanga? Hapo Shalulie alishakosa na yeye kwenye hicho kipindi cha kwanza, fikiria mapochi hayo unasema Kocha ana shida.

Timu ingefunga kwenye hizi nafasi wangeenda halftime walau na bao 3, lakini walienda na 0-1. Viongozi wanaapaswa kufanya kazi yao sio kuacha tu watu wanatafuta sababu rahisi ya Kocha hana uwezo, lakini benchi la ufundi nalo lifanye tathmini, lichukue hatua.

Group Stage hakujawahi kuwa kwepesi hizi timu kama CFFA mbovu kwa kiasi hiki zinaishia huku huku mara nyingi.

Ruhusuni maoni kutoka nje ya waliowazunguka na chawa hatakama yatakuwa yanakera lakini kama yanawapa kitu cha kukifikiria chukueni fanyieni kazi, kuliko kutaka kusifiwa tu."

AMESEMA MCHAMBUZI WA SOKA, BIN KAZUMARI

Je, NIUPI MTAZAMO WAKO KATIKA HILI ?
 
Nadhani changamoto ni kutokujiamini kwa wachezaji sijui imekuaje. Au kama sio hivyo, basi wameshalogwa na timu pinzani maana wanasifika kwa uchawi
 
Nadhani changamoto ni kutokujiamini kwa wachezaji sijui imekuaje. Au kama sio hivyo, basi wameshalogwa na timu pinzani maana wanasifika kwa uchawi
Huyu mganga hii 5 years nyuma alikua hajazaliwa?
 
Back
Top Bottom