Kocha wa Azam aliyetimuliwa atema nyongo, amtupia lawama Saad Kawemba

Keng'oni

Senior Member
Dec 30, 2013
179
250
Na Saleh Ally

JUMATANO hii, uongozi wa Azam FC ulitangaza kumfuta kazi kocha wake mkuu Zeben Hernandez.

Kama haitoshi ikawafuta kazi Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa Tiba za Viungo, Sergio Perez, wote hawa ni raia wa Hispania.

Uamuzi wa Azam FC kuwafuta kazi Wahispania hao ni kwamba, wameshindwa kuipa timu hiyo matokeo mazuri baada ya mechi 17 za Ligi Kuu Bara ikawa imeshinda saba, sare sita na kupoteza nne.

Uamuzi wa Azam FC kuwafuta kazi umetolewa baada ya makocha hao kwenda sare mbili mfululizo katika mzunguko wa pili, wakianza sare ya bao 0-0 dhidi ya African Lyon, halafu 1-1 dhidi ya Majimaji mjini Songea, zote zikiwa ni za ugenini.Kabla hajakusanya virago vyake na kurejea kwao Tenerife nchini Hispania, SALEHJEMBE ilifanya juhudi za kuwapata makocha hao na kuzungumza nao kwa lengo la kujua walichojifunza katika soka nchini na kipi hasa kilichowafanya kushindwa.

SALEHJEMBE: Pole, naamini ni safari za kimaisha.

Zeben: Kabisa, katika soka hili si geni, ingawa tumeumia sana.

SALEHJEMBE: Kipi hasa kimekuumiza?

Zeben: Mimi na wenzangu, tulianza kuamini kwamba sasa timu inakwenda kwa namna tunavyotaka, lakini ndiyo wameniondoa!

SALEHJEMBE: Kwani kabla haikuwa mnavyotaka?

Zeben: Kabisa! Kuna mambo mengi sana yalikuwa magumu kwangu. Kuanzia wiki mbili zilizopita, hali ilikuwa imetulia na tulianza kufanya kazi kwa amani.

SALEHJEMBE: Unaweza kueleza mambo ambayo hayakuwa yametulia?

Zeben: Nilifanya kazi kwa wakati mgumu sana, hasa kipindi cha usajili. Mimi nilitaka mchezaji huyu, kiongozi akaleta yule na baadaye kukawa na shinikizo la kuwasainisha.SALEHJEMBE: Ulisainisha wangapi kwa shinikizo na kiongozi huyo ni yupi, mmoja wa watoto wa Bakhresa?

Zeben: Watoto wa Bakhresa hawakuwa wakiingilia mambo yetu. Wako viongozi wamekabidhiwa majukumu ya kuisukuma Azam mbele, lakini ni tatizo. Wakati mwingine kila siku ya mechi, kiongozi anataka umpe kikosi saa 4 asubuhi. Ukimpa tu, anaanza kupangua, huyu abaki, huyu apangwe!

SALEHJEMBE: Uliripoti hilo kwa waajiri wako?

Zeben: Viongozi ndiyo waajiri wangu, na wao ndiyo walikuwa wakifanya mambo ya kujiangusha. Acha kuingilia kikosi, kwenye usajili ndiyo ilikuwa shida kubwa kabisa.

SALEHJEMBE: Ukubwa wa hiyo shida ulitokana na nini?

Zeben: Nilisema namtaka fulani, wao wakamleta mwingine. Kila baada ya muda waliletwa wachezaji kutoka Zambia, Ivory Coast na kadhalika. Na mwisho wakafeli licha ya kuwapa nafasi, nilisema awali siwataki lakini ikashindikana. Wakati mwingine unapigiwa simu na mtu humjui, unaambiwa kiongozi fulani kasema mchezaji fulani ajaribiwe. Siku tatu kiongozi anakuja anasema ni mzuri tumchukue.SALEHJEMBE: Unafikiri kuna viongozi waliokuwa wakifaidika na usajili?

Zeben: Ndiyo, watakuwa wanafaidika, sijui kifedha au kiundugu au urafiki.

SALEHJEMBE: Wiki za mwisho ulizosema ulianza kutulia zilikuwaje?

Zeben: Usajili wa mwisho kwenye dirisha dogo, nilisimamia mwenyewe. Kila kitu kilikwenda nilivyotaka. Nilitarajia sasa kuanza kuona mambo yanabadilika. Baada ya sare mbili, zote mechi za ugenini, nimefukuzwa, niwe mkweli nimeumia sana.

SALEHJEMBE: Unawazungumziaje wachezaji wa Azam FC?

Zeben: Wengi walikuwa watu wanaojituma, walitaka kufanikiwa. Mambo hayakuwa yamekubali lakini naamini baadaye yangekaa vizuri hasa katika mzunguko wa pili.

SALEHJEMBE: Huenda hawakuelewa mfumo wa Kihispania?

Zeben: Kivipi? Angalia walicheza soka safi, tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukufunga. Hapa huwezi kusema mfumo, badala yake tulikuwa na mambo ya kurekebisha na kufanya.

SALEHJEMBE: Labda mambo yapi?

Zeben: Kuhakikisha tunaanza kufunga au kuzitumia vizuri nafasi.

SALEHJEMBE: Kutokuwepo kwa Kipre Tchetche kulikuwathiri?

Zeben: Sana, ndiye alikuwa roho ya Azam katika ufungaji na safu yote ya ushambulizi. Nimepishana naye, pia Farid Mussa ndiyo alikuwa amesajili Tenerife.

SALEHJEMBE:Nilielezwa wakati unaingia, posho za ushindi zilikuwa zimeondolewa. Hili unalizungumziaje?

Zeben: Kweli, niliingia, nikakuta malalamiko makubwa ya wachezaji kwamba posho za ushindi zimeondolewa. Utaona hili lilikuwa tatizo jingine, wachezaji hawakuwa na furaha. Unawakosa wachezaji mahiri, unakuta wachezaji wanalia na kulalamika. Nilijitahidi kuwashawasihi waelewe.SALEHJEMBE: Viongozi unawazungumziaje?

Zeben: Wengi ni watu wazuri na tulishirikiana. Mfano marehemu Said, alikuwa bora na mchapakazi kama ilivyo kwa aliyekuwa makamu na sasa ni mwenyekiti, Nassor Idriss.

SALEHJEMBE: Hujamtaja Saad Kawemba, huyu ni mtendaji mkuu.

Zeben: Kiungwana nisingependa kumzungumzia. Kwangu naona kaniangusha kwa kiasi kikubwa, mambo mengi ambayo niliyaona si sahihi, yeye aliona sawa. Mfano wakati wa usajili, kuhusu wachezaji walioletwa na kadhalika.

SALEHJEMBE: Kwa hiyo ulipenda kila kitu ufanye wewe bila ya kushauriwa?

Zeben: Hapana, mimi ni kocha, najua mchezaji bora kuliko yeye, najua listi sahihi kuliko yeye. Hawezi mtu akawa haonekani mazoezini, anaonekana siku ya mechi halafu anakuwa anajua kipi ni kikosi sahihi na siyo kocha. Usajili, yeye atajua vipi kuliko mimi wakati hajafundisha hata timu ya daraja la tatu?SALEHJEMBE: Labda una maneno yapi ya kumuachia ili ajirekebishe kama binadamu.

Zeben: Aheshimu kazi za wenzake.

SALEHJEMBE: Unawaambia nini watu wa Azam FC uliofanya nao kazi kwa zaidi ya miezi sita?

Zeben: Kwangu mashabiki, wachezaji na viongozi wengine, ni watu bora kabisa. Nitawakumbuka na moyo unaniuma kuwaacha.

SALEHJEMBE: Wamiliki wa Azam FC wanajitahidi sana kuwekeza, timu haisongi. Wewe pia umeshiriki lakini haukuwa na matokeo mazuri, una neno la kuwaachia.

Zeben: Wanajitahidi sana kwa kiwango cha Afrika hasa katika uwekezaji lakini lazima wakubali, kuwekeza vifaa bila ya watu sahihi, mwisho watachoka kwa kuwa hawatapiga hatua. Hivyo watafute watu sahihi kusaidia wanachotaka kukiona kinatokea.

SALEHJEMBE: Nikutakie safari njema kurejea Tenerife.

Zeben: Nashukuru sana.

SOURCE: CHAMPIONI
Nilijua Hili ni Simba Na Yanga tu kumbe hata Azam.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,650
2,000
Mahojiano yanaonyesha dhahiri Saad Kawemba anapiga sana hela za usajili. Haishangazi wanasajili majeruhi ambao wanaishia kuitia hasara team.

Mzee Bakhresa amtimue na bora mmoja wa watoto wake wafanye kazi hiyo.

Mzee kadhamiria kuleta mapinduzi ya mpira Tanzania lakini kuna mafisi wanaharibu.
Azam ikifanikiwa, Yanga na Simba zitalazimika kubadilika! Huo utakuwa mchango tosha wa Azam kwa soka letu.

Wanadiriki hata kumpangia kocha timu ya kucheza! Sasa wanapiga dili za kuleta kocha mwingine wapige tena hela. Kabla ya kuleta kocha, atimue akina Kawemba kwanza. Aje mtu mwingine atafute kocha mpya.
 
dvjnews5

JF-Expert Member
Dec 22, 2016
369
225
Na Saleh Ally
JUMATANO hii, uongozi wa Azam FC ulitangaza kumfuta kazi kocha wake mkuu Zeben Hernandez. Kama haitoshi ikawafuta kazi Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa Tiba za Viungo, Sergio Perez, wote hawa ni raia wa Hispania.
Uamuzi wa Azam FC kuwafuta kazi Wahispania hao ni kwamba, wameshindwa kuipa timu hiyo matokeo mazuri baada ya mechi 17 za Ligi Kuu Bara ikawa imeshinda saba, sare sita na kupoteza nne.
Uamuzi wa Azam FC kuwafuta kazi umetolewa baada ya makocha hao kwenda sare mbili mfululizo katika mzunguko wa pili, wakianza sare ya bao 0-0 dhidi ya African Lyon, halafu 1-1 dhidi ya Majimaji mjini Songea, zote zikiwa ni za ugenini.Kabla hajakusanya virago vyake na kurejea kwao Tenerife nchini Hispania, SALEHJEMBE ilifanya juhudi za kuwapata makocha hao na kuzungumza nao kwa lengo la kujua walichojifunza katika soka nchini na kipi hasa kilichowafanya kushindwa.
SALEHJEMBE: Pole, naamini ni safari za kimaisha.
Zeben: Kabisa, katika soka hili si geni, ingawa tumeumia sana.
SALEHJEMBE: Kipi hasa kimekuumiza?
Zeben: Mimi na wenzangu, tulianza kuamini kwamba sasa timu inakwenda kwa namna tunavyotaka, lakini ndiyo wameniondoa!
SALEHJEMBE: Kwani kabla haikuwa mnavyotaka?
Zeben: Kabisa! Kuna mambo mengi sana yalikuwa magumu kwangu. Kuanzia wiki mbili zilizopita, hali ilikuwa imetulia na tulianza kufanya kazi kwa amani.
SALEHJEMBE: Unaweza kueleza mambo ambayo hayakuwa yametulia?
Zeben: Nilifanya kazi kwa wakati mgumu sana, hasa kipindi cha usajili. Mimi nilitaka mchezaji huyu, kiongozi akaleta yule na baadaye kukawa na shinikizo la kuwasainisha.
SALEHJEMBE: Ulisainisha wangapi kwa shinikizo na kiongozi huyo ni yupi, mmoja wa watoto wa Bakhresa?
Zeben: Watoto wa Bakhresa hawakuwa wakiingilia mambo yetu. Wako viongozi wamekabidhiwa majukumu ya kuisukuma Azam mbele, lakini ni tatizo. Wakati mwingine kila siku ya mechi, kiongozi anataka umpe kikosi saa 4 asubuhi. Ukimpa tu, anaanza kupangua, huyu abaki, huyu apangwe!
SALEHJEMBE: Uliripoti hilo kwa waajiri wako?
Zeben: Viongozi ndiyo waajiri wangu, na wao ndiyo walikuwa wakifanya mambo ya kujiangusha. Acha kuingilia kikosi, kwenye usajili ndiyo ilikuwa shida kubwa kabisa.
SALEHJEMBE: Ukubwa wa hiyo shida ulitokana na nini?
Zeben: Nilisema namtaka fulani, wao wakamleta mwingine. Kila baada ya muda waliletwa wachezaji kutoka Zambia, Ivory Coast na kadhalika. Na mwisho wakafeli licha ya kuwapa nafasi, nilisema awali siwataki lakini ikashindikana. Wakati mwingine unapigiwa simu na mtu humjui, unaambiwa kiongozi fulani kasema mchezaji fulani ajaribiwe. Siku tatu kiongozi anakuja anasema ni mzuri tumchukue.
SALEHJEMBE: Unafikiri kuna viongozi waliokuwa wakifaidika na usajili?
Zeben: Ndiyo, watakuwa wanafaidika, sijui kifedha au kiundugu au urafiki.
SALEHJEMBE: Wiki za mwisho ulizosema ulianza kutulia zilikuwaje?
Zeben: Usajili wa mwisho kwenye dirisha dogo, nilisimamia mwenyewe. Kila kitu kilikwenda nilivyotaka. Nilitarajia sasa kuanza kuona mambo yanabadilika. Baada ya sare mbili, zote mechi za ugenini, nimefukuzwa, niwe mkweli nimeumia sana.
SALEHJEMBE: Unawazungumziaje wachezaji wa Azam FC?
Zeben: Wengi walikuwa watu wanaojituma, walitaka kufanikiwa. Mambo hayakuwa yamekubali lakini naamini baadaye yangekaa vizuri hasa katika mzunguko wa pili.
SALEHJEMBE: Huenda hawakuelewa mfumo wa Kihispania?
Zeben: Kivipi? Angalia walicheza soka safi, tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukufunga. Hapa huwezi kusema mfumo, badala yake tulikuwa na mambo ya kurekebisha na kufanya.
SALEHJEMBE: Labda mambo yapi?
Zeben: Kuhakikisha tunaanza kufunga au kuzitumia vizuri nafasi.
SALEHJEMBE: Kutokuwepo kwa Kipre Tchetche kulikuwathiri?
Zeben: Sana, ndiye alikuwa roho ya Azam katika ufungaji na safu yote ya ushambulizi. Nimepishana naye, pia Farid Mussa ndiyo alikuwa amesajili Tenerife.
SALEHJEMBE:Nilielezwa wakati unaingia, posho za ushindi zilikuwa zimeondolewa. Hili unalizungumziaje?
Zeben: Kweli, niliingia, nikakuta malalamiko makubwa ya wachezaji kwamba posho za ushindi zimeondolewa. Utaona hili lilikuwa tatizo jingine, wachezaji hawakuwa na furaha. Unawakosa wachezaji mahiri, unakuta wachezaji wanalia na kulalamika. Nilijitahidi kuwashawasihi waelewe.
SALEHJEMBE: Viongozi unawazungumziaje?
Zeben: Wengi ni watu wazuri na tulishirikiana. Mfano marehemu Said, alikuwa bora na mchapakazi kama ilivyo kwa aliyekuwa makamu na sasa ni mwenyekiti, Nassor Idriss.
SALEHJEMBE: Hujamtaja Saad Kawemba, huyu ni mtendaji mkuu.
Zeben: Kiungwana nisingependa kumzungumzia. Kwangu naona kaniangusha kwa kiasi kikubwa, mambo mengi ambayo niliyaona si sahihi, yeye aliona sawa. Mfano wakati wa usajili, kuhusu wachezaji walioletwa na kadhalika.
SALEHJEMBE: Kwa hiyo ulipenda kila kitu ufanye wewe bila ya kushauriwa?
Zeben: Hapana, mimi ni kocha, najua mchezaji bora kuliko yeye, najua listi sahihi kuliko yeye. Hawezi mtu akawa haonekani mazoezini, anaonekana siku ya mechi halafu anakuwa anajua kipi ni kikosi sahihi na siyo kocha. Usajili, yeye atajua vipi kuliko mimi wakati hajafundisha hata timu ya daraja la tatu?
SALEHJEMBE: Labda una maneno yapi ya kumuachia ili ajirekebishe kama binadamu.
Zeben: Aheshimu kazi za wenzake.
SALEHJEMBE: Unawaambia nini watu wa Azam FC uliofanya nao kazi kwa zaidi ya miezi sita?
Zeben: Kwangu mashabiki, wachezaji na viongozi wengine, ni watu bora kabisa. Nitawakumbuka na moyo unaniuma kuwaacha.
SALEHJEMBE: Wamiliki wa Azam FC wanajitahidi sana kuwekeza, timu haisongi. Wewe pia umeshiriki lakini haukuwa na matokeo mazuri, una neno la kuwaachia.
Zeben: Wanajitahidi sana kwa kiwango cha Afrika hasa katika uwekezaji lakini lazima wakubali, kuwekeza vifaa bila ya watu sahihi, mwisho watachoka kwa kuwa hawatapiga hatua. Hivyo watafute watu sahihi kusaidia wanachotaka kukiona kinatokea.
SALEHJEMBE: Nikutakie safari njema kurejea Tenerife.
Zeben: Nashukuru sana.

SOURCE: CHAMPIONI
Nilijua Hili ni Simba Na Yanga tu kumbe hata Azam.
Anajua kuwalisha watu maneno huyu salehe jembe
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
8,757
2,000
Azam fc inaelekea ilikoenda Kajumulo,,,,,,namuona mzee Bakhresa akirudi kuisaidia Mbumbu fc,aka wazee wa vikao vya send off,wazee wa chapati in Kaduguda's voice
 
Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,541
2,000
Mahojiano yanaonyesha dhahiri Saad Kawemba anapiga sana hela za usajili. Haishangazi wanasajili majeruhi ambao wanaishia kuitia hasara team.

Mzee Bakhresa amtimue na bora mmoja wa watoto wake wafanye kazi hiyo.

Mzee kadhamiria kuleta mapinduzi ya mpira Tanzania lakini kuna mafisi wanaharibu.
Azam ikifanikiwa, Yanga na Simba zitalazimika kubadilika! Huo utakuwa mchango tosha wa Azam kwa soka letu.

Wanadiriki hata kumpangia kocha timu ya kucheza! Sasa wanapiga dili za kuleta kocha mwingine wapige tena hela. Kabla ya kuleta kocha, atimue akina Kawemba kwanza. Aje mtu mwingine atafute kocha mpya.

Hapa umezungumza kiuanamichezo bila ushabiki. Azam ina nafasi ya kuzitoa kwenye comfort zone Simba na Yanga. Likifanyika hili kampira ketu katakua tu

Na hiki kimekuwa kilio changu hata kwa Mtibwa. Nimemwambia Jamal Bayser ajenge timu sasa sio kila siku anauza wachezaji wote na kuanza upya
 
BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
7,500
2,000
Hawa viongozi nao kaazi kweli-kweli...wanamuangusha Mzee Bakhressa

Kama ni kweli anayoyafanya huyu saad' ni heri BSS ampe mtoto wake uongozi pale..
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Uyanga wa Saab Kawemba ndio unaiangusha Azam. Hata alipokuwa TFF mambo ni yale yale.Hafanyi kazi kwa maslahi ya Azam bali kushibisha tumbo kwani mapenzi yake kimpira yapo Yanga.
 
Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,408
2,000
Nafikiri Azam itafute kiongozi wa Nje asiye na mahaba na timu zetu hizi za kisiasa.Pia Azam wamchukue kocha wa Lyon inawafaa.Ama watafute kocha mwingine mzoefu na mpira wakiafrika wenye fitna na figisu nyingi kama huu wa bongo.Kamwe yule Babu wa vyura asijegusa Azam kufundisha ndio itaoza kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom