kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 717
MANJI NA WANACHAMA NA WAPENZI WA YANGA WASHTUKIA MPANGO WA CHAMA CHA CHADEMA WA KUTAKA KUWARUBUNI ILI WAKIUNGE MKONO CHADEMA.
Katika kile kilichoelezwa leo na wapenzi na wanachama wa mabingwa watetezi wa kandanda nchini na washiriki pekee waliobaki katika michuano ya kimataifa katika ukanda wa Afrika mashariki klabu ya yanga ya Dar es Salaam kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema wapo katika mpango wa siri wa kupata wafuasi toka yanga kwa kisingizio cha madai ya kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji ameonewa na serikali kufuatia sakata la madawa ya kulevya.
Mpango wenyewe ni kumshawishi Manji ahamie Chadema na kisha afuatwe na mashabiki wanachama na wapenzi wa timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Twiga na Jangwani. HATA HIVYO MANJI AMEKANUSHA KUWA NA MPANGO WA KUKIHAMA CCM.' Mimi ni diwani wa kata kwa tiketi ya ccm haya masuala yangu yasiyumbishe wanachama wapenzi mashabiki na hata wachezaji wa yanga kwani naamini matatizo haya ni ya muda na yataisha na afya yangu ikiimarika nitarudi kujenga upya yanga yetu alisema Manji kwa sauti ya upole na unyenyekevu. Wanayanga tupuuze maneno haya ya uzushi na tusikubali wanasiasa kututumia kama daraja kutimiza malengo yao ya kisiasa kama promo wanayofanya kwa Wema Sepetu.
Baadhi ya wanachama maarufu wa yanga wametoa rai kwa wenzao wasiyumbishwe na watu wanaotaka kuichonganisha yanga na serikali au chama tawala. Wanachama hao ni pamoja na muhidini Abuu wa tawi la uhuru kariakoo . Liana Godfrey wa tawi la facebook Tabata Mashaka muhuni wa Yombo, Pauline Anthony wa kurasini Aloyce Raymond wa Turiani Morogoro na wengineo wengi ambao wameionya Chadema kuacha mbinu za kiujanjaujanja kutafuta wanachama baada ya hivi karibuni kupoteza mvuto kwa kasi hasa baada ya Mheshimiwa rais Dk John Pombe Magufuli kuwapoteza vibaya Mafisadi na Ukawa kukosa agenda.
Mnyetishaji mmoja ambaye ni kada wa Chadema alisema wapo wafuasi wa simba ambao ni Chadema wanaandaliwa kuhamia yanga ili kukiimarisha Chadema kupitia yanga. Mpango huo unashabikiwa na wapinzani wa yanga kimpira ili kuwe na mgogoro na hatimaye yanga ipotee kimpira siku za usoni.
HONGERENI WANA YANGA KWA KUNG'AMUA MBINU CHAFU ZA KISIASA SHIKAMANENI KWA MANUFAA YA YANGA NA AMANI YA NCHI YETU.