Manji akana kujiunga CHADEMA

Manji akana kujiunga CHADEMA

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,571
Kada wa chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Sengerema , Alex Manji amekanusha uvumi unaonezwa dhidi yake kuwa amerejea kwenye chama chake zamani , Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

"Nilijiondoa CHADEMA baada ya kuona na kuridhika na mipangilio ya utekelezaji wa ahadi za serikali ya CCM kwa kuleta maendeleo,ikiwemo miundombinu ya barabara. Kwa kweli kazi nzuri zimefanyika na nyingi ya ahadi zimetimizwa".Alisema Manji.

Aliendelea kusema "Hao wanaoeneza uongo kwamba nimerejea CHADEMA wana nia ovu dhidi yangu hivyo wananchi na wana CCM wawapuuze na siasa zao chafu na majitaka.

Mimi bado ni mwana-CCM safi".Alisema anafahamu chanzo cha kuenezwa kwa uvumi huo ni baada ya kuonesha nia ya kuwania ubunge , lakini akadai ni baada ya kuangalia na kubaini jimbo lipi ambalo maendeleo yake ni duni sababu ya mbunge kushindwa kutimiza ahadi , huko ndiko atajitosa ili awatumikie wananchi.

Source: Majira
 
chadema kawaida yao kudandia watu kunasiku utasikia wamesema kuwa mkapa kajiunga chadema subiri mtaona uongo utadhani wamechanjiwa.
 
kugombea ni haki yake kikubwa yeye agombee watu watapima make wale wapiga kelele wa chadema hakuna walichofanya.
 
chadema kawaida yao kudandia watu kunasiku utasikia wamesema kuwa mkapa kajiunga chadema subiri mtaona uongo utadhani wamechanjiwa.

teh teh teh, ndiyo kazi iliyobaki wafanye baada ya wananchi kuwashtukia.
 
Kwanini kwenye heading yako usianze na jina lake la kwanza Alex..?
 
Siku hizi unavumisha mwenyewe kisha unakanusha vikali ili Nape akija akupandishe jukwaani na watu wakufahamu. Ujinga juu ya ujinga ndani ya upuuzi.
 
Kumbe manji wa sengerema ,,hana impact huyo,,anajijua havumi sasa anataka kutumia chama makini cha watu makini chadema ili avume,,,,amechelewa sana.
 
Kada wa chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Sengerema , Alex Manji amekanusha uvumi unaonezwa dhidi yake kuwa amerejea kwenye chama chake zamani , Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

"Nilijiondoa CHADEMA baada ya kuona na kuridhika na mipangilio ya utekelezaji wa ahadi za serikali ya CCM kwa kuleta maendeleo,ikiwemo miundombinu ya barabara. Kwa kweli kazi nzuri zimefanyika na nyingi ya ahadi zimetimizwa".Alisema Manji.

Aliendelea kusema "Hao wanaoeneza uongo kwamba nimerejea CHADEMA wana nia ovu dhidi yangu hivyo wananchi na wana CCM wawapuuze na siasa zao chafu na majitaka.

Mimi bado ni mwana-CCM safi".Alisema anafahamu chanzo cha kuenezwa kwa uvumi huo ni baada ya kuonesha nia ya kuwania ubunge , lakini akadai ni baada ya kuangalia na kubaini jimbo lipi ambalo maendeleo yake ni duni sababu ya mbunge kushindwa kutimiza ahadi , huko ndiko atajitosa ili awatumikie wananchi.

Source: Majira

Hongera mkuu kwa kupumulia makalio

Join Date : 29th April 2011
Posts : 9,119
Rep Power : 0
Likes Received393
Likes Given1
 
Manji hana msaada wowote kwa watuwenye akili timamu! kwnza hajulikani...
 
Mimi nakujua sengerema vizuri, huyo alex manji hana popurality kihivyo labda kama ndo anataka kujulikana kwa kupitia CDM..
 
Kuna ugumu sana baina ya wadanganyika juu ya uelewa wa majukumu ya mbunge kwa mujibu wa katiba!

Sina hakika kama kama kuwafanyia wananchi mambo kama ujenzi wa barabara, mifumo ya maji safi na taka, umeme, miundombinu ya elimu, afya, n.k. ni jukumu la mbunge...! Hili ni jukumu la serikali. Mbunge ana jukumu la kuisimamia na kuihoji serikali ili itimize wajibu wake kwa wananchi wake!

Sasa utasikia watu wanasema mbunge hajawafanyia chochote wananchi; Ikumbukwe serikali yoyote duniani huendeshwa kwa kodi za wananchi wake; sasa tunajenga hoja eti mbunge hajawafanyia hili ama lile wananchi kwani yeye anakusanya kodi ya aina yoyote kwa waliompigia kura jamani???!!!
 
Dahhhhhhh!
Nimekuja mbiiiiiiiiiio,kumbe manji mwenyewe ni 'aka'.
agrrrrrrrrrrrrr!
 
Back
Top Bottom