Manispaa ya Temeke katika kashfa ya uporaji wa ardhi

Mwalufunamba

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
211
129
Manispa ya Temeke imewapora ardhi wanachi wa Kata ya Somangila mitaa ya Kizani (Gezaulole), Mwela, na inaelekea maeneo ya Mwongozo.
Historia ya mradi
Mradi wa Viwanja 5,000 Eneo la Gezaulole mchakato wake na vurugu zake zilianza toka mwaka 2008. Ukiwa ni mradi ulioratibiwa na kutekelezwa na watumishi wachache wa manispaa ya Temeke wakishirikiana na Madiwani wa Manispaa hiyo ambao kwa wakati huo hadu sasa wengi wao wakiwa ni wa CCM.
Toka mwanzo wake hadi utekelezaji wake kuanza wananchi hawakushirikishwa. Wanachi wenye mashamba, eneo liliko chini ya mtaa wa Kizani ndiyo waliokuwa wakwanza kushtuka. Waliupinga mradi huo kwa kuunda kamati ya wanachi iliyoshughulikia mradi huu. Kitu cha ajabu, Diwani wa Kata ya Somangila, Mama Mpanjila,(ambaye kwasasa ndiye Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke) akishirikiana na watumishi hao wa Manispaa pamoja na Mkuu wa Wiliya ya Temeke kwa wakati huo;waliihujumu kamati ya wananchi kwa kutengeneza Kamati nyingine ya watu waliowataka wao na kuwafungana kuwabambikia kesi miongoni mwa wajumbe wa kamati ya awali iliyoundwa na wananchi.
Wanachi wa Gezaulole walifungua mashitaka katika Mahakama Kuu. Manispaa waliposikia hilo limetukia walikazana sana kuona kuwa wanafanikiwa. Mwaka jana mwanzoni Mahakama Kuu ilitoa "Stop Order" kwa Manispaa kutoendelea na Mradi huo hadi hapo kesi ya Msingi itakapokwisha. Manispaa walifunga macho na kmasikio kutia pamba, wakaendele na kutathmini ardhi ya wanachi, kutoa fidia kwa ardhi kwa malipo kiduchu, na kuuza upya viwanja vilivyopimwa. Zoezi la uuzaji wa viwanja lilifanyika mwaka 2011 Julai na 2012 Juni.
Dhuruma
Katika jambo lilisilokuwa la kawaida Manispaa wakisingizia wanataka kupima viwanja ili kuyapata makazi rasmi , wakiisha kuvipima waliviuza kwa bei kubwa sana wakitengeneza super-profit na si huduma tena.
Waliwalipa wanachi wenye mashamba fidia ya TSh.750/=kwa m [SUP]2[/SUP] bila kuyahesabia mazao yaliyokuwapo ndani mw a eneo husika. Manispaa ikaja kuuza eneo lililopimwa; kila m[SUP]2[/SUP] kwa TSh. 1000/= kwa wale waliokuwa na maeneo, na kwa wasiok uwa na maeneo m[SUP]2[/SUP] iliuzwa kwa TSh. 6000/=. Hii ilikuwa ni bei ya ununuzi wa maeneo ya makazi kwa mwezi Julai mwaka jana. Kama haitoshi, ndani ya mwaka huo huo wa fedha yaani 2011/12 wiki chache zilizopita wametoa tangazo la kuuza viwanja 1800. Bei ya m[SUP]2[/SUP] kwa wale ambao maeneo yao yalichukuliwa na Manispaa ni TSh 300/= na kwa wasiokuwa na maeneo TSh. 8000/=. Ikumbukwe kuwa fomu ya kuomba kiwanja ilinunuliwa kwa Tsh. 20, 000/= Julai mwaka jana na kwa sasa imeuzwa kwa TSh. 30,000/=.
Kutokana na bei za hapo juu, Manispaa iliwalipa wananchi wastani wa TSh. 3,000,000/= kwa ekari kama fidia na yenyewe kuwauzia wananchi wa wenye mashamba Gezaulole TSh. 8,000,000/= kwa ekari.
 
Usanii wa ugawaji viwanja
Mwaka jana wakiisha kutangaza siku rasmi ya kuuza fomu za kununua viwanja, usanii mkubwa ulifanyika. Ilipofika saa 4 asubuhi walitangaza Fomu zimekwisha. Vurugu zikatokea ikabidi Polisi kutoka Kituo cha Chang'ombe waitwe kuja kutuliza ghasia. Watu walipinga wakisema, haiwezekani kusema fomu zimeisha wakati watu walioingia ndani kuchukua fomu hawajafika hata 100. Matokeo yake yamekuwa ni aibu. Majina ya wajumbe karibu wote wa NEC ya CCM wamepewa viwanja, ikijulikana kuwa hata kwenye kupanga foleni hakuwepo. Nashindwa kuattach picha.

Katika zoezi la uchukuaji fomu sasa hivi, vituko vimezidi. Fomu zilliisha saa mbili. Watu waliokwenda Manispaa ya Temeke saa 11 alfajiri wamekosa fomu. Nini kimefanyika, huu ndiyo mchezo: kuna maafisa wa manispaa wamebook fomu kadhaa-wa-kadha, wapo waliotaka 50, 40,10 na 20. Wameandikisha majina ya jamaa wanaowataka na wengine na kuwachaji fedha kati ya 40,000/= hadi 100,000/= kwa fomu. Hela hiyo ikiisha kutolewa unapewa fomu na kuijaza.Kisha unamkabidhi muhusika yeye ndiyo ataipeleka manispaa.
Kuna mengi ya kuandika, Nitarudi baadaye.
Madudu haya Mkurugenzi wa Manispaa na Waziri wa Ardhi, Nyuma na Maendeleo ya Makazi wanajua.
 
Hapa ndipo unatamani Magufuri angeelea kubaki hii Wizara. Jamaa wana viburi sana halafu ni mabingwa wa kudhurumu maeneo ya watu.
 
Back
Top Bottom