Ni waziri yupi yule kilaza wa enzi ya Mkapa-Mungai Joseph nadhani, aliyefuta somo la kilimo skuli na huku akifahamu kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa hili na wawekezaji wengi wanakuja kuwekeza kwenye kilimo.
Je huyu naye si anawajibika? awajibishwe hata kama yu kaburini kwa kutunyima maelfu ya Wanafunzi ajira wakati ujao? Hili nalo litakuwa fundisho kwa maccm.
Si mnaona mlivyo madhaifu sasa kwa nini asingesomeka tangu mwanzo kuwa shule zinazoongozwa na manispaa zimefanya vibaya, mjifunze kuandika ili mueleweke kwa wananchi mnaowaomba kula lakini mkishika nyinyi hatamu ya uongozi sijui kama mtayaweza, labda muombe viongozi kutoka ccm.Hapa tunazungumzia shule za serikali zilizopo chini ya manispaa ya kinondoni!magamba akili fupi sana!fedha ni shule ya manispaa!?
Uongo mtupu, ninaifahamu shule moja ambayo ina division one zaidi ya 10 !!!!!
CHADEMA wangejaribu ku-break down kwa kila jimbo ili wabunge wa CCM waone madhara ya ndiyo zao bungeni. Kawambwa bado yuko ofisini anacheka. Kama Chami, Mkulo na Omar Nundu waliondolewa kwa sababu za kiutendaji, kwa nini Kawambwa abaki wakati generation inageuzwa mbumbumbu? 94% wamefeli, bado wana matumaini na Waziri kuwa ana jipya?
Kufeli kwa watoto wetu kwanza tuweke pembeni itikadi zetu. serikali inabeba sehemu tu ya lawama hizo wengine ni:-
1.Waalimu
2. wanafunzi
3. wazazi
4. jamii
Angalia shule binafsi na zile za seminary zinazong'ara kila mwaka zimefanya vibaya.
kuna tatizo kubwa kwenye sekta ya elimu zaidi ya kuilaumu serikali peke yake tunaweza tusipate jawabu la kudumu.
Vitu vyote ulivyotaja vimekuwepo siku zote, na hata serikali imekuwapo siku zote. Iweje sasa ndio matokeo yawe tofauti? Na kwanini serikali ilihaidi ufaulu kwa 70%? Ilitumia vigezo gani kutoa hizo ahadi?
Pili, mwanafunzi anaingia kidato cha kwanza hajui kusoma na kuandika, alifaulu vipi? Halafu useme, shule hazina walimu, au shule moja ina waalim 3 (shule nzima) watoto watafulu kwa nguvu za Prof Maji Marefu?
Matatizo kwenye elimu yamesemwa sana sana sana. HAKIELIMU wameandika report mara nyingi sana, lakini wakubwa bado hawaonekani kustuka. Sasa hivi ni tume inaundwa, lakini Wizara ya Elimu yenyewe bado wanakunywa chai na kula vitafunwa. Hawasemi wanapanga nini au wana nini jipya? Haya report ya tume ikija wataweza kusimamia kweli?
Waliwalazimisha walimu kurudi shuleni lakini walishindwa kuwalazimisha wafundishe! Lazima serikali iwajari walimu, hivi mna habari walimu wameyafurahia sana matokeo ya mwaka huu? Umeziona meseji wanazosambaziana? Una habari F za hesabu zipo kama laki 3 hivi? Maswali mengi majibu kiduchu
Ni za serikali hizo eti!Kwani huyo mto mada katoa takwimu zipi? zaidi ya kusema tu na watu wanamsapoti.
Sasa kama unafahamu mtu akikwambia wilaya ya kinondoni bila ya kunyambulisha anachokimaanisha! na mimi nataka kumwambia kama kiwilaya shule ya Feza ipo kwenye wilaya ya kinondoni na imetoa Div I 48, lugalo ina div I 3 au ana Kinondoni anayoimaanisha?
Hapa tunazungumzia shule za serikali zilizopo chini ya manispaa ya kinondoni!magamba akili fupi sana!fedha ni shule ya manispaa!?
Inawezekana wewe ni yule wa upande usioona,mnaotaka kuaminisha watu kuwa usiku ni mchana na masika ni kiangazi!Mtoa mada kaongelea shule za manispaa wewe unatakakupotosha maana kwa kututajia shule za wawekezaji!Na hujapenzwa na watu kumsapoti,sikushangai wewe na wenzako wa upande wako.Kwani huyo mto mada katoa takwimu zipi? zaidi ya kusema tu na watu wanamsapoti.
Sasa kama unafahamu mtu akikwambia wilaya ya kinondoni bila ya kunyambulisha anachokimaanisha! na mimi nataka kumwambia kama kiwilaya shule ya Feza ipo kwenye wilaya ya kinondoni na imetoa Div I 48, lugalo ina div I 3 au ana Kinondoni anayoimaanisha?
Si mnaona mlivyo madhaifu sasa kwa nini asingesomeka tangu mwanzo kuwa shule zinazoongozwa na manispaa zimefanya vibaya, mjifunze kuandika ili mueleweke kwa wananchi mnaowaomba kula lakini mkishika nyinyi hatamu ya uongozi sijui kama mtayaweza, labda muombe viongozi kutoka ccm.
Ahahaha yaani viongozi wa kitaifa waizungumzie shule ya watu binafsi?Tunapo laumu kuwa serikali imeshindwa kuimarisha elimu TUNAZUNGUMZIA SHULE ZILIZO CHINI YA SERIKALI na Diwani alikuwa sahihi!
Hata hivyo Kinondoni wamejitahidi sana kupata DIV 1 hizo 5,sisi Kyela HATUNA DIV 1 hata moja na DIV 2 tunazo 2 tu!Nipo tayari kushiriki maandamano ya kumtoa Dr Kwambwa kwa mustakabali wa nchi yetu!
Hivi kwa nini inaonekana kama vile ni jambo la kuidhihaki serikali eti kwa sababu walimu wamefelisha wanafunzi kwa sababu madai yao hayakusikilizwa,hii kazi ya ualimu haina ethics?
waliwalazimisha punda kwenda mtoni lakini wameshindwa kuwalazimisha kunywa maji. serikali ilitakiwa ilitambue hilo.Waliwalazimisha walimu kurudi shuleni lakini walishindwa kuwalazimisha wafundishe! Lazima serikali iwajari walimu, hivi mna habari walimu wameyafurahia sana matokeo ya mwaka huu? Umeziona meseji wanazosambaziana? Una habari F za hesabu zipo kama laki 3 hivi? Maswali mengi majibu kiduchu
Kuna kitu ambacho kimefichika kwenye matokeo hayo.Kila mtu anailaumu serikali na kila mtu ni mtaalamu wa kutambua kwa nini kizazi cha twitter/facebook kinafyatua ziro nyingi sana.
Inawezekana tatizo lipo hapo kwenye red. Kuna watoto nawajua wanatumia muda wao wote kwenye mitandao jamii, na walikuwa form four. wote wamepata ziro.