Manispaa ya Bukoba ina uhitaji wa daladala

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
7,072
2,000
Mji wa Bukoba ulio na watu zaidi ya laki mbili na eneo kubwa lenye makazi ya watu lakini cha kushangaza mji huu hauna route yoyote ya daladala zinazofanya usafiri ndani ya mji mbali na bodaboda, bajaji na taxi ambazo zina tozo kubwa.

Zamani mji huu ilikuwa na route za daladala hasa kutoka Vandarini mpaka Rwamishenye, stand Rwami nk, lakini vilikufa lakini sasa watu wanateseka kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine ukizingatia mji huu una milima mingi.

Mfano toka Kahororo km 5 toka Kyakairabwa km 6, toka kyebitembe km7, toka custom km 4, kutoka Kibeta na Saut km 10, kutoka Nyakato km 10 nk.

Hivyo watu wanateseka hasa kutembea hadi mji kutoka maeneo haya.

Tunawakaribisha wote wanaotaka kufanya biashara ya daladala anakaribiswa sana tunazihitaji mno tumechoka na bodaboda.
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,365
2,000
Halafu huu ndiyo uji ulikuwa unapambanishwa na Moshi kwa picha za RSA....kumbe hata usafiri wa dala dala hamna....kaazi kweli kweli
 

robert sendabishaka

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
2,521
2,000
daladala zinasafirisha abiria masafa marefu kama bukoba-muleba, bukoba-karagwe, bukoba-mtukula. kwakweli usafiri wa mizunguko ya viunga vya ndani k. v kashai, kahororo, nyamkazi, custom via mto Ngono, kibeta via Walkguard na rugambwa, hamugembe, rwamishenye, kagondo, kemondo, kyetema na katerero, katoma ni taabu na unajikuta umelipa gharama za kukufikisha nje ya wilaya. wawekezaji kwenye sekta ya usafiri walitazame hilo
 

GeeM

JF-Expert Member
Apr 11, 2014
1,899
2,000
Dont tell me! Umaarufu wote wa mkoa huu na watu wake kumbe bado wako very far behind?? Just kidding
 

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,398
2,000
Naomba hii mada iendelee kujadiliwa, inakuwaje mji unakosa daladala?
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,389
2,000
Jana kuna eneo niliona mahala n.meya akiitaji usaidizi wa ushauri juu ya masuala kadhaa kwa b.la madiwani, nafikiri ni vizuri pia tukamhoji hata yeye ili atoe majibu ni kwanini katika eneo lake la kiutawala wananchi hawapewi huduma hii muhimu na ya lazima kwao
 

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
7,157
2,000
Jana kuna eneo niliona mahala n.meya akiitaji usaidizi wa ushauri juu ya masuala kadhaa kwa b.la madiwani, nafikiri ni vizuri pia tukamhoji hata yeye ili atoe majibu ni kwanini katika eneo lake la kiutawala wananchi hawapewi huduma hii muhimu na ya lazima kwao
wahaya mbwembwe nyingi kumbe Hamna lolote kimji kimechakaa
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,272
2,000
stend ya bk inatia kichefuchefu kweli,hafu kingine watu wa bukoba wako static sana,ukabila umewaharibu sana hawa watu wanatakiwa kuombewa sana dunia ilishamove zamani sana hapo walipo katika mindset zao.HAIWEZEKANI WAPIGA DEBE STEND MNAONGEA KILUGHA TU,kwenye mabenki,maofisini yan inakera sana sjui kwanini tu iko hv bukoba mpaka karne hii ya 21
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,886
2,000
Mji Wa bukoba ulio na watu zaidi ya laki mbili na eneo kubwa lenye makazi ya watu lakini cha kushangaza mji huu hauna route yoyote ya daladala zinazofanya usafiri ndani ya mji mbali na bodaboda,bajaj na taxi ambazo zina tozo kubwa.zamani mji huu ilikuwa na route za daladala hasa kutoka bandarini mpaka rwamishenye.stand rwami nk lakini vilikufa lakini sasa watu wanateseka kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine ukizingatia mji huu una milima mingi.mfano toka kahororo km 5.toka kyakairabwa km 6 .toka kyebitembe km7.toka custom km 4.na kutoka kibeta na saut km 10.kutoka nyakato km 10 nk.hivyo watu wanateseka hasa kutembea hadi mji kutoka maeneo haya.tunawakaribisha wote wanaotaka kufanya biashara ya daladala anakaribiswa sana tunazihitaji mno tumechoka na bodaboda!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom