Manispaa moshi kwafukuta madiwani na mkurugenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manispaa moshi kwafukuta madiwani na mkurugenzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mnduoeye, Oct 13, 2012.

 1. m

  mnduoeye Senior Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF taarifa tulizozipata ni kuwa sasa hivi kuna vita kali ya chinichini kati ya madiwani wa Manispaa ya Moshina Mkurugenzi wao kuhusu ugawaji wa viwanja uliofanywa kinyemela na Mkurugenzi maeneo ya Majengo block R.Inasemekana eneo hilo lilikuwa eneo wazi katika kata ya Majengo lakini kwa hila eneo hilo limebatizwa na Mkurugenzi na ofisa ardhi kuwa ni eneo baki (reserve)na limegawanywa viwanja vitano na pia inasemekana aliyepewa ni mtu na mkewe tena matajiri wa kutupwa ndio wamepewa hivyo viwanja.Inasemekana pia katika kikao cha juzi cha Mipango miji hoja hiyo iliibuka na kuletaa mtafaruku mkubwa kati ya madiwani na Mkurugenzi wao na hata kutishia kikao kuvunjika lakini kwa kuwa hoja hiyo ilikuwa katika mengineyo kiliisha salama lakini bado ikaamriwa kamati ndog ipate majibu ya hoja hiyo siku ya jana .Ikumbukwe pia Baraza hilohilo liliunda kamati ya uchunguzi kuhusu viwanja vinavyotolewa kiholela wakati kuna kesi nyingi za madai ya ardhi inayoikabili Manispaa hiyo katika mahakama za ardhi. na madai mengine ya kutoa vibali holela vya ujenzi na ukarabati ambayo pia Mkurugenzi huyo alilalamikiwa pia na Mbunge PhilemonNdesamburo katika vikao vya bunge.Mlio karibu na Mwenyekiti wa mipango miji hebu mtujuze nini kinaendelea baada ya kikao cha jana.
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kiongozi wa kuteuliwa hakutakiwa kuwa na mamlaka yeyote dhidi ya viongozi waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi.kwani hii inaua mamlaka za wananchi kujiamulia mambo yao wenyewe kupitia kwa viongozi wao waliowachagua badala yakupitia kwa mtu aliyeletwa na mamlaka za juu. hili swala lazima kwy katiba mpya litazamwe upya kwani tanzania ni nchihuru hakuna haja tena ya wananchi kuongozwa na watawala wa kuteuliwa kwani wananchi wana busara ya kutosha ya kuchagua viongozi wao wenyewe.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kwa nini usijiulize Dr Slaa kwa nini anawafukuza madiwani wa Arusha na Mwanza wakati wamechaguliwa na wananchi.
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  slaa hana mamlaka ya kumfukuza diwani isipokuwa kamati kuu inayo mamlaka ya kukufuta uanachama tu kwa kukiuka
  katiba yao. usichanganye uanachama na udiwani kwani hakuna mtu anayepigiwa kura kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
   
 5. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  KWIWKIWKIWKWIWKWI:focus::focus::focus::focus::focus::focus::focus::focus: WACHA :blah::blah::blah::blah::blah::blah::blah:
   
 6. Nyiluka

  Nyiluka Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Pinda si alishatangaza mkurugenzi mpya,hv anatakiwa aanze kazi lini?
   
 7. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ukweli ni kwamba mkurugenzi ni mpita njia, tofauti na madiwani ambao kwa kiasi kikubwa ni wakazi wa maeneo husika na wana maslahi ya muda mrefu katika eneo husika. Matokeo ya maamuzi mabovu ya leo yatawakuta wakiwa hapo wakati mkurugenzi anaweza kuwa ameshahamishwiwa mahali pengine. Mfumo huu ni tatizo kubwa kwa maendeleo endelevu.
   
 8. m

  mnduoeye Senior Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyetangazwa ni wa hamashauri ya wilaya ya Moshi yenye majimbo ya Vunjo na Moshi vijijini sio Moshi mjini(manispaa)
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Ritz, una matatizo gani na Dr. Slaa? Teh teh teh! Angalia usije mpa mjukuu wako jina lake.
   
 10. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ritz Dr. Slaa ana mamlaka ya kufukuza bali kamati kuu ndo ina mamlaka ya kumfuta mtu uanachama wala si udiwani.
   
Loading...