Mangula: Nguvu ya CHADEMA inatisha

Mangula: Nguvu ya CHADEMA inatisha

ahahah hizi ni ndoto za mchana kabisa, CDM ndo wanapumulia machine chama chao kinafutika kwenye ramani ya dunia 2015. Katibu mkuu wa CDM kaanza u Vasco Dagama kwa ziara za marekani, anatafuta uhalali wa kutafuna pesa ambazo CDM wanapata kutoka kwa walalahoi na wahisani!
Baada ya Uchaguzi wa 2010 Viongozi wa CDM walimdanganya Slaa kwamba kashinda! yaani ni kichekesho uwezi kukosa hata theluthi ya wabunge wa kuchaguliwa majimboni alafu ukaota umeshinda Uraisi!!.
My advice kwa Slaa 2015 agombee jimboni kwake tu ubunge, wananchi wa jimbo lake pengine bado wanamkubali, akigombea uraisi ndo utakuwa mwisho wake kisiasa kwani atashindwa vibaya sana.

If wishes were horses you will be riding on them
 
T 2015 CDM. ccm kuwa chama kikuu cha upinzani. Hahahahaaa sipati picha SAVIMBI atakua wapi kipindi hicho.
 
after understand the SOSOMO party has rot they decide to give back to mangolo and kinano and the weaked one mwingolo and nopuye to shift slowly sosomo to NYUMBA YA MILELE, through my own view mr jk want the country turn into real democracy of party interchange in leading government but WAHAFIDHINA,such as wossire, lokuvo and few others hate that too much, dr jk know the important of this too and he want to through away the single party monopoly of leadership,the time has reach there will be no escapement.

Mkuu hiki KISWANGLISH chako kigumu sana bana unaonaje ukitutafsiria kwa kiswahili sisi ambao tulisoma ngumbalu ili tukuelewe?
 
Teh Teh Mangula anafanya kazi ya CHADEMA akiwa CCM.
 
CCM yenyewe ilizikwa siku alipozikwa Mwl.Nyerere na baada ya hapo zikabaki picha za CCM ndo zinajifanya kuongea na kutisha watu kama vinyago vya kwenye mashamba ya mahindi dhidi ya tumbiri ila nao wakishtuka siku moja wanaelewa kumbe ule ni usanii siyo mtu wala nini... leo tunavyoongea mifupa ya ccm nayo ilishaoza kaburini
 
Ndiyo ni kweli kuna baadhi ya mambo chadema inatisha,kama vile kufundisha wananchi kuandamana,kusema uongo,na kupora wake za watu.

Wanaoongoza kwa uongo ni MACCM. Kama ulishawahi porwa mke bac ulikuwa umeoa KAHABA. Upate mke kwenye madanguro utegemee atakaa nyumbani?
 
Wajamaa kama Mangula kawaida yao ni kusema ukweli na kwao fitina ni mwiko! Anayeweza kusimama jukwaani kwa sasa na kubeza nguvu ya CHADEMA si mkweli na wala haitakii mema CCM. Ni vema CCM iangalie ni wapi ilipopoteza mvuto kwa Watz walio wengi- plus their own members,na kujirekebisha - if it is not too late!
 
Makamu mwenyekiti wa CCM,Ndugu Philip Mangula,amesema nguvu ya CHADEMA inakitishia CCM.Ameelezea kushangazwa kwake na nguvu ya CHADEMA dhd ya CCM yenye wanachama wengi.
My take:
Ni dhahiri sasa kuwa hata viongozi wa CCM wanatambua kuwa CHADEMA kinaelekea kushika dola 2015.SOURCE MAJIRA YA LEO Tarehe 10/10/2013

- Source ni gazeti la Majira tu? Una maana Tanzania Daima na Mawio hawakumsikia akisema hayo? Maaana angesema kweli hayo maneno leo Tanzania Daima lingekuwa na sherehe kubwa sana,


Le Mutuz
 
Wednesday, October 9 2013, 22 : 51

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania (Bara), Philip Mangula ameshangazwa na chama hicho kuwa na ‘jeshi’ kubwa la wanachama, lakini linazidiwa nguvu na jeshi dogo la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatua ambayo imemfanya aamke na kusoma alama za nyakati kwa kuwarudia wananchi.

Akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waandishi wa habari jana kabla ya kuanza ziara yake jijini, Mangula alisema; “CCM ina jeshi kubwa la wanachama lakini linashindwa na jeshi dogo la CHADEMA ambalo halina hata anuani... hivyo nimeona ipo haja kurudi kwenu kuanzia ngazi ya chini kupitia matawi, shina na wananchi mnieleze tatizo ni nini?” Alisema ili kufikia wananchi nkoani Dar es Salaam, atafanya ziara katika wilaya zote za mkoa huo na kukutana na watendaji, wanachama na wananchi kwani kila mwana CCM ni askari wa mstari wa mbele, lakini anashangazwa na nguvu ndogo iliyopo sasa.

“Chama kikiwa na nguvu ndipo na Serikali inavyokuwa na nguvu, umefika wakati tuelewe kuwa ni muhimu chama kiwasemee watu na si viongozi wa chama wakisemee; hivyo uhai wa chama ni jambo muhimu kwa wana CCM,” alisema Alieleza kuwa makundi yaliyotokana na uchaguzi wa 2010 ndani ya chama hicho, bado yapo na yanaendelea kwa kasi, hali iliyoathiri zaidi Chama mpaka kufikia mwaka 2012, hivyo mkakati wa kujua vipi yaondolewe pasipo kuathiri zaidi 2014 mpaka 2015 unahitaji kuwepo na mipango imara.

Mangula alisema katika ziara yake hiyo ya mafunzo ambayo imetokana na kutambua kuwa nguvu ya chama ni uwepo wa wanachama, atatenga muda mwingi kuzungumzia changamoto zinazowakabili na kuwagawa wana CCM. Alisema kwa kufanya hivyo atapata sababu zinazokwamisha maendeleo ya chama hicho. Alihimiza wana CCM kuelewa kuwa katika wiki ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, ipo haja kuenzi harakati zake kwa kukiongezea nguvu chama. Mangula alisema kujenga chama kunahitaji kujitoa hata kufikia kuacha nafasi ya madaraka kama alivyofanya Mwalimu Nyerere. “Wakati wa wiki ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni muhimu kuwa na chama chenye nguvu na kujitoa kwani Mwalimu aliacha hata nafasi ya Uwaziri Mkuu na k umuachia Mzee Rashid Kawawa kwa lengo la kurudi katika kazi za ujenzi wa chama na pia tukumbuke Mwalimu aliacha kazi ya Urais mwaka 1985 na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Mwinyi, ambapo yeye alirudi tena kufanya kazi za chama hivyo kukijenga chama kunahitaji kujitoa ili kiweze kuwa na
 
ondoa takatkata yako,mangula uko mfuko mwa mafisadi huna lako ww ni muhuri tu, subiri uone kazi ya chadema
 
Wednesday, October 9 2013, 22 : 51

"Chama kikiwa na nguvu ndipo na Serikali inavyokuwa na nguvu, umefika wakati tuelewe kuwa ni muhimu chama kiwasemee watu na si viongozi wa chama wakisemee; hivyo uhai wa chama ni jambo muhimu kwa wana CCM," alisema

Kikwete umemsikia makamu wako?
 
Kama CCM wataka kurejesha imani kwa wananchi na wakirudishe Chama hiki madarakani bila bughudha kuanzia uchaguzi wa mwakani wa serikali za mitaa na ule wa 2015.. basi wafanye yafuatayo>>>

1. Wahakikishe mchakato wa katiba mpya unafanyika bila matatizo yoyote huku wakiwaunga mkono wazanzibari ambao wanataka tuwe na serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Tanzania...waachane na wale wanaotetea masilahi kwa masuala ya muungano wa mkataba ama serikali Tatu. CCM itetee tuwe na serikali moja tu.

2. Kuanzia sasa wale wote wanaohusika na madawa ya kulevya hapa nchi hata huko nje ya nchi watiwe nguvuni na sheria zetu ziboreshwe ili ziruhusu adhabu kali (kama ya huko china...kuuwawa)

3. Kuanzia sasa wale wote walioficha pesa za wizi kutoka kwa ama serikali ya watanzania ama taasisi zisizo za kiserikali( dini n.k) ambazo zingewasidia watanzania wakamatwe mara moja nakufunguliwa mashitaka...na ikibidi wafilisiwe.

4. Wale waliohusika katika wizi wa EPA, Mikataba ya ajabu ya gesi na madini...Richmond nk. wote wakipate cha mtema kuni kwa mujibu wa sheria zetu.

Najua yapo mengine muhimu,lakini CCM ianze na haya...kama kweli wanataka kuiongoza Tanzania baada ya 2015 badala ya kutawala kama wanavyofanya sasa huku wakiitetemekea CHADEMA.
 
hivi huyu mzee ameishamaliza fungate ? Si tuliambiwa ameoa juzijuzi !
 
Ni vema ametambua ukweli utamweka huru nankuchukua hatua sahihi KJIUZURU umakamu mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom