• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mangula katolewa kafara na CCM

  • Thread starter melimeli maganga pau
  • Start date
M

melimeli maganga pau

Senior Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
148
Points
0
M

melimeli maganga pau

Senior Member
Joined Jun 23, 2012
148 0
Nguvu ya pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi

Tumezoea kuona mtu akifa hafufuki tena na wakati mwingine tunaweza kusema kuwa ni mwisho wa kila kitu hapa duniani, umaarufu wa mtu hupotea kabisa, biashara zake nazo hupotea kabisa na hata wana ndugu huanza kumsahau taratibu mwisho jina lake hubaki katika historia tuu.

Lakini hili la kufufuka limewezekana kwa wanasiasa kwamba wakati mwingine mwanasiasa anaweza kupotea katika ulingo wa siasa mpaka kusahaulika kabisa lakini siku moja tena siasa ikamrudisha katika madaraka kwa mara nyingine akaendelea kutamalaki ndio maana nasema nguvu ya pesa inaweza kununua madaraka na madaraka yakanunua uongvozi.

Nasema hivyo kwa maana hii ni takribani wiki mbili sasa tangu kikao cha nane cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi ccm {NEC} kumalizika pale Kizota mjini Dodoma na kumrejesha tena madarakani aliye kuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi wa awamu ya tatu katika uongozi wa Rais mstaafu ndugu Benjamin Wiliam Mkapa ndugu Philip Mangula. Aliyeonesha umahili wake katika medani za kisiasa hapa nchini kwa wakati huo na falsafa ya uwazi na ukweli.

Philip mangula alimaliza uongozi wake wa chama cha ccm alionekana ni kiongozi ambaye angeweza kupewa tena nafasi katika awamu ya nne ya Rais kikwete lakini alitoswa na Jakaya na kuamua kurudi zake huko Njombe kijiji cha Malinyi kuendelea na shughuli zake za kilimo cha viazi na nyanya na kupotea kabisa katika siasa.

Kama ujuavyo utamu wa madaraka, mangula aliamua tena kujitosa katika siasa alipojitokeza tena hadharani kuomba nafasi ya mwenyekiti wa chama mkoa wa irnga kabla ya kugawa mkoa na Njombe hata hivyo alishindwa kufurukuta kutokana na upepo uliokuwepo kwa wakati huo maana alionesha kuto kukubalika sana na wajumbe waliokuwa wakimzomea mara kwa mara alipokuwa akigawa vipeperushi vya wasifu wake huku wajumbe wakikejeli kwa maneno ya wazi kwamba huu sio wakati wa vipeperushi bali ni wakati wa vipeperushwa wakiwa na maana kuwa mwenye nguvu ndio mwenye nafasi ya kupata uongozi.

Na ndivyo ilivyo kuwa baadaye Deo au maarufu kama jah people kuibuka na ushindi mkubwa na dhamana ya kuongoza mkoa ikashikwa na mtu mwenye elimu ya ngumbaru na mangula kurudi zake njombe hapo ndipo ishara za wazi za kufa kisiasa kwa mangula kukaonekana wazi lakini juzijuzi tu hapa mangula kalamba dume kule dodoma na nyota yake kuanza kutamalaki tena na kuukwaa umakamu wa mwenyekiti wa chama Tanzania bara hivi ni sawa na kufufuka kisiasa.

Tukumbuke kuwa pia kuwa mangula ni kizazi cha wale wanasiasa wazalendo walitanguliza maslahi ya chama na taifa mbele badala ya ubinafsi, walipigania uhuru na walikula amini ya dhati ya kutumikia taifa na sio kutafuta ufahari wa fedha na umwinyi ,wao kwao cheo kilikuwa ni dhamana.

Sasa mangula kapewa rungu ataweza kukimbizana na mbio za dot komu za vijana ndani ya chama? Mimi naona ni changamoto kwake kuanza kukabiliana na wafanyabiashara, mafisadi, na makundi ya uchochezi na kuzirejesha ofisi za chama kuwa ni za kiitikadi na uadilifu na kuziacha ofisi za chama zilizogeuzwa sehemu ya magendo, ubinafsi, ubinafisishaji, ugenishaji wa mali za umma kwa kuvunja makundi ya wanyonyaji, kupe, wabaguzi wanyanyasaji na wakandamizaji ambao ndio wamehodhi madaraka ya chama na serikali kwa kuwageuza raia kuwa wakimbizi wa mifumuko ya bei katika nchi yao.

Mangula amekubali kusulubiwa msalabani kamayesu ili kukinusuru chama kabla ya uchaguzi ujao wa 2015 akiamini ataweza kuirejesha ccm kama ile ya wamu ya kwanza ya pili naya tatu iliyokuwa ikisimamia maslahi ya wakulima na wafanyakazi kila la heri Philipo Mangula shika tena hatamu hiki ni kipindi cha chukua chako mapema kabla hujawahiwa na wajanja.

Mangula amefufuliwa kisiasa ataweza kuongoza chama ambacho nguvu ya pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi??? Utaweza kurejesha heshima na haiba ya CCM iliyopotea miongoni mwa umma?

Kila la heri Mangula kupambana na kasi mpya ari mpya na nguvu mpya kwa kuwaletea wanachama imani namalizia kwa kusemakuwa naamini kuwa pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi.
 
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
1,448
Points
1,225
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
1,448 1,225
Kwa sifa hizo anafaa kuwa msimamizi mpya wa mirathi wa CCM, kwani viongozi wasasa wa CCM ni wasimamizi wa mirathi ya marehemu CCM kwani CCM ilishakufa.
 
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Messages
10,215
Points
1,250
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2009
10,215 1,250
Ninachojua kuhusu Mangula so far ni kuwa ana hasira na ccm ya sasa. Ndio maana siku ile ya kuteuliwa hakutaka hata kuongea. Ana mawili hadi kufika 2015. Mosi ni kujenga tena shavu, pili ni kupambana na ghadhabu aliyo nayo
 
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,573
Points
1,250
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,573 1,250
Kwa kawaida taasisi iwayoyote inapaswa kutomtegemea mtu mmoja au kikundi cha watu, bali inapawa kutegemea kanuni zilizopo. CCM, kama imeweka kanuni, imani na miongozo lakini haifuati miongozo hiyo bali inategemea mtu mmoja tena mzee kukirejesha kwenye chati chama, sio sahihi, imepotoka. Mangula wala Kinana hawaji na miongozo mipya, watatumia miongozo ileile. Ikiwa Mwenyekiti na Rais wa nchi ameshindwa na wimbi la wanachama wenzake sioni ni namna gani na kwa nguvu ipi Mangula ataweza. Mangula alianza kujulikana uwezo wake katika siasa za chama tangu akiwa kijana akawa anakua na itikadi ya chama chake. Kuendelea kumshikilia Mangula kuna maana hakuna tena vijana waadilifu na wachapa kazi walioandaliwa "groomed" kushika nafasi yake kisiasa endapo yeye atazeeka au hata kufariki dunia. Maana yake ni nini? CCM ni baba mgumba, hana warithi. Wote wamepungukiwa na utukufu. Si jambo la kujivunia kwake Mangula na chama chake. Mwalimu asiyefaulisha hana maana yoyote hata kama yeye anaweza kufaulu mtihani wa wanafunzi wake. Mwalimu mzuri ni yule mwenye wafuasi wengi kwa akili na tabia pia.
Nguvu ya pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi

Tumezoea kuona mtu akifa hafufuki tena na wakati mwingine tunaweza kusema kuwa ni mwisho wa kila kitu hapa duniani, umaarufu wa mtu hupotea kabisa, biashara zake nazo hupotea kabisa na hata wana ndugu huanza kumsahau taratibu mwisho jina lake hubaki katika historia tuu.

Lakini hili la kufufuka limewezekana kwa wanasiasa kwamba wakati mwingine mwanasiasa anaweza kupotea katika ulingo wa siasa mpaka kusahaulika kabisa lakini siku moja tena siasa ikamrudisha katika madaraka kwa mara nyingine akaendelea kutamalaki ndio maana nasema nguvu ya pesa inaweza kununua madaraka na madaraka yakanunua uongvozi.

Nasema hivyo kwa maana hii ni takribani wiki mbili sasa tangu kikao cha nane cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi ccm {NEC} kumalizika pale Kizota mjini Dodoma na kumrejesha tena madarakani aliye kuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi wa awamu ya tatu katika uongozi wa Rais mstaafu ndugu Benjamin Wiliam Mkapa ndugu Philip Mangula. Aliyeonesha umahili wake katika medani za kisiasa hapa nchini kwa wakati huo na falsafa ya uwazi na ukweli.

Philip mangula alimaliza uongozi wake wa chama cha ccm alionekana ni kiongozi ambaye angeweza kupewa tena nafasi katika awamu ya nne ya Rais kikwete lakini alitoswa na Jakaya na kuamua kurudi zake huko Njombe kijiji cha Malinyi kuendelea na shughuli zake za kilimo cha viazi na nyanya na kupotea kabisa katika siasa.

Kama ujuavyo utamu wa madaraka, mangula aliamua tena kujitosa katika siasa alipojitokeza tena hadharani kuomba nafasi ya mwenyekiti wa chama mkoa wa irnga kabla ya kugawa mkoa na Njombe hata hivyo alishindwa kufurukuta kutokana na upepo uliokuwepo kwa wakati huo maana alionesha kuto kukubalika sana na wajumbe waliokuwa wakimzomea mara kwa mara alipokuwa akigawa vipeperushi vya wasifu wake huku wajumbe wakikejeli kwa maneno ya wazi kwamba huu sio wakati wa vipeperushi bali ni wakati wa vipeperushwa wakiwa na maana kuwa mwenye nguvu ndio mwenye nafasi ya kupata uongozi.

Na ndivyo ilivyo kuwa baadaye Deo au maarufu kama jah people kuibuka na ushindi mkubwa na dhamana ya kuongoza mkoa ikashikwa na mtu mwenye elimu ya ngumbaru na mangula kurudi zake njombe hapo ndipo ishara za wazi za kufa kisiasa kwa mangula kukaonekana wazi lakini juzijuzi tu hapa mangula kalamba dume kule dodoma na nyota yake kuanza kutamalaki tena na kuukwaa umakamu wa mwenyekiti wa chama Tanzania bara hivi ni sawa na kufufuka kisiasa.

Tukumbuke kuwa pia kuwa mangula ni kizazi cha wale wanasiasa wazalendo walitanguliza maslahi ya chama na taifa mbele badala ya ubinafsi, walipigania uhuru na walikula amini ya dhati ya kutumikia taifa na sio kutafuta ufahari wa fedha na umwinyi ,wao kwao cheo kilikuwa ni dhamana.

Sasa mangula kapewa rungu ataweza kukimbizana na mbio za dot komu za vijana ndani ya chama? Mimi naona ni changamoto kwake kuanza kukabiliana na wafanyabiashara, mafisadi, na makundi ya uchochezi na kuzirejesha ofisi za chama kuwa ni za kiitikadi na uadilifu na kuziacha ofisi za chama zilizogeuzwa sehemu ya magendo, ubinafsi, ubinafisishaji, ugenishaji wa mali za umma kwa kuvunja makundi ya wanyonyaji, kupe, wabaguzi wanyanyasaji na wakandamizaji ambao ndio wamehodhi madaraka ya chama na serikali kwa kuwageuza raia kuwa wakimbizi wa mifumuko ya bei katika nchi yao.

Mangula amekubali kusulubiwa msalabani kamayesu ili kukinusuru chama kabla ya uchaguzi ujao wa 2015 akiamini ataweza kuirejesha ccm kama ile ya wamu ya kwanza ya pili naya tatu iliyokuwa ikisimamia maslahi ya wakulima na wafanyakazi kila la heri Philipo Mangula shika tena hatamu hiki ni kipindi cha chukua chako mapema kabla hujawahiwa na wajanja.

Mangula amefufuliwa kisiasa ataweza kuongoza chama ambacho nguvu ya pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi??? Utaweza kurejesha heshima na haiba ya CCM iliyopotea miongoni mwa umma?

Kila la heri Mangula kupambana na kasi mpya ari mpya na nguvu mpya kwa kuwaletea wanachama imani namalizia kwa kusemakuwa naamini kuwa pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi.
 
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
13,377
Points
2,000
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
13,377 2,000
Nguvu ya pesa inanunua madaraka na madaraka yananunua uongozi

...ndugu Philip Mangula. Aliyeonesha umahili wake katika medani za kisiasa hapa nchini kwa wakati huo na falsafa ya uwazi na ukweli.

Philip mangula alimaliza uongozi wake wa chama cha ccm ...lakini alitoswa na Jakaya na kuamua kurudi zake huko Njombe kijiji cha Malinyi kuendelea na shughuli zake za kilimo cha viazi na nyanya na kupotea kabisa katika siasa.

Kama ujuavyo utamu wa madaraka, mangula aliamua tena kujitosa katika siasa alipojitokeza tena hadharani kuomba nafasi ya mwenyekiti wa chama mkoa wa iringa ...alishindwa kufurukuta ....waliokuwa wakimzomea mara kwa mara alipokuwa akigawa vipeperushi vya wasifu wake huku wajumbe wakikejeli kwa maneno ya wazi kwamba huu sio wakati wa vipeperushi ....

...mangula kurudi zake njombe hapo ndipo ishara za wazi za kufa kisiasa kwa mangula kukaonekana wazi lakini juzijuzi tu hapa mangula kalamba dume kule dodoma na nyota yake kuanza kutamalaki tena na kuukwaa umakamu wa mwenyekiti wa chama Tanzania bara hivi ni sawa na kufufuka kisiasa.

Tukumbuke kuwa pia kuwa mangula ni kizazi cha wale wanasiasa wazalendo walitanguliza maslahi ya chama na taifa mbele badala ya ubinafsi, walipigania uhuru na walikula amini ya dhati ya kutumikia taifa na sio kutafuta ufahari wa fedha na umwinyi ,wao kwao cheo kilikuwa ni dhamana.

Sasa mangula kapewa rungu.... .

Umesema Mangula amekabidhiwa rungu.

Mangula atakuwa ameshajifunza kuwa alifanya kosa....unapojiwekea miko ya kutokudokoa keki ya taifa, kutokuwa fisadi, kutokufanya ubadhirifu katika nchi ya wadanganyika unachukuliwa kuwa ni "mjinga", "bw.e.ge", mshamba...

Sasa ameshaona mabosi wake,Mkapa na wenzake na mali walizojigawia.....

Umesema kuwa anahasira? pia amekabidhiwa rungu?

Kama unafahamu utajiri,mali alizonazo leo...subiri 2015 ulete uzi mwengine utujuze kama atakuwa ameutupa uzalendo jalalani..uzalendo umemshinda au amezidiwa nguvu tu na ubinafsi?

Naogopa Kafara itakayogeuka kufuru.​
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,932
Points
1,500
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,932 1,500
Mangula kamata mwizi meeeeen
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,932
Points
1,500
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,932 1,500
Huyu mzee ni smart sana,hana longolongo,yeye ni kazi tu,atakuwa mwiba mkali sana kwa wapinzani,lets watch and see
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,932
Points
1,500
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,932 1,500
Hilo rungu alilokabidhiwa atakuwa anapiga kichwani tu bila kukwepesha,mana navomjua kwa kunyoosha mambo.jiandaeni kusambaratika kabla ya 2015
 
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
19,515
Points
1,500
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
19,515 1,500
Huyu mzee ni smart sana,hana longolongo,yeye ni kazi tu,atakuwa mwiba mkali sana kwa wapinzani,lets watch and see
Naanza kuliona anguko la ccm,yaani inaelekeza nguvu zake kupambana na upinzani badala ya kuishmamia serikali yake kutekeleza wajibu wake. kweli ccm imepoteza mwelekeo
 
Forum statistics

Threads 1,403,282
Members 531,135
Posts 34,419,680
Top