Mangula ataka suluhu na UKAWA

Mangula ataka suluhu na UKAWA

amba.nkya

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
446
Reaction score
131
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimetangaza kuwa kitaandaa mkutano wa faragha kwa viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na kuwaalika watu mashuhuri ili kutafakari hali na mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na kutafuta suluhu kabla halijaingia awamu ya pili ya majadiliano.

Bunge hilo lilikumbwa na mgawanyiko Aprili 16, mwaka huu baada ya wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake na kile walichosema upendeleo na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa TCD, Philip Mangula, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu kikao cha TCD kilichofanyika Jumapili iliyopita kwa lengo la kujenga maelewano katika Bunge Maalum la Katiba.

Mangula ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, alisema kamati ya ufundi (TC) ya TCD ilipendekeza uandaliwe mkutano wa faragha wa siku mbili ili kutafakari hali na mwenendo wa Bunge hilo ambalo linatarajia kukutana tena katika awamu ya pili na ya mwisho kwa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu.

Mangula alisema ilipendekezwa na TC ya TCD katika faragha hiyo wangealikwa pia baadhi ya watu mashuhuri nchini wajumuike na wajumbe wa TCD katika kupata maridhiano kuhusu mwenendo wa Bunge hilo kwa nia ya kulinusuru.

"Ni katika kupata ufumbuzi wa mwenendo mzima wa ushiriki wa vyama vyote vya siasa ambavyo ndiyo wadau wakuu na muhimu wa mchakato huu kabla Bunge la katiba halijaingia awamu ya pili ya majadiliano ambayo yataanza Agosti," alisema Mangula.

Alibainisha kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya baadhi ya vyama kususia Bunge hilo na kutoka nje ya Bunge Maalum la Katiba.

Wajumbe wa Ukawa waliosusia Bunge hilo ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi. Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa vyama vingine nje ya Ukawa walisusia bunge hilo.

Miongoni mwao ni Mwenyekiti wa United Democratic (UDP), John Cheyo; Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na Mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi.

Mangula alisema lengo na madhumuni ya majadiliano hayo ni kuona sababu zilizowafanya baadhi ya washiriki wa Bunge hilo kususia.

Kwa mujibu wa Mangula wajumbe wa TCD walishindwa kukamilisha maandalizi ya mkutano huo kutokana na kutokuwapo wawakilishi wa vyama vya Chadema na CUF ambao hawakuhudhuria ili kupata maelezo fasaha kuhusu sababu zilizowalazimisha kususia Bunge Maalum la Katiba licha ya kuwapo kanuni na taratibu za kutatua matatizo na kutokuelewana katika Bunge hilo.

"TCD ni kama imepasuka, tunataka kutanzua vyama sita vilitoka vyama 16 vilibaki na vyama vitatu vilirudi na hawa waliorudi wanasema walipotoka, walidhani ilikuwa kwa muda tu na wamerudi kuendelea," alisema na kuongeza:

"Ndiyo maana walirudi … tunataka njia nzuri ya kujenga na kuendeleza umoja wa kitaifa katika nchi yetu."

Kadhalika, Mangula alisema wajumbe pia walikubaliana kuitisha kikao cha Baraza la taifa la vyama vya siasa litakalojumuisha vyama vyote 22 vyenye usajili wa kudumu ili kuendelea kutafakari mchakato wa awamu ya pili ya Bunge Maalum la Katiba.

TCD inaundwa na vyama vyenye wabunge ambavyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP.

Wakati TCD inasaka mwafaka, CCM kilishatangaza kwamba hakitakuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo na Ukawa wala kuiruhusu serikali yake kuwabembeleza wajumbe wa umoja huo kurejea bungeni.

Uamuzi huo ulifikiwa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho mwezi uliopita na kwamba hatua inayofuata ni kwa viongozi wake nao kwenda kwa wananchi kuwaeleza ukweli kama Ukawa wanavyofanya.

Sababu kubwa iliyowafanya Ukawa kususia Bunge hilo ni uamuzi wa CCM kukataa mapendekezo ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba sura ya kwanza na ya sita kuhusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa Muungano.

Rasimu hiyo inapendekeza kuitwa Shirikisho na muundo wa serikali tatu, mapendekezo ambayo CCM inayapinga.

Akitangaza uamuzi wa Ukawa kujiengua kwenye Bunge hilo, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa wamechoshwa na ubaguzi na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba kwa maana hiyo wanajiondoa bungeni ili kuwaacha ‘Nterahamwe' kuendelea na ubaguzi wao.

Chanzo:
Nipashe - 11/06/2014
 
Katiba ya CCM tunasema NO! Rasimu ya Warioba ndio inakubalika.
 
Mkuu si Wasira aliapa kule Zanzibar kuwa hawako tayari kupewa masharti na UKAWA sa kikao cha nini?
 
Mkuu si Wasira aliapa kule Zanzibar kuwa hawako tayari kupewa masharti na UKAWA sa kikao cha nini?
Mkuu, maji yamewafika shingoni haya majitu, UKAWA ni mwiba kwao
 
Yako wapi yale maneno ya yule mpiga debe wao kwamba "Ukawa wasirudi kutuvurugia utulivu wa bunge letu la katiba" ??

CCM kama mnataka UKAWA warudi Bungeni na nyie mjirekebishe matendo yenu, kinachojadiliwa mule ni Rasimu ya katiba iliyowasilishwa na Jaji Joseph Sinde Warioba na si vinginevyo!!
 
CCM msiwe na akili za kijima za mtu mmoja @nape nnauye
 
Mbowe: CCM ni Mbugi

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amekifananisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mchezo wa ‘Mbugi’. Kwa mujibu wa Mbowe, Mbugi ni mchezo wa soka usio na sheria, wala refa.
Alisema kwenye mchezo wa Mbugi hakuna idadi kamili ya wachezaji, kila mchezaji akiingia anachezea timu anayotaka, katikati ya mchezo anaweza kubadilisha timu na kuchezea timu nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza Baraza jipya la Mawaziri Kivuli lenye ya wajumbe wa UKAWA, Mbowe alisema wanachosema na kufanya CCM kwa sasa ni sawa na Mbugi, kwani hawana kanuni na kila mtu anaweza kusema anachotaka.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na kauli na misimamo tofauti kuhusu UKAWA zinazotolewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Akitolea mfano alisema hivi karibuni Kamati Kuu ya CCM ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni mjumbe, wamepitisha azimio la kutoshughulika na UKAWA kwani wameamua kutoka kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
“Pinda huyo huyo akihitimisha hotuba yake, anawasihii UKAWA kurudi bungeni. Juzi Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano), anasema UKAWA walitoka bila sababu, watarudi bila sababu, lakini ukimsikiliza Nape Nnauye na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana wanasema UKAWA wasibembelezwe, waachwe wabaki nje ya Bunge. Hii ni Mbugi.
“Kinana kaja kavua shati kaingia kwenye Mbugi, Nape naye Mbugi, Wassira katoa shati kaingia kwenye mchezo Mbugi, hawana kanuni, sheria. CCM ni Mbugi,” alisisitiza Mbowe.
 
Mkuu, maji yamewafika shingoni haya majitu, UKAWA ni mwiba kwao

Tatizo ni kuwa CCM waneamua kuwa wapinzani wa rasmu waliyoiandaa na waliyoiwasilisha wenyewe. Sasa kwa hili sielewi kama wanajiandaa kuwa wapinzni2015.
 
Taarifa hii imeandikwa tofauti na ile ya HabariLeo ambayo inadaiwa Mangula alisema kuna mashirika ya nje yanawalipa Wajumbe wa Ukawa kwenye bunge la katiba mamilioni ya pesa na kuwa walitakiwa viongozi hao wakalielezee hilo huko TCD. Swali langu ni kwa nini vyombo vya dola visiwafuate hao watoaji na wapo kwani wa hongo hiyo ya wazi wazi na yenye madhara kwa nchi yetu wakawa hoji na kuwa chukulia hatua. Hizi siasa za uchonganishi hazitatufikisha mbali bali zitaliaribu taifa letu.

Ninachokiona hapa kwa mawazo yangu pande hizi mbili (ukawa na CCM) kila moja kwa sababu zake hawataki bunge la katiba liendelee. Ukawa wanajua kabisa CCM hawayakubali mapendekezo ya Tume ya Warioba ambayo ndiyo msingi wanaouunga mkono kwa Katiba mpya na kuwa hawawezi kuwashawishi wenzao kwa hoja kubadili msimamo huo. CCM hawakuukubali kuanzia mwanzo mchakato huu wa katiba mpya na wameingia katika mchakato siyo kama taasisi bali kwa vile mwenyekiti wao aliamua, na kwa jinsi hiyo hawaoni umuhimu wa kupata katiba mpya ambayo itaondoa kwa kiasi kikubwa mfumo na muundo uliopo. Na kwa jinsi hii sasa juhudi ya makundi haya mawili ni kutaka kuonyesha umma ni nani kavuruga mchakato wa katiba mpya na siyo kutafuta juhudi za kuridhiana na kuuendeleza mchakato.
 
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimetangaza kuwa kitaandaa mkutano wa faragha kwa viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na kuwaalika watu mashuhuri ili kutafakari hali na mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na kutafuta suluhu kabla halijaingia awamu ya pili ya majadiliano.

Bunge hilo lilikumbwa na mgawanyiko Aprili 16, mwaka huu baada ya wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake na kile walichosema upendeleo na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa TCD, Philip Mangula, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu kikao cha TCD kilichofanyika Jumapili iliyopita kwa lengo la kujenga maelewano katika Bunge Maalum la Katiba.

Mangula ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, alisema kamati ya ufundi (TC) ya TCD ilipendekeza uandaliwe mkutano wa faragha wa siku mbili ili kutafakari hali na mwenendo wa Bunge hilo ambalo linatarajia kukutana tena katika awamu ya pili na ya mwisho kwa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu.

Mangula alisema ilipendekezwa na TC ya TCD katika faragha hiyo wangealikwa pia baadhi ya watu mashuhuri nchini wajumuike na wajumbe wa TCD katika kupata maridhiano kuhusu mwenendo wa Bunge hilo kwa nia ya kulinusuru.

Ni katika kupata ufumbuzi wa mwenendo mzima wa ushiriki wa vyama vyote vya siasa ambavyo ndiyo wadau wakuu na muhimu wa mchakato huu kabla Bunge la katiba halijaingia awamu ya pili ya majadiliano ambayo yataanza Agosti, alisema Mangula.

Alibainisha kuwa hatua hiyo ilichukuliwa baada ya baadhi ya vyama kususia Bunge hilo na kutoka nje ya Bunge Maalum la Katiba.

Wajumbe wa Ukawa waliosusia Bunge hilo ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi. Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa vyama vingine nje ya Ukawa walisusia bunge hilo.

Miongoni mwao ni Mwenyekiti wa United Democratic (UDP), John Cheyo; Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na Mwenyekiti wa National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi.

Mangula alisema lengo na madhumuni ya majadiliano hayo ni kuona sababu zilizowafanya baadhi ya washiriki wa Bunge hilo kususia.

Kwa mujibu wa Mangula wajumbe wa TCD walishindwa kukamilisha maandalizi ya mkutano huo kutokana na kutokuwapo wawakilishi wa vyama vya Chadema na CUF ambao hawakuhudhuria ili kupata maelezo fasaha kuhusu sababu zilizowalazimisha kususia Bunge Maalum la Katiba licha ya kuwapo kanuni na taratibu za kutatua matatizo na kutokuelewana katika Bunge hilo.

TCD ni kama imepasuka, tunataka kutanzua vyama sita vilitoka vyama 16 vilibaki na vyama vitatu vilirudi na hawa waliorudi wanasema walipotoka, walidhani ilikuwa kwa muda tu na wamerudi kuendelea, alisema na kuongeza:

Ndiyo maana walirudi  tunataka njia nzuri ya kujenga na kuendeleza umoja wa kitaifa katika nchi yetu.

Kadhalika, Mangula alisema wajumbe pia walikubaliana kuitisha kikao cha Baraza la taifa la vyama vya siasa litakalojumuisha vyama vyote 22 vyenye usajili wa kudumu ili kuendelea kutafakari mchakato wa awamu ya pili ya Bunge Maalum la Katiba.

TCD inaundwa na vyama vyenye wabunge ambavyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP.

Wakati TCD inasaka mwafaka, CCM kilishatangaza kwamba hakitakuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo na Ukawa wala kuiruhusu serikali yake kuwabembeleza wajumbe wa umoja huo kurejea bungeni.

Uamuzi huo ulifikiwa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho mwezi uliopita na kwamba hatua inayofuata ni kwa viongozi wake nao kwenda kwa wananchi kuwaeleza ukweli kama Ukawa wanavyofanya.

Sababu kubwa iliyowafanya Ukawa kususia Bunge hilo ni uamuzi wa CCM kukataa mapendekezo ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba sura ya kwanza na ya sita kuhusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa Muungano.

Rasimu hiyo inapendekeza kuitwa Shirikisho na muundo wa serikali tatu, mapendekezo ambayo CCM inayapinga.

Akitangaza uamuzi wa Ukawa kujiengua kwenye Bunge hilo, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa wamechoshwa na ubaguzi na uchakachuaji wa Rasimu ya Katiba kwa maana hiyo wanajiondoa bungeni ili kuwaacha Nterahamwe kuendelea na ubaguzi wao.

Chanzo:
Nipashe - 11/06/2014
kwahiyo wanakutana na ukawa ili wajadiliane namna ya kupinga rasimu ya katiba? Wajadili jinsi ya kumtukana mzee warioba? Ccm ndo inayo takiwa kujirudi na itangaye kuwa sasa imeacha myenendo yake ya awali wakifanya hivo ukawa itakosa hoja!
 
Huu ndio ukomavu wa kisiasa,wale mnaopinga msimamo huo hamjui mnalolitenda wala maana ya majadiliano ya pamoja kwa mustakabali mwema wa taifa,binafsi nimefurahishwa na kauli hii,jamii inapokuwa kwenye total political dilemma hakuna mwenye kuendelea kutunisha msuli bali jambo jema ni wote kwa pamoja kudefine stake zetu na kukaa mezani kukubaliana kwa ajili ya manufaa ya taifa.Ni lazima tukubali kukosoa na kukosolewa na mshindi apatikane kwa hoja malidhawa inayoyabeba maslahi mapana ya jamii na si kubeba maslahi finyu ya wachache.
 
Hivi huyu Mzee Mangula hamalizi HONEY MOON! Simba ndiye mnyama anayeamika kuwa na HONEY NDEFU. Sasa naona mzee Mangula anataka kungia in the Books of Guinness world records kwa kuvunja urefu wa honey moon za ma-Simba.
 
Huu ndio ukomavu wa kisiasa,wale mnaopinga msimamo huo hamjui mnalolitenda wala maana ya majadiliano ya pamoja kwa mustakabali mwema wa taifa,binafsi nimefurahishwa na kauli hii,jamii inapokuwa kwenye total political dilemma hakuna mwenye kuendelea kutunisha msuli bali jambo jema ni wote kwa pamoja kudefine stake zetu na kukaa mezani kukubaliana kwa ajili ya manufaa ya taifa.Ni lazima tukubali kukosoa na kukosolewa na mshindi apatikane kwa hoja malidhawa inayoyabeba maslahi mapana ya jamii na si kubeba maslahi finyu ya wachache.
Aongeee na ccm wenzake kwanza juu ya kujadili rasimu iliyo mezani.Sii ile ya mfukoni kwa Nape
 
Back
Top Bottom