Mangula acheza rafu CHADEMA

Mangula acheza rafu CHADEMA

KIMBURU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
210
Reaction score
189
MPANGO mchafu wa kukichafua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa umefichuka, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Philipo Mangula akituhumiwa kuratibu harakati hizo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya CCM, zimebainisha kuwa, chama hicho kimechapisha mamia ya kadi za CHADEMA ambazo zimesambazwa kwa watu maalumu walioandaliwa ambao wameambiwa wazirejeshe leo wakati wa mkutano wa hadhara na kumkabidhi Mangula, wakidai wameihama CHADEMA.

Imebainika kuwa, zaidi ya wanafunzi 200 wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa tayari wamekabidhiwa kadi hizo, na fedha za kujikimu ambapo watajitangaza kama wana-CHADEMA waliohamia CCM baada ya kuchoshwa na upinzani katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa.
Mbali na kadi, CCM pia imetengeza fulana za CHADEMA walizopewa wanafunzi hao, na kwamba chama hicho kimemwaga maelfu ya fedha kwa wasomi hao kama njia ya kufanikisha mpango huo.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Mtama Joseph amekiri kusikia taarifa hizo, lakini akadai kuwa kama ni kweli basi, utakuwa ni mpango unaotumika na watu waliopoteza mwelekeo.
“Ni kweli kuna taarifa hizo zimezagaa hapa chuoni kwamba kuna wanafunzi 200 ambao wamepewa sh 5,000 kila mmoja, na kadi zenye nembo ya CHADEMA ili warudishe kwenye mkutano wa CCM utakaofanyika kesho (leo) katika viwanja vya Mwembetogwa,” alisema.
Mtama alisema kama habari hizo ni za kweli, litakuwa jambo la kusikitisha na linaloonesha kuwa watu walioshindwa kufikiri na kuwajibika hutumia mbinu chafu kwa kuwa hawana fikra zingine zaidi ya rushwa.
Mmoja wa vijana wanaodaiwa kutumiwa katika mpango huo (jina limehifadhiwa) amekiri kuwa miongoni mwa viongozi wanaoratibu mpango huo na kwamba yeye na wenzake wameahidiwa sh 500,000 kila mtu pindi watakapofanikisha hujuma hiyo.
Kijana huyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa kuhofia usalama wake, alisema tayari kuna vijana 17 ambao wameandaliwa pamoja na kuratibu, lakini pia kufanya kazi ya kuichafua CHADEMA kwa namna watakavyoelekezwa pindi wakifika mkoani hapa kwa ajili ya mikutano ama shughuli nyingine.
Mbali na hilo, kijana huyo alisema CCM pia imeandaa magari kusomba wanachama wake kutoka vijijini kuletwa katika mkutano wa leo kwa madai ya kutaka ionekane ina wanachama wengi, hivyo kuondokana na aibu ya kukosa watu katika mkutano wake.
Katibu wa CHADEMA Manispaa ya Iringa, Suzan Mgonukulima alisema kuna mbinu chafu zilizobainika kutumika kuhujumu CHADEMA ambazo wananchi wanatakiwa kuwa nazo makini.
Alisema kufichuka kwa siri hizo, ni ishara wazi kuwa watu wanaojitangaza kurudi CCM sio wanachama halisi, bali waigizaji na kuonya kuwa mchezo huo ni ishara ya wazi kuwa sasa serikali inatishiwa na CHADEMA.
Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi (CHADEMA) ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji ya wilaya, alisema propaganda za CCM zimepitwa na wakati na kwamba ni dalili za kutapatapa kwa sababu wanajua kuwa mwaka 2015 wanaachia ngazi.
Source: Tanzania Daima

My take:
Haya yaliyoandikwa na Gazeti hili yana ukweli kabisa, mimi mwenyewe ni miongoni mwa watu waliofuatwa na magamba kutimiza mpango wao wa kishenzi bt nikagoma coz sikutaka kujidhalilisha kwa kufanya mambo ya kishenzi yasiyokuwa na tija katika maisha yangu.
CCM wanafanya mambo ya kitoto bila kufikiria faida yake ni ipi. Kwa kifupi wanajidanganya wenyewe, watu wa Iringa walishaichoka CCM muda mrefu na hawako tayari kuendelea kudanganywa na Magamba. VIVA CHADEMA, VIVA OUR BELOVED Rev. P. MSIGWA.
 
hizo mbinu mbona ni za kitoto...kama wameshindwa kuongoza nchi si wakabidhi kwa wananchi
 
Wasomi wa chuo kikuu kusaliti umma wakiwa masomoni! Wakipata dhamana ya kuongoza nchi tutegemee nini? Wananchi ni vema sasa kuchukua hatua dhidi ya mbegu hii mbaya ya usaliti inayopandikizwa na kurithishwa kwa kundi hili. Bodaboda wa Iringa kamata hawa watu muwafundishe adabu kama mbunge wa Masasi.
 
Mwanangu kashapewa elfu hamsini na kadi ya chadema atakayo mkabidhi mangula,na ameingia mtini.
 
Ccm byeeeeeeeeeeeeeeeeeeee b4 2015
 
Wakipanda jukwaani wataje yeye kadi yake namba ngapi amepewa ofice ipi ya cdm
 
aibu kubwa kwa chama kinachojitanabahisha na amani na utulivu kujihusisha na maigizo kama haya!..uzoefu wao wa miaka hamsini ndio huu.Mangula kachoka. kinana mdebwedo na ccm kaputi...
 
Huyu si ndiye alisema atatumia miezi sita kwenye mapambano ya rushwa? Sasa mbona anatumia muda wa mwezi mmoja pekee, kufanya yale yale au yanayofanana na hayo waliyofanya wenzake ambao alionesha kwa maneno kuwa anataka kupambana nao?

This is pure Chichidodo type. Kweli CCM na rushwa, ni sawa na ngozi na mwili! Ukiiondoa rushwa ni sawa umeondoa ngozi kwenye mwili. Cant survive without.
 
Wasomi.....very stupid tumeshapoteza hata heshima ya kuitwa wasomi..sh. 5000.......njaa mbaya sana,......makamanda bodaboda halali yenu hao wahuni.....watakuwa ndio wezi wa pikipiki hao kwa njaa zao hizo.
 
Ni vuzuri kuweka bayana uongo wa ccm ili watanzanie wajue jinsi ambavyo wamekuwa wakiongozwa kinafiki na watu hawa. Tunaweka mikakati ya kutuondoa tulipo wao wanaweka mikakati ya kuturudsha nyuma. Wataja haibika na anguko lao la karibia..
 
Utachafua chadema hutachafua mawazo ya watanzania wote mangula

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu KIMBURU asante sana kwa taarifa, kinacho nisikitisha ni hawa vijana wetu tunaowatarajia katika harakati za ukombozi wa nchi hii kumuondoa mkoloni mweusi kukubakli kutumiwa kama toilet paper. Hii sakata limenikumbusha umuhimu wa barafu (kisamurai) pindi tulipokuwa tukisoma pale SHYCOM. Hivyo ni vyema Mkwawa ikaanzisha Barafu na kuwashughulikia hao wanao dhalilisha chuo kwa mujibu wa kanuni za barafu, na ikibidi watakao bainika watengwe na jumuia ya wanachuo kama wasaliti wa mabadiliko.
 
Mkuu KIMBURU asante sana kwa taarifa, kinacho nisikitisha ni hawa vijana wetu tunaowatarajia katika harakati za ukombozi wa nchi hii kumuondoa mkoloni mweusi kukubakli kutumiwa kama toilet paper. Hii sakata limenikumbusha umuhimu wa barafu (kisamurai) pindi tulipokuwa tukisoma pale SHYCOM. Hivyo ni vyema Mkwawa ikaanzisha Barafu na kuwashughulikia hao wanao dhalilisha chuo kwa mujibu wa kanuni za barafu, na ikibidi watakao bainika watengwe na jumuia ya wanachuo kama wasaliti wa mabadiliko.
Kinachowaponza hawa watoto ni njaa coz semester inaelekea ukingoni na boom limekata. Ndio maana hata wasichana wanaishia kujiuza kwa bei rahisi. CCM wanatumia advantage ya umaskini kukamilisha mission zao. Lakini utafika wakati wananchi watasema ukweli kupitia box la kura.

 
Kinachowaponza hawa watoto ni njaa coz semester inaelekea ukingoni na boom limekata. Ndio maana hata wasichana wanaishia kujiuza kwa bei rahisi. CCM wanatumia advantage ya umaskini kukamilisha mission zao. Lakini utafika wakati wananchi watasema ukweli kupitia box la kura.

Mkuu Kimburu mie nina mtizamo tofauti, kinacho wasumbua hawa vijana siyo njaa bali ni uwezo wao wa kufikiria umefikia ukomo na elimu yao haina msaada tena, kama kweli ni njaa Tsh.5000/= itamsaidia nini?
 
Back
Top Bottom