BETTY BHOKE
DAILY NEWS
...It is alleged that on March 15, this year.......for costs of staying in hospital for one week and $7,000 for two weeks in hotel accommodation for her and three weeks for her attendant.
...demanding for specific damages of 1,575,000/- and $24,120 and general damages of 135m/-
...Some 20 minutes into the party room, the advocates went to their table
...The assault lasted nearly four minutes, during which Ms Kinambi's friends pleaded with the advocate not to assault her to no avail. Finally, Good Samaritans interceded, pleading with him not to hurt the woman.
... loss of reputation as an unmarried Muslim girl
Hii habari, kama ni kweli, inasikitisha sana. Japo imekaa kidaku na kihohehahe.
Hivi huyu mwanamke mfanyabiashara ambae DAILY NEWS wamemwita "muslim girl" ana umri gani huyu?
Gazeti linasema kipigo kimetokea March 15 mwaka huu. Siku tano zilizopita. Halafu victim anadai damages za matibabu ya wiki tatu! Toka lini? How? I mean, how?
Gazeti linasema "the advocates went to their table." The "advocates," yupi hapo katajwa zaidi ya huyo Magai?
DAILY NEWS wanasema Ms. Kinambi kadai "damages of 1,575,000/- and $24,120 and general damages of 135m/-" Mwandishi kwanza kakoroga dola na shillingi, halafu kachanganya format ya kuandika namba zote (...,000) na kutumia kifupi (135m), halafu kajaribu ku break down the damages akatofautisha 1,575,000/ na $24.120 bila kusema amezitenga kwa nini. Maana zote ni damages! Isitoshe, damages na general damages kwa hapo tofauti yake sijui ni nini walahi. Yani vitu vimekaa kama vimeandikwa kijinga kijinga hivi. Amedai damages na general damages!
News story iko based on "alleged." Lakini hawasemi alleged na nani. Ukisoma gazeti lenye hadhi duniani utakuta, kama wanaelezea kisa kama hiki kilichoenda mahakamani, watasema whether imekuwa alleged kwenye court papers au kama ni eye witness, ama mwandishi mwenyewe kachunguza evidence fulani and so forth. Hawa hawajasema imekuwa alleged wapi, kwenye stendi ya magari ya Posta-Baharini?
Na huyo eye witness wao nae atakuwa ali miss the action vile vile. Wanasema huyu lawyer alikutana na kina mama kwenye meza, hapakuwa na tukio, wakatengana, ikaja baadae lawyer akaibuka ukumbi wa densi kuanza kumpiga mtu kwa dakika nne, huku ana shout kumlazimisha aondoke hapo "for no apparent reason." Well, ina maana kati ya kukutana mezani na pale kwenye kipigo jamaa alirukwa akili, no words were exchanged in the interim, nothing. Salaam, kipigo! Halafu wakati wa kipigo cha dakika nne ina maana lawyer alikuwa anarudia neno hilo hilo ondoka ondoka! Well, wamesema alikuwa akitukana. Alikuwa anamwambiaje na hayo matusi? We mwongo? Unanifukuzia ndege? Malaya? What? Hakutoa clue? Talking about "for no apparent reason," no no no, huyu shahidi wa DAILY NEWS aliona malue lue kwa sababu s/he missed the action!
Mwandishi anasema wakati wa kipigo kulikuwa na hawa marafiki wa Ms. Kinambi wanasihi asiendelee kumpiga, dakika 4. Halafu wakaja wasamaria wema "wakaingilia kwa kumsihi asimuumize ." Yani walichofanya wasamaria wema "walioingilia" na walichofanya wale ambao hawakuingilia ni kile kile, kumsihi asiendelee kumpiga! Tunaongelea the DAILY NEWS, historically, the paper of record la Tanzania.
Hadithi ya Daily News imekaa kijinga kijinga hivi.