Maneno yetu yanavyopishana na vitendo vyetu ndio siasa za Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Taarifa nilizozipata kutoka kwa viongozi wa CHADEMA Morogoro ni kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo limezuia sherehe za mahafali ya vijana wa CHADEMA wa vyuo vikuu vya Morogoro (CHASO) kwa madai ya kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani. Mahafali hayo yalikua yafanyike kesho na Mgeni Rasmi alikua Mhe.Edward Lowassa, Waziri mkuu wa zamani.

Wakati huohuo mahafali ya vijana wa CCM mkoani humo, yataendelea hapo kesho kama ilivyopangwa katika ukumbi wa Hoteli ya Savoy iliyopo mjini Morogoro. Viongozi wa CCM wamedhibitisha mahafali hayo kuwepo na kwamba hadi jioni ya leo hakuna taarifa yoyote rasmi waliyopewa kuwazuia
 
Nawahakikishia kwa mtindo huu mpya ulioanzishwa tegemeeni matukio ya mapigano baina ya wanaupinzani upande mmoja na upande mwingine CCM wakisaidiwa na polisi; ni suala la muda tu kabla hali ya Zanzibar haijahamia huku.
Hivi mbona vyama vya siasa vikiachiwa vikafanya siasa zao hakunaga baya lolote... hii hofu ya ccm imetokea wapi kuna nini nyuma ya pazia wanahofia?
 
It's a sign of weak leadership, maana moja ya sifa kuu ya kiongozi dhaifu ni kutokupenda hoja au mambo tofauti na yake. Unapokataza watu wasifanye jambo kwa madai ya hali ya kiusalama halafu wafuasi wako unawaruhusu tafsiri yake ni nini?
 
Hatari sana Mkuu
 
Intelijensia imeshaona jamani si kwisha?? Wakija Polisi kuwalinda Chaso mwaweza kuwa-mistake kuwa wana nia mbaya mkawadhuru. CCM hawana beef na Polisi.
Yawezekana pia mgeni rasmi wenu akawasema vibaya viongozi wa kitaifa, kumbukeni ule ni mkusanyiko wa hadhara. Likitamkwa neno pale, nnani atalizuia?
Unyonge sio sifa mbaya, tungojee 2020 tuwarudie wale wale wananchi. Utulivu si ujinga, unaweza kusema mengi zaidi kwa kutulia. Mbona wabunge waliamua kutoka nje na kuwaachia ukumbi wajiamulie mambo yao. Chaso tulizeni mzuka ( I quote Sugu) ulimwengu unaona
 
Lakini

Lakini wao wakiwasema vibaya viongozi wa upinzani hadharani ni sawa?
 
Hakuna dhambi mbaya kama uoga fanyeni hayo mahafali yenu kwa nguvu.
 
Intelijensia imeshaona jamani si kwisha?? Wakija Polisi kuwalinda Chaso mwaweza kuwa-mistake kuwa wana nia mbaya mkawadhuru. CCM hawana beef na Polisi.
Yawezekana pia mgeni rasmi wenu akawasema vibaya viongozi wa kitaifa, kumbukeni ule ni mkusanyiko wa hadhara. Likitamkwa neno pale, nnani atalizuia?
Unyonge sio sifa mbaya, tungojee 2020 tuwarudie wale wale wananchi. Utulivu si ujinga, unaweza kusema mengi zaidi kwa kutulia. Mbona wabunge waliamua kutoka nje na kuwaachia ukumbi wajiamulie mambo yao. Chaso tulizeni mzuka ( I quote Sugu) ulimwengu unaona
Intelijensia inaona chadema tu?
 
Jamaan naombeni kujunzwa haya mahafali ya kichama yalikuwepo tokea zamani au miaka hii ya karibuni?
 
Watanzania shida ya siyo mahafali wana shida nyingi maji, elimu, barabara, afya.
 
Taarifa nilizozipata kutoka kwa viongozi wa CHADEMA Morogoro ni kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo limezuia sherehe za mahafali ya vijana wa CHADEMA wa vyuo vikuu vya Morogoro (CHASO) kwa madai ya kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani. Mahafali hayo yalikua yafanyike kesho na Mgeni Rasmi alikua Mhe.Edward Lowassa, Waziri mkuu wa zamani.

Wakati huohuo mahafali ya vijana wa CCM mkoani humo, yataendelea hapo kesho kama ilivyopangwa katika ukumbi wa Hoteli ya Savoy iliyopo mjini Morogoro. Viongozi wa CCM wamedhibitisha mahafali hayo kuwepo na kwamba hadi jioni ya leo hakuna taarifa yoyote rasmi waliyopewa kuwazuia

hao viongozi wa ccm wamekuthibitishia ww kuwa mahafali yatakuwepo? weka source, sio kutafutiza vihoja, mnabaki kulialia kama mad*m.
 
Watanzania shida ya siyo mahafali wana shida nyingi maji, elimu, barabara, afya.
Miaka 54 ya Uhuru tumeshindwa,tutaweza kweli kwa miaka kumi tu? Inabidi tupige marufuku na mikusanyiko ya harusi,misiba nk.otherwise hatutaweza kuyatatua hayo matatizo
 
Back
Top Bottom