Maneno yanayoishi toka utotoni hadi utu uzima,

Maneno yanayoishi toka utotoni hadi utu uzima,

Gmarra

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
516
Reaction score
506
Habari za weekend Wakuu

Mimi nikijana Mwenye umri wa miaka 20s.Bila kuchelewa niende moja kwa moja kwenye mada.
Pindi nilipokuwa nasoma shule ya msingi & secondary, Ambao ni umri ambapo watoto huwa na uwezo wa kuelewa na kuchanganua mambo, kuna maneno ambayo nilikuwa naambiwa au kuskia wenzangu wakiambiwa na Wazazi, Walezi na hata Walimu wao, Ambayo naweza sema yananisaidia/ yanaishi mpaka sasa, Baadhi ni kama:

1.Ukitaka kufanya kitu ambacho unajua fika hutokikamilisha, Bora
usikifanye maana itakuwa ni uchafu, kwani kila kitu kinapofanyika huhitaji pesa na mda, ili kikamilike, hainabudi kuacha kufanya kitu kingine ( opportunity cost), kwani hivi vitu (mda na pesa) vikipotea huwa havijirudii tena.

2.Kwenye mambo yamapenzi, Kipindi naingia umri wa kibalehe, "Usije ukapenda kuwa karibu na wake za watu"aliniambia Mzazi wangu bora uwe na mtoto wa mtu lakini si mke wa mtu. kwani hicho kitu kinaweza kusababisha aibu, kupoteza mali , kifo na hata ulemavu wa kudumu.
.
3.Kuwa na wapenzi wengi sio ufahari, bali ni ujinga tu. Itakupelekea ushindwa kupiga hatua kwenye nyanja kimaendeleo, kwani budget ya kipesa na mda itakuwa ngumu sana, Maranyingi kichwani utakuwa na kazi ya kuandaa timetable usijulikane na hata wao (wanamake) wasijuane. Kwahivyo hutofiria mambo ya maendeleo.

4.Umhimu wa siri, waswahli husema " hakuna siri ya watu wawili'. Ukisikia mtu ameaga dunia basi ujue kuna vitu ambavyo alifanya katika uhai wake hakuwahi kuvisimlia/ kumshirikisha Mtu mwingine, si kila kitu lazima umwambie rafki, ndgu au mke wako, kwani husaidia kutunza utu wako na heshima kwa jamii inayokuzunguka, pia ni vigumu sana kumjua mtu mzuri na mbya kwako.

5. Usifanye mambo kwa kufuata mkumbo,Kwani kitu cha kipumbavu kitakuwa cha kipumbavu tu hata kama watu milioni kumi wakisema kitu hicho ni kizri. Ni mhimu kufanya jambo ambalo unaona ni zuri kwako na jamii inakuzunguka pasipo kuangalia/ kusikiliza watu wanasema nni juu ya hicho kitu.

6. Usiige kila kitu. Sio kila kitu wanachofanya wezako nawe lazima ufanye,( effect of peer group), hii kitu ilinisaidia sana Mimi nilitokea shule moja ya msingi ambayo ilikuwa kijijin, na secondary nilienda kusoma shule ambayo ilikuwa katikati ya mji, Huko nilikukutana na marafiki wengi na waaina mbalimbali mfano; wavuta bangi, na wale ambao walijihusisha na mapenzi. Japo nilikuwa nashinda nao lakini sikuwahi hata maramoja
kuiga hivyo vitu.

7.Jifunze kusamehe. Katika maisha jambo zuri na njia nzri ya kufkia malengo , Ni kuwa na mazoea ya kusamehe kwani inawezekana yule uliyemkosea au aliyekukosea leo, kesho au keshokutwa atahitaji msaada kutoka kwako au wwe Utahitaji msaada pia.

Nawe andika Yale ambayo uliyasikia ulipokuwa mdogo, lakini bado yanaishi mpaka sasa.Ili tupate kujifunza.
 
Tanzania ni nchi maskini.
Tanzania ni nchi tajiri.

Huwa sielewi nishike lipi kati ya hayo.
 
"Mimi ni mwanaume" na kweli mpaka leo mimi ni mwanaume.
 
Mimi niliambiwa kama hutakua mwaminifu katika vitu vidogo basi hata ukipewa vitu vikubwa hutakua na uaminifu navyo!!!
 
rafiki wa kweli na msiri wako ni mama yako mzazi na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom