Kaaya10
Member
- Dec 11, 2017
- 37
- 53
Ipo nguvu katika maneno. Maneno yanaumba. Ukweli ni kwamba maneno yanauwezo mkubwa sana wa kuathiri maisha ya mtu iwe ni chanya+ au katika mwelekeo Hasi- kwa sababu Imani ya mtu katika jambo fulani huja kwa kusikia au tuseme miongoni mwa njia za kujifunzia ni kwa kusikia.
Kama tunavyojifunza kuongea kwa kusikia ndivyo na tabia tunajifunza kwa kusikia. Kuna maneno Fulani ukiyasikia hususani kwa watu wako wa karibu unaamini huo ndio ukweli au uhalisia wa maisha.
Kuna maneno katika hali ya kawaida ukimwambia mtu anakwambia futa hayo maneno maana anaamini yataambatana na uhalisia wa hilo jambo kutokea.
Vivyo hivyo katika masuala ya kiuchumi, yapo maneno tumeyasikia sana kama vile PESA MWANAHARAMU, PESA HAZIOTI JUU YA MITI, PATA PESA TUJUE TABIA YAKO, PESA NI CHANZO CHA MAOVU, NI RAHISI NGAMIA KUPENYA KWENYE TUNDU LA SINDANO KULIKO TAJIRI KUURITHI UZIMA WA MILELE.
Haya maneno mara nyingi yameingia kwenye nafsi zetu na kuweka mgomo wa kutafuta pesa au ukizipata yanakulazimisha kuzitumia ziishe ili usiwe miongoni mwa matajiri ukaukosa ufalme, au ukawa na pesa ukawa na tabia mbaya au ukafanya uovu.
Haya maneno yameathiri familia nyingi sana katika kujitafutia fedha utasikia hata mtu anakwambia utakua masikini kama Fulani, Maneno ni roho na yanaweza kujenga kitu kwenye fikra za mtu na kuathiri kabisa namna anavyofanya maamuzi hususani kwenye masuala ya fedha.
Kuna haja ya kujitathmini na kuangalia ni maneno gani uliyasikia na kuambiwa ambayo yameathiri maisha yako kwa namna yeyote na kukurudisha nyuma kiuchumi.
Utasikia mtoto wa nyoka ni nyoka wakimaanisha lazima kuna vitu unarithi kutoka kwa wazazi na ndio hayo maneno. Utajiri na umasikini hufuata mkondo hata elimu ufuata mkondo kwa sababu ya maisha ya nyumbani.
Mzazi mwenye kipato kizuri anamnenea mwanae maneno ya kufanya nae apate motisha wa kufanya kazi na kujipatia maendeleo ya kiuchumi.
Karibu ujifunze nasi
Kumbuael Yesaya Kaaya 0769160382
Kaaya2012@gmail.com