Maneno ya Shangazi yametimia

Maneno ya Shangazi yametimia

Joined
Jun 12, 2015
Posts
58
Reaction score
24
Habari wa kuu,

Nakumbuka kitambo siku moja nilikuwa napiga story na shangazi Yangu kuhusu maswala ya ndoa ndipo akaniuliza kuwa ninapenda kuoa mwanamke wa namna gani, nikamwambia ninapenda mwanamke mzuri sana ndio awe mke wangu,lakini yeye akaniambia namnukuu "wanawake wazuri kwa muonekano wengi wanamatatizo sana.

Wengi huwa hawana malengo na hawawezi kuvumilia shida,ukiwapa ugali wa dona na chips yai lazima watachagua chips yai kwa sababu wanapenda vitamu na siyo vitu vyenye faida,wanawake wazuri wanavitimbi ambavyo wanaume wengi hawawezi kuvumilia, mwanangu oa mwanamke mwenye uzuri wa moyo na matendo upate kuyafurahia maisha ya ndoa, achana na mwanamke mzuri sana kwa sura na umbo atakutesa nafsi yako."

Hayo maneno aliniambia miaka 7 iliyopita hapa katikati nilifanikiwa kuwa na wasichana wazuri sana kwa sura na maumbo katika mahusiano lakini wote niliachana nao kutokana na kutokuwa waminifu, sasa nashukuru mungu nimepata msichana wa kawaida ananipenda sana na hivi sasa tupo kwenye utaratibu wa kufunga ndoa, sio siri huyu dada ananipenda sana na ananiheshimu sijawahi kupendwa hivi tangu nizaliwe. Maneno ya shangazi yametimia"mwanangu oa mwanamke mwenye uzuri wa moyo na matendo upate kufurahia maisha ya ndoa".

Nadhani mtakuwa mmejifunza
 
Tuletee basi kadi ya mwaliko wa harusi.......mkono mtupu haulambwi........
 
Tuletee basi kadi ya mwaliko wa harusi.......mkono mtupu haulambwi........

shosti changa kwanza........michango ya harusi siku hizi bila kuchanga 100,000 na kuendelea hupati mwaliko
 
Kwanza uzuri wa mtu upo kwa mtazamaji.
Afu hizi mambo za kuvumilia sijui mimi huwa sizielewagi.
 
Mkuu usituchangishe kuoa...komaa mwenye...onesha uume wako siyo kutuchangisha....
 
shosti changa kwanza........michango ya harusi siku hizi bila kuchanga 100,000 na kuendelea hupati mwaliko

Nitachanga siku mkewe anaenda kujifungua........au shule ya mtoto.......kula utamu sichangi.........
 
mmh mbona kuna wazuri wengi tu wameoleka na wanawaheshimu waume zao..ila pia ukumbe vzur vina gharama waachie wanavyoviweza
 
CV CV CV

mtu yeyote mwenye CV ya kumpa ajira popote atavumiliaje kuajiriwa
kwenye kampuni ambayo mshahara hauna uhakika na mdogo?
why avumilie?
most women kuolewa ni kama kama kutafuta ajira

except mwaj waukweli
 
​Sijui kwa nini mimi siwezi mzungumzia mtu nafsi yake kuwa "huyu mwanamke ananipenda sana"...
 
Wazee wetu walidumu na bibi zetu si kwa sababu ya raha za nyakati hizo bali kwa kusikiliza mashauri ya wazazi wao katika kuchagua wachumba.....bahati nzuri wazee wetu huwa hawatumiii hisia katika kutuchagulia wachumba bali hutazama uhalisia......miaka mingi waliyoishi hapa duniani imewasaidia kuyaona mengi na kujifunza vitu vingi sana ambavyo sisi hatuvijui.....wanapotuambia kuwa mwanamke Fulani hafai au mwanaume Fulani hafai si kwa sababu hawapendi kijana wao apate raha na kipenzi cha moyo wake bali hawataki kijana wao aje kujuta maishani mwake kwani wanajua kuwa hisia huisha kwa kipindi Fulani na baada ya hapo yanafuata maisha halisi ya ndoa.......Bahati mbaya vijana wengi wanashindwa kuyafuata na kusikiliza maoni ya wazee wao kwa sababu ya kutawaliwa na hisia kipindi watafutapo wachumba kiasi cha kusahau mambo ya msingi kwa mke mwema ambayo ni stara na tabia njema....
 
Habari wa kuu,

Nakumbuka kitambo siku moja nilikuwa napiga story na shangazi Yangu kuhusu maswala ya ndoa ndipo akaniuliza kuwa ninapenda kuoa mwanamke wa namna gani, nikamwambia ninapenda mwanamke mzuri sana ndio awe mke wangu,lakini yeye akaniambia namnukuu "wanawake wazuri kwa muonekano wengi wanamatatizo sana.

Wengi huwa hawana malengo na hawawezi kuvumilia shida,ukiwapa ugali wa dona na chips yai lazima watachagua chips yai kwa sababu wanapenda vitamu na siyo vitu vyenye faida,wanawake wazuri wanavitimbi ambavyo wanaume wengi hawawezi kuvumilia, mwanangu oa mwanamke mwenye uzuri wa moyo na matendo upate kuyafurahia maisha ya ndoa, achana na mwanamke mzuri sana kwa sura na umbo atakutesa nafsi yako."

Hayo maneno aliniambia miaka 7 iliyopita hapa katikati nilifanikiwa kuwa na wasichana wazuri sana kwa sura na maumbo katika mahusiano lakini wote niliachana nao kutokana na kutokuwa waminifu, sasa nashukuru mungu nimepata msichana wa kawaida ananipenda sana na hivi sasa tupo kwenye utaratibu wa kufunga ndoa, sio siri huyu dada ananipenda sana na ananiheshimu sijawahi kupendwa hivi tangu nizaliwe. Maneno ya shangazi yametimia"mwanangu oa mwanamke mwenye uzuri wa moyo na matendo upate kufurahia maisha ya ndoa".

Nadhani mtakuwa mmejifunza

punje la harusi linanihusu hapo..
 
Kwanza nikupongeze kwa kupendwa lakini nikupe "usia". Unapopendwa yakupasa na wewe kupenda kwani mapenzi ni Mfano wa ile dhana ya "demand & supply". Kimoja kikizidi basi mushkeli hutokea.
 
Face your fear, wanawake hawaogopwi. Akikuketea ujinga unamuweka pembeni.
 
Back
Top Bottom