Maneno ya ccm uenda yana ukweli... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno ya ccm uenda yana ukweli...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, Jun 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  CCM Imejipanga Vizuri kwa Ushindi

  Hivi karibuni Chama chetu (CCM) kilikamilisha kujipanga kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao, hali ambayo inatuhakikishia kuendelea kufanya vizuri katika uchaguzi ujao hasa ikizingatiwa vyama vya upinzani vimeshindwa kabisa kujipanga kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na kutokuwa na uongozi makini na imara ikiwa ni pamoja na wananchi kukosa kuwa na imani navyo. Kutokana na migogoro isiyokwisha na matatumizi mabaya ya mamilioni ya ruzuku wanayopata kutoka Serikalini.

  CCM imejiandaa vizuri kwa kuendelea kujiweka karibu na uma wa Watanzania jambo ambalo limejidhihirisha hata katika matokeo ya Serikali za mitaa ambapo hakuna hata Chama kimoja cha upinzani kilichoweza kupata walau asilimia 2 huku CCM tukishinda kwa kishindo cha asilimia 93.

  Katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu tayari tumeshanunua magari aina ya Land Cruiser hard top 150 ambazo zimesambazwa katika wilaya zote nchini kurahisisha usafiri kwa viongozi wetu, hivi karibuni tunategemea kununua magari ya kutosha kwa ajili ya misafara ya wagombea wa Urais, Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar, pamoja na magari mengine 26 kwa ajili ya mikoa yote.

  Utaratibu wa uchangiaji fedha kwa ajili ya uchaguzi huo uliozinduliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete umepokelewa vizuri na wananchi hivyo kutarajia kufikia malengo yaliyowekwa.

  Kamati za kufanikisha ushindi zimeshaundwa katika kikao kilichopita cha NEC kilichofanyika Mjini Dar es Salaam tarehe 8/4/2010 kama ifuatavyo:-

  Kamati ya Utekelezaji ambayo ndiyo itakuwa na jukumu la kusimamia shughuli zote za kuleta ushindi Kamati hii itakayoongozwa na Katibu Mkuu Mhe. Yusuf Rajab Makamba (MB.(MNEC) na itajumuisha Wenyeviti wa Kamati nyingine zote zilizoundwa kwa ajili ya kuleta ushindi kama zifuatazo:-

  Kamati ya Mkakati na Uenezi itakayokuywa chini ya Mhe. Abdurahman Omar Kinana, Kamati ya Fedha, Nyenzo na Vifaa vya Kampeni itakayokuwa chini ya Mhe. Zakhia Hamdan Meghji.

  Ni mategemeo yetu kupata ushindi mkubwa zaidi wa kishindo kuliko ule wa mwaka 2005 ambao tulipata asilimia 80.3 kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano, asilimia 53 kwa Urais wa Zanzibar na viti 206 vya Ubunge kati ya viti 232 vilivyopo sasa ambapo kati ya viti 182 vya upande wa Tanzania Bara CCM ina viti 176 na upinzani viti 6, kwa upande wa Zanzibar CCM viti 31 na CUF viti 19 bila ya kujumuisha viti maalum.

  Ni mategemeo yetu kurejesha viti 6 vilivyo chini ya upinzani bara na kushinda viti vingi zaidi Zanzibar baada ya utekelezaji mzuri wa Ilani uliofanywa na Serikali zetu mbili.

  Ni matarajio yetu vyombo vya habari vitaendelea kutoa fursa sawa kwa vyama vyote na kutojishirikisha katika utoaji wa taarifa zisizo na ukweli ambazo zinaweza kuleta machafuko katika nchi bila sababu yo yote ya maana.

  Wenyewe mmeshuhudia jinsi Serikali zetu zilivyoweza kutekeleza ahadi zetu za 2005-2010, mmeshuhudia jinsi tulivyojipanga tayari kwa ushindi wakati wapinzani wetu wakiwa kimya na mikakati sifuri jambo linalotuhakikishia ushindi kwa lazima mwaka huu kama kauli mbiu yetu ya mwaka 2010 USHINDI NI LAZIMA.

  Imetolewa na:-  Richard Hiza Tambwe,


  NAIBU MKUU WA KITENGO CHA PROPAGANDA  Website Rasmi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  .........aah kumbe bi. mdogo,Hiza, nae unajua kuandika vi-point vzr vya kipropaganda!!! you people, you eat politics...you sleep politics...you walk politics....you talk politics...lakini when it comes to stabilize and boost national and public economies=zero!! 1USD=1500.....1kg of sugar=1700TShs. Strategy yenu ya kuwafanya raia wasiijue haki zao kwa kuwanyima elimu ya kawaida na ya uraia ni nzuri kwa muda maana jamaa including taasisi za kidini ziatendelea kuwapa elimu ya uraia na watawang'oa tu madarakani. Mimi nina kadi ya CCM ila being CCM member sio guarantee niwape nyie kura il hali you dont deliver. Our days are countable!!! Baregu....mbayuwayu insults.....Zombe.....Liyumba.....Chenge.....RA.....Bosco Kimera......Edo Lowasa.......IPTL.....EPA.....TRL......Dowans......Radar......Gulfstream Jet.....ATCL.......Net Solution......TICTS....etc=nawachinjia baharini. Mtu aliyekiri kulazimishwa ku-sign EPA na Balali na RA leo ndio Treasurer wetu!!!! Ptuuuu(nimetema mate chin)!!!!! au kwa vile ni mama mkwe wa M/kiti wetu???? Mbona mmemsahau Chenge kama mwanasheria wa kamati kuu ya Kampeni? RA kama chief fund raiser wetu? imekula kwetu..................!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wamesahau kusema wameandaa kilo ngapi za chumvi, sukari, unga, pia wameandaa TShirt, kofia, khanga, nk na vile vile TSh ngapi za kuwahonga walalahoi? Wanajiandaa na ushindi mwingine wa kishindo feki? Kaaazi kweli kweli! Kama wangekuwa wanakubalika magari yote ya nini?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa nini asitaje pia..."Tuna hakika kufanya vizuri kwa sababu Tume ya uchaguzi (NEC) iliteuliwa na Mwenyekiti wa chama chetu, kwa hiyo hakuna wasiwasi katika maamuzi yake hata pale yanapokuwa tete, na kwamba kwa ujumla uwanja wa siasa hauna usawa kutokana na sheria zilizopo zinazopendelea chama chetu kushinda."
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  bajeti ya kila mgombea ubunge was CCM haipungui 200M lakini sheria inasema 40M.... wait and see how they will smash wapinzani!!! tena hao wanaojigawa kama amoeba reproductive process

  THE CURRENT OPPOSITIONS STRATEGIES WONT EVER OUST CCM HATA NYERER AFUFUKE NA KUWA KIONGOZI WA UPINZANI.... THINK ABOUT IT!!
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Au pia... "Tumejiandaa kukupua tena katika taasisi nyingine ya umma kuwawezesha wagombea wetu mamilioni ili ku-wasmash wale wa upinzani. safari hii tutahakikisha hatutafanya kosa tena tugundulike kama vile Kagoda.
   
Loading...