Maneno mazito ya Albert .N. Sanga; usikate tamaa

mkaamweusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2013
Posts
618
Reaction score
828
Ameandika,kuhusu zile nyakati ngumu tunazopitiaga,nguri huyu katika ukuta wake wa facebook!nikaona niibebe kama ilivo niilete jamvini,inaweza wasaidia wanajukwaa!

NAOMBA NIKUTIE MOYO RASMI:-
(PLEASEEEEEE USIKATE TAMAA, CHONDE! CHONDEEEE!)

Katika hali yeyote ngumu unayoweza kujikuta uko nayo katika maisha, ikiwa unamwamini Mungu, wala usipaniki na kuchanganyikiwa. Nyaluke wa SmartMind nina neno kubwa na wewe.

NIKWAMBIE KITU?

Mungu anapendaga kutatua mambo magumu ili ajipatie utukufu mkubwa. Ukiona upo katika magumu huo ndio muda sahihi wa ku-relax kabisaa. Tena ikibidi, jifungie chumbani, jifunge kibwebwe, washa mziki wako mkubwa wa kumsifu Mungu, then dance mpaka mwili ulowe jasho. Muda wote vaa sura ya tabasamu na usijikunyate hata kidogo.

Mwingine ataniambia, "wee Nyaluke unaongea tu, hujajua majaribu ninayopitia". Ohoo, kwani kipi hasa kinachokuaumbua ambacho unahisi Mungu hana "uwezo" wa kukusaidia?

1). Madeni yaliyoshindikana?

Hilo Mungu halimshindi kwa sababu alishawahi kumuokoa mama mmoja mjane ambae wadeni walinadisha kila kitu na bado wakawa wanataka kunadisha hadi watoto wake. (2Wafalme 4:1--). Wewe kama benki wametangaza kuuza nyumba ama mali zako, huna sababu ya kupaniki, bado hujafikia hali aliyofikia huyu mama mjane. Amini tu ya kwamba Mungu anaweza kukuokoa hata sekunde moja kabla ya mnada. Ujue, Mungu anaanziaga pale akili yako inapoishia.

2). Umepoteza kitu? (Ajira, mali, mchumba, n.k)

Kwenye hili eneo ndipo hasa utampenda Mungu. Kuna jamaa walishawahi kupoteza shoka lililotumbukia mtoni. Mungu kupitia kwa Elisha akalifanya lile shoka likaonekana likiwa linaelea juu ya maji (2Wafalme 6). Ukiacha hivyo, Mungu anasema kwa kila ulichopoteza, basi atakurudishia double. (ISAYA 61: 7). Si unaona, enhee? Sasa kwa nini unaendelea kuugua moyoni?

3). Umesubiri ndoa muda mrefu haikuji?

Hofu zingine unajitafutia pasipo sababu. Hivi hujajua kwamba Rebeka alifuatwa na ndoa ikatokea paaaap! (Mwanzo 24). Kipi kinakupanikisha eti kwa sababu umevuka miaka 30+, unachanganyikiwa na kuanza kujirahisi na kujionjesha kwa wanaume? Maadam unamwamini Mungu, hata kama umefikiaha 40+, usipaniki, washenga wa Isaka wako wako njiani wanakuja. Usianze kuzurura, kujigongesha kwa akina Said ukapishana na washenga.

4). Umetafuta mtoto/watoto muda mrefu bila mafanikio?

Hongera sana. Tena naomba unitumie namba yako kwa WhatsApp text (0688726442) kwa sababu wewe sio wa kawaida kabisa. Bora nijisogeze kwako mapema ili nianze kupokea neema uliyoibeba. Unajua kwa nini? Nimefuatilia toka Mwanzo hadi Ufunuo katika Biblia, nimegundua kwamba wanawake wooote waliochelewa kuzaa, ama ambao kubeba mimba kwao kulikuwa kiutata, waliwazaa watu wakuu sana(great men of God).

Huamini? Kamuangalie Sara alimzaa Isaka na unaujua ukuu wa Isaka! Hanna alimzaa Nabii Samweli. Mariam ambae nusura mimba imdharirishe alimzaa Yesu Kristo. Rebeca alipobeba mimba, ilimsumbua sana lakini akaja kuzaa mataifa makubwa. Nikwambie kitu? Kuchelewa kwako kubeba mimba sio bure, hizo mimba zinazoharibika sio bure, kwa sababu kuna mtoto/watoto wakuu sana wanaotakiwa kubebwa katika tumbo lako. Wako njiani, tulia, wala usiwe na wasiwasi.

Ukiona hadi mie nakuomba namba yako ujue nimeshaona wewe ni mama wa watu wakuu, ni bora tujipendekezage kwako mapeeeeema. Waambie mawifi wanaokuzodoa, wataarifu wakwe wanaokuona mjaza choo tu, wajulishe marafiki wanaokuhurumia kisa umechelewa kupata watoto:- ya kwamba Isaka wako anakuja, ya kwamba twin wako (Yakobo ma Esau) wanakuja, ya kwamba Samweli wako yuko njiani!

5). Umekosa ajira?

Wewe ndio naomba usiwaze kabisa. Yesu Kristo, ananifurahishaga sana mifano yake. Kuna jamaa katika Mathayo 20:1-16, walikuwa wamekaa mkao wa ajira lakini ajira zikawa hazipo. Kati yao kuna ambao waliajiriwa mida ya lala salama (kwa kuchelewa sana), lakini unaambiwa wakanufaika sawa na wale waliowahi kuajiriwa. Usipaniki kuona kwamba uliomaliza nao wameshaajiriwa na wewe bado unahanyahanya mitaani, kwa sababu Mungu anaweza kukupiga bonge la suprise ya ajira, huo mshahara na marupurupu hadi utasahau ikiwa umewahi kuishi bila ajira maishani mwako. Nipe tano basi!

6). Ndoa yako iko ICU inapumulia mashine?

Kumsema mwenzi wako kwa watu na mabaya yake sio suluhu! Kupeleka malalamiko kwa washenga ni utoto! Kushtakiana kwa paroko ama kwa pasta haiwezi kusaidia sana! Kususa vyakula vya jikoni na vya kitandani sio dawa! Kutafuta faraja nje ya ndoa ni kujiongezea msala! Kukata tamaa ni kujimaliza! Kuendelea kulalamika inakudharirisha! Kutafuta talaka sio utatuzi wa wa tatizo!

Hujajua kwamba yupo Yesu Kristo mtuliza bahari? (Marko 4:35-41). Kwa kuwa Yesu ni yeye yule jana leo na milele, anaweza kuiokoa ndoa yako sasa hata kama umeshaikatia tamaa. Ukishamuamsha ndani yako, mawimbi yanayoipiga ndoa yako ni lazima yatatulia fasta.

HEBU NIAMBIE..

Je, bado umekata tamaa? Ahaa, bwaaaaaaaana! Basi piga selfie unitumie kwa WhatsApp nijue kwamba umeinuka upya. Usiniangushe! Sawa enhee?
 
Yaani ukae geto uanze kumcheza Mungu ndomboro ya solo, achen upuuzi nyie walokole

Mnaikurupukia vibaya bible

Hata wayahudi toka wanazaliwa had kesho hawajawahi kurukaruka na kucheza ndombolo kwenye ibada.
 
Mkuu umenena vyema sana,,,nikupe like kwanza,,,,hakuna namna nyingine zaidi ya kumwomba Mungu kwa kila jambo...
 
Yan nimesoma ujumbe umeniingia mpaka kwenye damu na kujihic mwepec.. Mungu hukupa majaribu mazito bila kujia amekuandalia furaha ya kudumu milele na milele kwenye maisha yako.. aiseh ubarikiwe sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom