Maneno maarufu secondary za bweni

ijoz

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
731
710
Wakuu,amani kwenu...
Ningependa tukumbushane maneno maarufu yaliyokuwa yanatumika shule za secondary hasa boarding.
Mi nakumbuka maneno kama:
1.Njuka,kitimoto,mkia,nyoya=form one
2.Kufufuka=kuamka usiku kusoma.
3.Kuwa Mongwe= Kuishiwa pesa.
Sifongo=Uji usiokuwa na sukari.
4.Kuchoma=Kuingia bwenini ukiwa umevaa viatu/kandambili
5.Top layer=watoto waliokuwa wanakuja kuchukua mabaki ya vyakula.
6.Nelkon,Abbot,Lambert,Lodgers,UP,BS,Mkate,Jacky Fernandes,Nalndel Kumar=miongoni mwa vitabu maarufu vya sayansi.
Mnaweza kuendeleza list...
 
Boy = Mwanafunzi mnaetokea mkoa mmoja
Ng'ande = Kande
Kitei = Wali
Sumu = Uji wa dona
Vitufti/ Mapisi = Mjumuiko wa vitafunwa kama mandazi, bagia, half cakes....
Mtego = mwanamke mrembo, tv au filamu.
Chui = Ugali wa dona
 
Back
Top Bottom