MANENO KUNTU YA Mwalimu Julius K. Nyerere

MANENO KUNTU YA Mwalimu Julius K. Nyerere

Joined
Mar 3, 2013
Posts
30
Reaction score
4
Wakati mwingine watu tukizungumza shida za jumuiya, yaani siyo shida za mtu mmoja mmoja. Ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba kwa kweli hizo ni shida za jumuiya, siyo uzushi wetu wenyewe kwa faida yetu wenyewe. Mambo tunayozungumza katika mikutano yetu hayana budi yatokane na watu wenyewe huko vijijini kwao. Tukiisha kuyazungumza na kuona jinsi ya kuondoa shida hizo hatuna budi turudi tena kwa watu wenyewe kule vijijini tuzungumze upya shida hizo na jinsi tunavyofikiri shida hizo zaweza kuondolewa kama mawazo yetu na mawazo ya watu wenyewe yatakubaliana vema
~ Mwalimu Julius K. Nyerere katika kitabu chake cha TANU NA RAIA.

Unaweza Kukisoma hapa
▶▶ www.vitabutanzania.com/tanu.php

Ukisoma kitabu hiki mambo mengi yaliyo kuwa yanapingwa na Mwalimu Julius K. Nyerere Sasa ndo yanatokea


 
Maandiko ya Mwalimu ni ya kipekee. Watawala na watawaliwa wengi kwa sasa hawayataki kwa sababu yanawaumbua. Mimi maandiko ya Mwalimu ndiyo dira yangu ya maendeleo. Ukiyasoma maneno ya Mwalimu lazima utakuwa mtu muungwana na mpenda binadamu wenzako na pia mazingira yanayokuzunguka.
 
Back
Top Bottom