Manchester United wang'olewa na Sevilla katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

chriss cr Tz

Member
Jun 20, 2017
24
15
7cbdde81-ea45-4832-990f-787551273496.jpeg
33621450-7534-4bff-b611-5358eeb0c7d1.jpeg
f5dc3d48-ae68-41b6-87c0-cf85d9bdbdbd.jpeg



ULAYA: Klabu za Soka za Sevilla ya Uhispania na AS Roma ya Italia jana usiku zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bigwa barani humo

Sevilla wamefuzu baada ya kuitandika Manchester Utd goli 2-1 katika mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Old Traford baada kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uhispania

AS Roma jana akiwa katika uwanja wa nyumbani alipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mechi ya marudiano . Mechi ya kwanza Shakhtar alipata ushindi wa goli 2-1. Roma anafuzu kwa sheria ya goli la ugenini

Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo Barcelona anakutana na Chelsea katika uwanja wa Camp Nou, huku Besiktas anakutana na Bayern Munich
 
Hapana mkuu si tupo vzr mbna
Vizuri wapi kamanda!!

Mechi ambazo zinasadikika kama big match Man United inajihami sana(kupaki basi) sasa naona mpaka timu za kawaida tabia imekomaa kama ngozi ya mamba.

Mimi mwenyewe Shabiki wa Man united damu damu tangu mwaka 2001.
 
Vizuri wapi kamanda!!

Mechi ambazo zinasadikika kama big match Man United inajihami sana(kupaki basi) sasa naona mpaka timu za kawaida tabia imekomaa kama ngozi ya mamba.

Mimi mwenyewe Shabiki wa Man united damu damu tangu mwaka 2001.
Kwamba tuseme xhida iko wapi
 
Back
Top Bottom