C E O wa Manara Tv na Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Haji Manara amefunguka kuwa miongoni mwa wanawake majasiri Duniani ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa Habari Manara amesema ni mwanamke gani anaweza kuvumilia matusi kila siku na akanyamanza kimya.
"Kuna muda Rais Samia anatukanwa na watu aliyowasaidia kuwatoa magerezani lakini hajawahi kuwajibu wala kuwafungulia mashitaka" Alisema Haji Manara
Acha chuki Binafsi.
Wangapi wanamsifia huyo Mama na hawapo hata kwenye nafasi ya kugombea udiwani?
Kwani Haji akitaka kuwa Mbunge wa Ilala Kuna tatizo Gani?
Gerezani wameenda wangapi na wametoka na Maisha yanaendelea!
Wananchi wataojisahau wakampa Jimbo Manara haki ya Mungu nawaonea huruma maana waliharibu kumkumbusha ahadi zake za kampeni itakuwa ni kuchambwa tu mpaka wakome
Sasahv kule mjengoni hakuna maajabu yoyote so hata mtoto mdogo anaweza kuingia tuu. Bunge lililoweka maana ya bunge ni lile la kipindi kile cha Marehemu mzee Sitta.