Manara akwepa lawama

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara amedai anaonewa kwa kupewa lawama zisizomuhusu baada ya kile kinachoaminiwa kuwa naye ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika makubaliano na mdhamini wao mpyaSportpesa


Manara amesema hayo siku moja baada ya mfanyabiashara , Mohammed Dewji kutoa kauli ya kusikitishwa na uongozi wa klabu ya Simba kusaini mkataba wa udhamini wa muda mrefu na Sportpesa bila ya kumshirikisha yeye, ambaye aliweka nguvu zake nyingi katika klabu hiyo.


“Uongozi wowote ni Jalala ila uongozi wa mpira ni Dampo, ‘sometimes’ napokea lawama zisizonihusu, ‘but’ nina moyo wa chuma na nina uzoefu wa kuwa kiongozi katika tasnia tofauti, kazi yangu ni kuhabarisha umma, mengine ni kunionea”ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Aidha, Manara amesema kuwa hakuhusika kwa chochote katika mchakato huo lakini kwakuwa yeye nikiongozi amesema yuko tayari kupokea lawama zote zinazoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama

70d39041f85686c45bb632053bd22574.jpg
 
Lakini afafhali katika hilo deal na tigopesa sijui watapata name nauli ya kwenda FIFA, maana nyepesi nilizopata ile $15,000 walizosema hawajapata bado.
 
Back
Top Bottom