Manabii na pesa

Manabii na pesa

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Nimekuwa nikifuatilia mahubiri ya Manabii lakini kila wakihubiri wanatanguliza pesa ya kutoa sadaka au ujenzi wa Makanisa yao. Mfano pale Mwanza mwezi mmoja uliopita kuna Mhubiri alikuwa na mahubiri uwanja wa Kirumba, sharti alilolitoa ni kuwa ili uombewe kama una matatizo lazima utoe laki moja. Sisi wote tunasoma Biblia wapi pameandikwa ili upate huduma ya maombi sharti utoe pesa?. Ninyi Manabii tuogopeni Mungu tuache kutanguliza pesa mbele.
 
joseverest umekuwa mzito sanaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

sent from my samsung galaxy s8+ using jamiiforums mobile app
 
Ni kweli mkuu siku hizi ni biashara

hakuna nabii ulimwengu huu wa sasa

Do Something 2day That Your Future Will Thank You 4
 
Nimekuwa nikifuatilia mahubiri ya Manabii lakini kila wakihubiri wanatanguliza pesa ya kutoa sadaka au ujenzi wa Makanisa yao. Mfano pale Mwanza mwezi mmoja uliopita kuna Mhubiri alikuwa na mahubiri uwanja wa Kirumba, sharti alilolitoa ni kuwa ili uombewe kama una matatizo lazima utoe laki moja. Sisi wote tunasoma Biblia wapi pameandikwa ili upate huduma ya maombi sharti utoe pesa?. Ninyi Manabii tuogopeni Mungu tuache kutanguliza pesa mbele.
Mambo ya kaisali muachie kaisali kwenye na yamungu tufate Mimi na wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanachokifanya hao jamaa nimekiingiza kwenye mila na desturi mpya potofu.
Yesu anasema "Nitakapoinuliwa juu, nitawavuta wengi kwangu"
Wao wanainua Juu MPESA,TIGOPESA,AIRTELMONEY, ACCount za benki na visosi vya Sadaka kwa jina la yesu.

Ngoja watu waibiwe maana walikataa wenyewe Kuwekeza kwenye kujisomea neno na kuwekeza kwenye akili za hawa wapambanaji.
 
Nimekuwa nikifuatilia mahubiri ya Manabii lakini kila wakihubiri wanatanguliza pesa ya kutoa sadaka au ujenzi wa Makanisa yao. Mfano pale Mwanza mwezi mmoja uliopita kuna Mhubiri alikuwa na mahubiri uwanja wa Kirumba, sharti alilolitoa ni kuwa ili uombewe kama una matatizo lazima utoe laki moja. Sisi wote tunasoma Biblia wapi pameandikwa ili upate huduma ya maombi sharti utoe pesa?. Ninyi Manabii tuogopeni Mungu tuache kutanguliza pesa mbele.
MKUU dini ni moja tu hapa duniani,,,ISLAM ,,,,,mti wenye matunda mazuri ndio unapigwa mawe siku zote,, katika uislamu hakuna mambo ya kutaperiana pesa wala upuuzi mwingine, na ukileta utaperi watu SIO wajinga lazima wakuambie kweli,,

Hayo mambo ya ugaidi ni wakristo ndio wanapanga matukio yote ktk Nchi zote duniani wakishirikiana na watu wenye majina ya kiislamu fake,,

Chief waislamu ni wavumilivu mnoo, , na wakichoka uvumilivu huwa wameruhusiwa kulipiza ila kusamehe Ni bora wameambiwa na mola wao,,, nyinyi wakristo HAMNA uvumilivu boss,,,ukitaka kujua nyi hamna uvumilivu, ,,shuhudia hapa me ntakavyoyaoga matusi ya Wakristo mkuu
 
Wale ni matapeli sio viongozi wa dini wanafki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yamkini nyakati za mwisho zikifika hata wateule watapotoshwa, ni kipindi kigumu sana hiki katika unabii '' wengi watakuja kwa jina lake wakifanya MIUJIZA, lakini iweni makini '' kizazi hiki kina husudu miujiza na hii itakuwa chanzo cha hata wateule kukengeuka, fuateni NENO, na sio MIUJIZA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga ndio waliwao! Siku hizi shida zako mtaji hasa upande wa maombezi

Sent using Jamii Forums mobile app
48 Laws of power.

Law 27.

People have an overwhelming desire to believe in something. Become the focal point of such desire by offering them a cause, a new faith to follow. Keep your words vague but full of promise; emphasize enthusiasm over rationality and clear thinking. Give your new disciples rituals to perform, ask them to make sacrifices on your behalf. In the absence of organized religion and grand causes, your new belief system will bring you untold power.......

Watumishi hucheza na hiiiii
 
MKUU dini ni moja tu hapa duniani,,,ISLAM ,,,,,mti wenye matunda mazuri ndio unapigwa mawe siku zote,, katika uislamu hakuna mambo ya kutaperiana pesa wala upuuzi mwingine, na ukileta utaperi watu SIO wajinga lazima wakuambie kweli,,

Hayo mambo ya ugaidi ni wakristo ndio wanapanga matukio yote ktk Nchi zote duniani wakishirikiana na watu wenye majina ya kiislamu fake,,

Chief waislamu ni wavumilivu mnoo, , na wakichoka uvumilivu huwa wameruhusiwa kulipiza ila kusamehe Ni bora wameambiwa na mola wao,,, nyinyi wakristo HAMNA uvumilivu boss,,,ukitaka kujua nyi hamna uvumilivu, ,,shuhudia hapa me ntakavyoyaoga matusi ya Wakristo mkuu
Unaposema dini ni moja tu ndipo unapokosea
 
Ndugu zanguni....wala tusipate taabu, yote haya yalitabiriwa zamani......ni yanatimilika tuu kwa sasa. Hakuna haja ya kutukana wala kudhihaki dini (ukristo), haya yanatokea kutimiliza unabii.

Mathayo 7:15-20

" 15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua"
 
Back
Top Bottom