Mamlaka zinawaza nini kusaidia Wanafunzi wanaoshindwa kuchangiwa gharama za lishe shuleni?

Mamlaka zinawaza nini kusaidia Wanafunzi wanaoshindwa kuchangiwa gharama za lishe shuleni?

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
427
Reaction score
666
Tutakumbuka Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha huduma muhimu ya chakula na lishe inapatikana kwa Wanafunzi wa elimu ya msingi mashuleni.

Utaratibu huo unatekelezwa kutokana na Mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa Elimumsingi, ambapo wazazi na wadau wanatakiwa kuchangia vitu mbalimbali kuwezesha huduma hizo, mfano Chakula, Mafuta, Sukari, Chumvi pamoja na mahitaji mengine ya kupikia sambamba kuwezesha Malipo ya Wapishi.

Shule nyingi zimekuwa zikitekeleza mwongozo huo tokea ulipotangazwa, ambapo Uongozi wa Shule umekuwa ukiweka utaratibu wa namna huduma hizo zinavyoweza kupatikana.

Udadisi wa kizalendo uliofanyika katika Shule mbalimbali zilizopo Jijini Dar es Salaam, unabaini wazi utaratibu ambao unatumika katika Shule nyingi ni wazazi kutakiwa kuchangia gharama za wastani wa Shilingi 500 hadi 1500 kila siku ya masomo kwa kila Mwanafunzi.

Gharama hizo zimekuwa zikitumika kuwapatia mahitaji ya huduma ya chakula shuleni ikiwemo uji na chakula cha mchana.

Hata hivyo licha ya baadhi ya Wazazi kuwa na mwitikio wa kuchanga michango hiyo lakini baadhi ya Wanafunzi wamekuwa wakiikosa huduma hiyo muhimu kutokana na Wazazi wao kushindwa kumudu gharama hizo kwa kila siku.

Na licha ya baadhi ya watoto kunufaika lakini suala hili limekuwa likipelekea mazingira ya unyanyapaa kwa watoto ambao wanakosa huduma hizo kutokana na kwamba wazazi wao wameshindwa kuchangia michango.

Kwenye Shule nyingi ikifika muda wa kupata huduma hizo muhimu baadhi ya Wanafunzi wanalazimika kukaa kando ili waliolipia gharama waweze kupatiwa huduma chakula.

Kutokana na mazingira hayo udadisi wa kizalendo unabaini kuwa yanapelekea watoto hao wanaowekwa kando kuwa katika mazingira ya kunyanyapaliwa au kijinyanyapaa jambo ambalo uenda likawa linaweka katika mazingira ya kutofanya vizuri katika masomo yao.

Licha ya kuwepo kwa wazazi wanaoshindwa kuchangia kutokana na kukosa uelewa wa kutosha au kutolizingatia suala hilo lakini kuna kundi kubwa la wazazi ambao ushindwa kuchangia gharama hizo kutokana na kuwa na kipato duni ambacho kinawafanya washindwe kumudu gharama.

Kuna baadhi wa Wazazi au walezi ambao kipato chao ni duni lakini wanao Watoto watatu ambapo kila siku kila Mtoto anatakiwa kwenda na Shilingi 1000 jambo ambalo linakuwa gumu kwao.

Wito wangu kwa mamlaka napendekeza Serikali itenge ruzuku ambayo itakuwa inaenda kwenye Shule za msingi kwa ajili ya kuchangia huduma za chakula hususani kwa Watoto ambao kupitia uongozi wa Shule utabaini hawawezi kumudu gharama husika.

Lakini Serikali inaweza kuandaa mpango maalum shirikishi wa Kitaifa unaowashirikisha wadau kuchangia kwenye mfuko maalumu unaoweza kusaidia watoto hao kuwa katika mazingira rafiki ya kupata haki ya elimu kwa usawa.

Ni muhimu kama Taifa tumeamua kulitekeleza suala hilo tukalipa mazingatio bila kuacha watoto nyuma, suala hili tunaliweza hata kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima Serikalini.


Pia soma:
~
Wazazi wa wanafunzi Shule ya Sekondari BUJUNANGOMA, tumechoka na Michango, Rushwa, Utumikishwaji wa watoto wetu shuleni
~ Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda apiga marufuku Shule kuzuia Wanafunzi ambao hawajalipa fedha za michango
 
Mamlaka zinawaza matumbo yao tu sababu watoto wao hawana shida ya lishe kwenye shule zao zaidi mamlaka zinafaidika na uduni wa lishe bora kwa watoto wa akina yahe ili watawaliwe kirahisi na wawe watumwa watiifu.
 
Back
Top Bottom