Mamlaka ya Rais kumteua mkuu wa chuo kikuu

wamisako

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
917
871
Rais MAGUFULI kamteua mh jakaya mrisho kikwete kua mkuu wa chuo KIKUU cha dar es salaam, maswali nayo jiuliza nikweri Rais anamamlaka ya kumteua mkuu wa chuo kikuu katika vyuo vya serikali? Pili kwanini vyuo vikuu vya serikali wakuu wa vyuo ni marais wastaafu? Tatu before kuteuliwa kwa jakaya kikwete nani alikua mkuu wa chuo cha University of dar es salaam?? Nne vipi kuhusu kigezo cha elimu kinazingatiwa au hakizingatiwi katika kumteua mkuu wa chuo kikuu, mfano mtu mwenye masters awaongoze maprofesa na ma dokta??
 
Ngoja waje ila najua mkuu wa chuo hicho alikufa mwaka juzii.
 
Rais MAGUFULI kamteua mh jakaya mrisho kikwete kua mkuu wa chuo KIKUU cha dar es salaam, maswali nayo jiuliza nikweri Rais anamamlaka ya kumteua mkuu wa chuo kikuu katika vyuo vya serikali? Pili kwanini vyuo vikuu vya serikali wakuu wa vyuo ni marais wastaafu? Tatu before kuteuliwa kwa jakaya kikwete nani alikua mkuu wa chuo cha University of dar es salaam?? Nne vipi kuhusu kigezo cha elimu kinazingatiwa au hakizingatiwi katika kumteua mkuu wa chuo kikuu, mfano mtu mwenye masters awaongoze maprofesa na ma dokta??
Cheo cha chancellor ni ceremonial position....Ni cheo cha heshima lakini haki affect directly utendaji wa chuo moja kwa moja...mtendaji mkuu ni Vice chancellor ambaye ni Prof Mkandara.

Nahisi vigezo vinavotumikaga ni heshima na mchango wa mtu husika ktk sekta mbalimbali ni kama uprofesa wa heshima aliopewa nchini China na pia degree nyingi za heshima anazopewa....

Na pia Influence yake ktk jumuiya za kimataifa ...mfano Ban ki moon alimteua kuongoza jopo la wasomi ktk tafiti ya afya na hata aliongoza jopo la wasomi ktk kampeni za malaria afrika so influence yake....ni moja ya chachu ya uteuzi wake..

Na hata heshima anazopewa na vyombo vya kimataifa kama African statesman of the year....So ni suala la heshima na wala halihusiani moja kwa moja na utendaji wa chuo

Na pia ameteuliwa baada ya aliyekuwa Chancellor wa chuo Balozi Nicholaus Kuhanga kufariki....na pia uone Balozi kuhanga ni kutokana na cheo chake na sio usomi sana....
 
mbona hata mbeya university mkuu wa chuo ni mark mwandosya na makamu wake ni msambichaka
 
watu wavivu sana kutafuta maarifa kwa kujisomea kila kitu nikuuliza JF,
 
Ambassador (rt) Kuhanga alikuwa Ag. Chancellor baada ya kufariki Balozi Kazaura (RIP). Kuhusu uteuzi wa Chancellor ni dhana iliyoanza wakati wa Nyerere ambapo yeye ndiye alikuwa mkuu wa Chuo. Baadaye akagatua madaraka kwa kuweka msaidizi. Hivyo ndivyo walivyoteuliwa kina Msekwa, Kuhanga mwenyewe, Bomani, etc.

Kiujumla ile ni nafasi ya kisiasa tu na haina uhusiano wa kiutendaji wa kila siku wa chuo. VC ndiye mtendaji mkuu wa Chuo Kikuu (nikitumia case study ya UDSM).

Details zingine mleta thread jishughulishe kutafuta.
 
Back
Top Bottom