Mamlaka ya rais ktk mjadala wa katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya rais ktk mjadala wa katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by politiki, Nov 11, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wale wote wanaotaka kumpa Rais nguvu ya ku control swala hili la katiba wameweka SIASA mbele badala ya maslahi ya nchi kwani Urais ni moja kati ya taasisi ambayo mamlaka yake yanajadiliwa na swala zima la katiba kwahiyo mhusika hawezi kupewa control ya mjadala unaojadili mamlaka yake yanayomuhusu. hii ni sawa na Rais kuongoza kikao kinachojadili mshahara wake haiwezekani na hapa kitachojadiliwa ni hoja ya mamlaka ya Rais kwahiyo kama Rais hawezi kutoa muongozo wa namna ya kujadili mamlaka yake?? wananchi pekee yao ndio inabidi wapewe mamlaka ya kuamua nchi iongozwe vipi bila kuingiliwa na mtu yeyote au taasisi yeyote. tusipoangalia swala hili la katiba litatuingiza matatizoni kwa sababu ya viongozi wachache wanaojaribu kulinda maslahi yao ya kisiasa badala ya kuweka maslahi ya taifa na wana harakati tuwe tayari kupambana ili kuakikisha wanasiasa hawa maslahi hawaaribu zoezi hili zima.

  dalili mbaya zimeanza kusikika kwa waziri wa katiba Kombani akiiambia kamati ya bunge kuwa imwamini tu RAIS kuwa na mamlaka yote kuhusu swala la katiba kwani ameaminiwa na wananchi walio wengi that is boo shit, my questions to kombani are what about trusting wananchi to decide their own fate ?? do you think Mr.president cares much about wananchi's interest than themselves ?? itafikia mahala watanzania itabidi tufuate njia waliopita ndugu zetu wa Kenya kama kweli tunataka katiba mpya ya ukweli nchi hii.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,307
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mamlaka ya rais yagawa Kamati ya Katiba [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 11 November 2011 09:30 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Neville Meena, Dodoma
  Mwananchi

  KAMATI ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala imeshindwa kufikia mwafaka kuhusu muswada wa Sheria ya Mapitio na Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni Jumatatu ijayo.

  Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo, jana zinasema wajumbe hao bado wamegawanyika kuhusu suala la sheria inayokusudiwa kutungwa kumpa Rais mamlaka makubwa katika mchakato huo wa kupatikana kwa katiba mpya.

  Habari hizo zinaeleza kwamba wanabishania wanachodai kuwa ni muswada huo kumpa Rais madaraka makubwa ambayo ni pamoja na kuteua wajumbe wa tume ya Kukusanya Maoni, sekretarieti ya Tume hiyo na wabunge 116 kuingia katika Bunge la Katiba.

  “Kwa hali hii Katiba inaweza kuwa ni mali ya Rais, maana hata wajumbe wa sekretarieti anatakiwa kuteua yeye! Hii ni 'too much' (imezidi). Kwa maana hiyo, mchakato mzima unashikwa na Rais mwenyewe,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

  Taarifa zaidi zinasema kutokana na mvutano huo, suala hilo sasa limechukua mtizamo wa itikadi za vyama, na kwamba wajumbe ambao ni wabunge wa CCM katika kamati hiyo wameanza kulegeza msimamo na kukubaliana na mapendekezo ya Serikali, huku wabunge wa upinzani wakitaka kufanywa kwa marekebisho.

  Kwa mujibu wa habari hizo, wajumbe hasa wale kutoka upinzani wanataka madaraka ya Rais yapunguzwe kwa kuipa Tume ya Kukusanya Maoni kutoka kwa wananchi ndiyo ipewe mamlaka ya kuteua sekretarieti yake badala ya suala hilo kufanywa pia na Rais.

  Juzi, Waziri wa Katiba na Sheria, Celine Kombani aliliambia Mwananchi kuwa tatizo la wanaodai kuwa Rais ana madaraka makubwa hawatoi mapendekezo mbadala na jinsi ya kurekebisha pendekezo hilo.

  “Sasa Rais ndiye aliyepo, kwa nini hawataki kumwamini wakati alipigiwa kura na wananchi wengi? Lakini, basi waseme wao wanatakaje,” alisema Kombani.

  Mmoja wa wajumbe alisema: “Mahali tunapofika, ni kama kila mmoja ataondoka na msimamo wake kwenda nao bungeni. Hata leo, mbele ya Waziri (Kombani) tumeshindwa kufikia mwafaka, sasa hiyo siyo dalili njema."

  Hali hiyo ya kutoafikiana miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo inatoa ahueni kwa Serikali kuweza kupitisha mapendekezo yake bila kupata upinzani mkubwa kutoka kwa kamati hiyo kama ilivyokuwa awali.

  Vikao vya Kamati hiyo vimekuwa vikivuta wabunge wengi hata ambao si wajumbe wake, ili kufuatilia kinachoendelea kwenye meza ya majadiliano baina ya wajumbe husika kwa upande mmoja, kamati na Serikali kwa upande mwingine.

  Kutokana na unyeti wa suala la katiba, Spika wa Bunge Anne Makinda aliongeza wajumbe watano katika Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili kupanua wigo wa mjadala wa suala hilo.

  Makinda aliliambia Mwananchi mwanzoni mwa wiki hii kuwa wabunge hao watano wanaruhusiwa kupiga kura kwenye uamuzi. “Kikanuni hawa niliowateua mimi wanaruhusiwa kupiga kura na nimefanya hivyo kutokana na unyeti wa suala lenyewe,” alisema Makinda.

  Wajumbe hao ni Mwanasheria Mkuu wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed pamoja na Deogratius Ntukamazina ambaye ni Mbunge wa Ngara (CCM).

  Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, sasa utasomwa bungeni kwa mara ya pili na umetengewa siku tatu kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kupitishwa na Bunge.

  Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Aprili 5, mwaka huu, lakini, ukarejeshwa Serikalini ili kufanyiwa marekebisho kadhaa na kuandikwa kwa Kiswahili kabla ya kurejeshwa tena Bungeni.

  Kutokana na hali hiyo Serikali ilipata upinzani mkali kutoka kwa wabunge na wanaharakati ambao walidai kwamba muswada huo ulipaswa usomwe kwa mara ya kwanza kutokana na kufanyiwa marekebisho makubwa tofauti na ule wa awali.

  Hata hivyo Kombani alisema juzi kuwa: “Muswada huu uliposomwa kwa mara ya kwanza haukuondolewa, bali ulipelekwa kwa umma ili ukajadiliwe”.

  “Mabadiliko mengi yanayolalamikiwa yalitokana na hoja za wananchi, hii ni ishara kwamba tulizingatia hizo hoja, sasa kwa mujibu wa taratibu za miswada ni kwamba utasomwa kwa mara ya pili, kama mnavyoona kwenye ratiba,” alisema Kombani.

  Mkurugenzi wa Huduma za Bunge, John Joel aliliambia Mwananchi kuwa kwa mujibu wa taratibu, muswada huo hauwezi kutangazwa tena katika Gazeti la Serikali wakati ulishatangazwa Machi mwaka huu.

  Ratiba ya Mkutano wa Tano wa Bunge inaonyesha kuwa Muswada huo utasomwa kwa mara ya pili Jumatatu, Novemba 14 mwaka huu na kuendelea kujadiliwa na Jumanne, Novemba 15 na Jumatano Novemba 16 mwaka huu.

  Hatua ya muswada huo kupangwa kusomwa kwa mara ya pili, inatafsiriwa kuwa ni “ushindi” kwa Serikali dhidi ya waliokuwa wakipinga hatua hiyo kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni wananchi kupewa muda zaidi kwa ajili ya kuujadili.

  Mjadala wa muswada huo utatanguliwa na semina kwa wabunge wote itakayofanyika kesho Jumamosi hatua inayotafsiriwa kuwa ni kujaribu kupunguza hoja ambazo zinaweza kujitokeza na pengine kuukwamisha.

  Baadhi ya wanaharakati wanaopinga muswada huo kusomwa kwa mara ya pili ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Jukwaa la Katiba ambao wameenda mbali na kudai kuwa Waziri Kombani, amechakachua muswada huo.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa nini hakuna mbunge toka CHADEMA? nachoona ni triplicates toka magamba pamoja na wenza wao..Kweli nimeamini huyo spika mwanamama ni joker!!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia hao wabunge 5 aliowaongeza Makinda hakuna hata mmoja toka kwenye CHADEMA! Ameptiwa? Ni makusudi kawakwepa CHADEMA ndio chama cha upinzani bungeni chenye wabunge wengi. Na kama sio usanii wa Makinda na ccm wenzanke kubadili kanuni CHADEMA ndio chama kikuu cha Upinzani bungeni? Majina haya hapa:

  1. Mwanasheria Mkuu wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge,
  2. Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila,
  3. Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka,
  4. Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed
  5. Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratius Ntukamazina


  Kama alivyosema mwenyewe Makinda hawa wajumbe 5 aliowaongeza wataruhusiwa kupiga kura? Kwa maana hiyo basi Makinda anafanya ujanja ili wapiga kura wa YES wawe wengi maana CUF ni swa na CCM na Kafulila anaweza kubadilika. Shida ninayoona hapa ni kujiamini mno kwa hawa wana-ccm kuwa bado wana mbinu za kuchezea watu akili! Na akilini mwao wanafikiri CHADEMA ni wabunge na watu wengine wachache. Hawaelewi kabisa kuwa CHADEMA ndio wanaongoza hii nchi kwa sasa sababu CHADEMA ni umma wa watanzania uliochoshwa na siasa za kiimla zilizojaa unyonyaji.

  Muswada wa sasa bado una matatizo ya msingi na hautakubalika kwa wanachi piga ua kama hawakufanya marekebisho. Huu usanii wanaofanya Dodoma utaingiza nchi kwenye mgogoro. Muswada una matatizo, Rais ana mamlaka makubwa mno.
   
 5. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kama alivyosema waziri, changia: Unataka uweje?
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Anheuser, Si kweli hata kidogo kuwa watu hawajachangia muswada uweje. Kwa muda mrefu sasa watu mbalimbali (individually) na organisations wametoa maoni (specific suggestion) lakini Waziri Celina Kombani na mabosi wake wameamua makusudi mazima kupotosha kuwa 'watu wanalalamika lakini hawatosi suggestion! Ni mara ngapi watu wamesema Rais amepewa madaraka kupita kiasi? Kwa nini Celina Kombani na genge lake wanang'ang'ania hiki kifungu? Hii ni katiba wa wanachi wa Tanzania au ni ya Rais? Ukishakosea kwenye hili la usitegemee kupata product inayokubalika kwa unawaongoza (wananchi). Ukiwa na tume inayo-report kwa Rais basi tegemea utendaji wa kikada kama ambayo tumekuwa tunashudia wakuu wa mikoa, wilaya n.k. Watafanya kazi za bosi na sio wananchi. Kumbe tunakata katiba ya wananchi na sio ya Rais.

  Nafasi ya Zanzibar/muundo wa muungano bado ni kitendawili. Kwa muda mrefu watu wa Zanzibar wametaka kura ya maoni juu ya ama wanataka kubaki kwenye muungano na kama wanataka uwe ni muungano wa aina gani. Hivyo hivyo nilidhani upande wa bara watu wangepewa nafasi ya kujadili aina ya muungano wanaotaka. Kwa hali ilivyo sasa ni kwamba watasoma huu muswada week ijayo lakini kama kawaida kiburi chao kitawaletea matatizo makubwa kuna 'GAP' kubwa sana juu ya nini wananchi wanataka na kile wanachofanya hawa wanasiasa.

  Binafsi nadhani makosa yalianza mbali. Celina Kombani anaweza akawa na uwezo mzuri kwenye mambo mengi lakini niseme kwa nia njema sidhani kama huyu mama ana uwezo wa kusimamia wizara hii wakati huu wa kuandika katiba mpya. And so far amedhihirisha mapungufu makubwa - najua mwanasheria mkuu anambeba sana but at the end of the day huwezi kufanya kazi kwa kukopa ujuzi kwa mwenzio kila siku!

  Pili, sijui Spika wa Bunge alikuwa anakusudia nini kuteua wabunge wasio na uzoefu kwenye nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na katiba na sheria. Mwenyekiti ni mbunge mpya -viti maalum ccm, hivyo hivyo makamu mwenyekiti ni mgeni bungeni na pia na ccm viti maalum. Knowing kwamba Tanzania iko kwenye mchakato wa katiba, na pia kutambua kuwa katiba ndio kitu kinachotuunganisha sote watanzania pamoja na tofauti zetu, nilitegemea Spika awe na busara ya kuweka watu wenye uzoefu wa sheria kwenye eneo la katiba na pia ahakikishe kamati inaongozwa na wabunge toka vyama vikuu viwili bungeni (sio kimoja) Ukishafanya one-sided leadership kwenye issue inayotakiwa iunganishe wananchi kama hii ya katiba ni dhahiri itakuwa ngumu sana kuepuka malumbano unless uliowaweka wana utashi/ujasiri wa kuwa neutral. Unfortunately hadi sasa kamati inaburuzwa kama sio malumbano. Je katiba itapatikana kwa mtindo huu? Na kama itapatikana itakuwa katiba inayokubalika kwa wananchi wengi?

  La mwisho. Tume ya uchaguzi (NEC) kukusanya maoni nadhani ni madharau ya hali ya juu kwa watanzania. Bila kumumunya NEC wanahusika moja kwa moja na migogoro ya kisiasa inayoendelea sasa hivi. Kama sio uchakachuaji wao watanzania wangekuwa na kiongozi/viongozi wanaowataka na waliowachagua. Kwa sasa ni kama umma uko kwenye forced marriage. Sasa inakuwaje hii tume iliyooza kupewa jukumu nyeti kama la kuratibu maoni? Watakwepaje ugonjwa wao wa kuchakachua?
   
Loading...