Mamlaka ya mji mdogo Katoro

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,334
6,641
Habari za majukumu wanaJF?

Kuna mji mdogo unaokua kwa kasi sana mkoani Geita inayoitwa Katoro. Kwa wale wageni...Ukitoka Geita mjini kuelekea njia ya kwenda Chato au Bukoba unapita Katoro kabla ya njia panda ya Chato na Kahama.

Naomba kutoa wito kwa mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro kwanini wanaona mji unakua kwa kasi vile alafu wao wapo kimya kuhusu mipango mingi. Mji unajengwa ovyoovyo tu bila kuacha njia za Maji; Barbara ya kutenganisha mtaa na mtaa wala sehemu ya kupita maji safi na Maji taka.

Serikali iangalie Katoro kwa jicho la haraka sana la sivyo mipango miji wanaenda kushindwa wasipochukua taadhari mapema.
NB: Sijajua kama ndo sehemu husika ya mada husika.
 
Kuna baadhi ya halmashauri maofisa ni mizigo kama magunia ya vinyesi, wanatakiwa kutumbuliwa majipu
 
Back
Top Bottom