ukhuty
JF-Expert Member
- Oct 9, 2016
- 16,851
- 41,924
haya. ndio tunayotaka kuyaona sio kukurupuka tuKampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries kwa kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) pamoja na taarifa kutoka Mamlaka Ya Udhibiti wa Hali ya Hewa (Zanzibar) inapenda kuwatangazia abiria wake wote wanaosafiri baina ya Dar es Salaam na Zanzibar kwa kutumia vyombo vya kilimanjaro kwamba usafiri huo umesitishwa kwa leo tarehe 23/10/2018 kutokana na hali ya hewa mpaka itakaporuhusiwa na mamlaka husika pamoja na hali baharini kutulia. Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi ama tembelea office zetu.
======
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi na wanaotumia usafiri wa majini kufuatia kuwapo kwa upepo mkali.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Oktoba 23, 2018, Samwel Nguya kutoka kituo kikuu cha utabiri cha TMA amesema watu wawe makini na mamlaka zinazoshughulika na usafiri wa majini ziwe makini kwa kuchukua tahadhari kuhakikisha hakuna maafa yanayoweza kutokea.
Amesema upepo huo unatokana na kuimarika kwa hali ya hewa kwenye eneo la Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika na mfumo wa upepo wa Kusini.
Nguya amesema upepo huo mkali utavuma kwa siku tatu kwenye Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi na maziwa yote makuu ikiwamo Nyasa, Viktoria na Tanganyika na mikoa yote iliyopakana na maeneo hayo, ikiwamo na mikoa ya kanda ya kati.
“Tunaendelea kufuatilia mwenendo wa upepo huo na kutoa tahadhari kila inapolazimika kufanya hivyo, wanaotumia vyombo vya maji wachukue hatua ikiwamo mamlaka zinazohusika na usafiri wa majini,” amesema Nguya.