Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,628
- 6,669
Kheri JF,
Baada ya mvua kuadimika na kiangazi kutamalaki kila kona ya nchi tangu mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, watanzania wengi hasa wakulima walikumbwa na hofu kubwa sana
Kukosekana kwa mvua huko mamlaka husika TMA imekua kimya na kushindwa kuwaeleza watanzania ukweli kuwa mwaka huu hakuna mvua za masika hivyo waache kutumia gharama na nguvu zao kwenye kilimo.
Ni takribani wiki mbili zimepita tangu mvua ziliporudi na kunyesha nchi nzima huku wakulima wakirejewa na imani na hapo ndipo wakajitoa tena kuingiza mitaji yao shambani, huku wasijue kuwa mvua zile zilikua ni za siku chache tu na zitatoweka.
Hapa ndipo hasara kwa wakulima ipo, mvua ilirudi na sio ya uhakika hasa kwa mikoa ya kaskazini lakini mamlaka husika zikawa kimya bila ya kuwataarifu wakulima kuwa mvua hizo ni za muda mfupi.
TMA ni muda muafaka sasa mtoke mtuambie ni nini hatima ya kiangazi hiki?
maana mmetupa hasara isiyostahiki yetu ilhali nanyi mpo mnakula mishahara tu.
Kiukweli wakulima tumeingiwa na hasara kubwa, kwani tuliamua kulima na kupanda mazao upya kwani mazao ya awali yalikua yamekauka.