mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
Napongeza mabadiriko yanayoendelea kufanyika katika mamlaka ya Bandari hususani kiuongozi na kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
Nina wazo ya kuwa Mamlaka ianzishe utoaji wa incentives au tunzo tozo kwa watumiaji endelevu wa Bandari na ambao wamekuwa wakichangia pato la taifa kupitia utumiaji wa bandari pamoja na changamoto za hapa na pale.Hili linaweza kufanywa kwa mkakati wa pamoja kati ya TRA na TPA wakiwa wadau wakubwa wa mapato yatokanayo na tozo,kodi za uagizaji na upitishaji mizigo katika bandari zetu.
Suala hili laweza kwenda sambasamba na kutambua mchango anuai wa mawakala wa forodha wanaowahudumia kwa uaminifu na weredi wateja ambao ni watumiaji wazuri wa Bandari zetu.Ninayo imani ya kuwa kumbukumbu zipo na hivyo mkakati huu waweza kuwa motisha na mbinu nzuri ya kuwahudumia na kuthamini biashara wanayotupa kama nchi.
Wateja toka nchi kama Zambia,Congo DRC,Rwanda,Burundi,Uganda ,Malawi na Kwingineko.Mwisho Tuangalie uwezekano wa kujenga Customer Services Lounge nje ya bandari katika maeneo ambayo waagizaji wa ndani na wa nje waweza kupata taarifa,maelekezo na ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya mizigo..Katika hili tusisubiri Sabasaba au Nane nane pekee.