Mamlaka ya Anga (TCAA) kununua rada nne

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,505
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), inatarajiwa kununua rada nne kwa ajili ya kumulika anga la Tanzania mpaka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mwandamizi wa TCAA, Maria Memba, rada iliyonunuliwa hivi karibuni ni ya mwaka 2002. Alisema ili kukamilisha ununuaji wa rada hizo, TCAA ipo katika hatua za kukamilisha mkopo, utakaowawezesha kununua rada hizo kwa gharama za Euro milioni 22 (Sh bilioni 43).

“Rada hizi zitafungwa Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Alisema mkopo huo utakapopatikana, mradi huo unatarajiwa kuchukua miezi 18 tangu kusainiwa kwa mkataba. “Mradi huo ni sehemu ya mkakati wa TCAA kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za uongozaji ndege ili kutoa huduma hizo kwa haraka, tija na kuongeza usalama katika sekta ya usafiri wa anga nchini na duniani,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alinukuliwa akisema mradi huo ukikamilika utakuwa na faida nyingi kiusalama, kwani kwa kutumia rada mwongoza ndege anaweza kuongoza ndege nyingi zaidi kwa ufanisi na kuongeza mapato.


Chanzo: Habari Leo
 
Hivi ile kesi ya kuongoza ndege zinazopitia katika anga la Rwanda limefikia wapi, hizi Rada zimenunuliwa kutoka wapi France au Israel maana kuna wakati kulikua na kaharufu ka mchezo wa chenge, CC barafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom