Mameya/wenyeviti wa Halimashauri zote nchini kukutana Arusha Juni 9

kalisti lazaro

New Member
Jun 3, 2016
2
3
Mh mstahiki Meya wa Jiji la Arusha atakuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili Juni 9-10/2016,wa mafunzo wa mameya/wenyeviti,Wakurugenzi wa halimashauri za Majiji,manispaa,na miji,nchini,pamoja na wataalam wa mipango miji.Mkutano huu unalenga kujadili mipango iliyopo nay a baadae ya TACINE,(Tanzania cities network)pamoja na kupata maelekezo muhimu ya serikali kuu kwa viongozi wapya wa serikali za mitaa.Pamoja na hayo Mstahiki Meya wa Jiji atatoa uzoefu wa jiji la Arusha hasa namna bora ya kuongoza Halimashauri kwa uwazi,na uwajibikaji.(umma kupata taarifa ya baraza live kupitia redio na social media)Pia Meya wa Arusha atawapa fursa wanasemina ya kujifunza yafuatayo kutoka Arusha

1.Utunzaji bora wa mazingira wa jiji la Arusha

2.Uzoefu wa Jiji la Arusha katika kutekeleza PPP

3.Mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya electronic

4.Jinsi ya kudhibiti watumishi HEWA

Juni 12-13/2016 Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri wote wa UKAWA watakuwa na kikao Arusha,kikao hiki ni cha mkakati wa namna bora ya kushirikiana,na kubadilishana uzoefu wa uongozaji wa Halimashauri ili kuwa na matokeo tarajiwa.

Hii ni fursa kubwa kwa watu wa Arusha maana mikutano hii itakuwa na washiriki Zaidi ya 160.Wagenoi wataanza kuingia Arusha kuanzia kesho Jumanne,hivyo meya anaomba wananchi wote wa Jiji la Arusha kuwakirimu wageni wote kwenye maeneo mbalimbali watakayofikia.
 
Mheshimiwa Meya tunakushukuru sana kwa taarifa , naomba muwafundishe watu wa ccm namna ya kisasa ya kuendesha vikao , kuna taarifa kwamba mtagawa IPAD kwa kila mjumbe , eti ni kweli ?
 
Mheshimiwa Meya tunakushukuru sana kwa taarifa , naomba muwafundishe watu wa ccm namna ya kisasa ya kuendesha vikao , kuna taarifa kwamba mtagawa IPAD kwa kila mjumbe , eti ni kweli ?
Comment yako, hahahahahhhahha. Leo unasemaje kuhusu Meya wetu huyu???!!!
 
Back
Top Bottom