Mameya watatu wamvaa magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mameya watatu wamvaa magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, May 13, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  "MAMEYA WATATU WAMVAA MAGUFULI"
  Wa kwanza kuponda kauli ya Magufuli ni Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, ambaye alimtaka Magufuli kuacha ubabe na asikilize maagizo ya bosi wake, Rais Jakaya Kikwete, aliyoyatoa juzi mjini Dodoma wakati akifungua semina elekezi kuwa watekeleze wajibu wao kwa kutumia busara.
  Alisema anafahamu fika kuwa Magufuli ana ugomvi na mmoja wa wamiliki wa makampuni yanayojihusisha na mabango, hivyo alimuasa kuwa makini ili ugomvi wake huo usiwasababishie wengine hasara na usumbufu.
  “Yeye ana ugomvi na mtu mmoja, lakini anasahau kuwa wanaotangaza kwenye mabango ni wengi, yeye tunajua anachofanya ni kumkomoa mtu mmoja ambaye ana ugomvi naye, lakini hiyo si aina ya utendaji kazi ambayo Rais Kikwete anataka na ndiyo maana juzi Dodoma kawaambia watumie busara na hekima waache ubabe, labda hakumsikia vizuri bosi wake wakati anasema waache ubabe,” alisema Silaa.
  Alisema kauli ya Magufuli kuwa fedha za mabango zinatumika kwa kulipana posho kwenye halmashauri ni dhihaka ya hali ya juu ambayo haivumiliki.

  “Kwa mujibu wa sheria, udiwani ni kazi ya kujitolea maana haina mshahara, hii si kazi ya mshahara kama yeye, kwa hiyo sisi tunaona si bure huyu ndugu yetu labda anatafuta umaarufu wa kuwania urais, lakini sisi tunamwambia kama anautaka urais autafute kwa njia zingine sio kuharibu mipango ya maendeleo ya nchi hii,” alisema.

  “Kutuambia sisi tunalipana posho fedha za kodi ya mabango ni utovu wa nidhamu wa kupindukia, mwambieni aache na asirudie tena kutudhihaki, ingawa hatupendi malumbano naye, lakini asituvunjie heshima,” alisema.

  sijui anatafuta nini labda umaarufu,” alisema.

  “Mwambieni hapa ni mjini asidhani yuko Chato, aliyemwajiri yeye Magufuli na wenzake juzi kawaambia Dodoma watumie busara katika maamuzi yao na tunadhani wamemwelewa,” alisema.----------

  CHANZO: NIPASHE
  SEMINA ELEKEZI NI UFISADI na huu ni ushahidi wa mwanzo
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye bold siasa haijavamiwa kweli?
   
Loading...