Elections 2010 Mambo

Mesaka

Member
Nov 5, 2010
31
2
wanajamii,

Hivi inaingia akilini kweli kwamba ni wa haki kama hili jambo/mabo yaliyotokea katika jimbo la segerea, kwamba mgombea anakamatwa na masunduku ya kura na ambayo hayaonekani katika kata fulani (Buguruni) halafu anatangazwa ndiye Mshindi?

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu sidhani kama atakubali na kusema uchaguzi ni huru na haki. Wala hakuna anayetarajia kwamba watuhumiwa wa uchakachuaji Usalama wa Taifa kama walivyotuhumiwa na Dr. Slaa) wangejitokeza hadharani na kesema kweli tumekisaidia chama tawala kushinda.

Mbali na hili sijasikia mtu yeyote anaye pinga uwepo wa barua juu ya makubaliano ya mkutano wa Mwanza kama ilivyosomwa na Dr. Slaa.

Ninaamini katika uhusika wa Usalama wa Taifa katika uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi kama ifuatavyo;

1. Kwa nchi iliyokithiri kwa ufisadi, na viongozi kupatikana kwa ufisadi hatutegemei kupata serkali iliyo tofauti na ufisadi, kwani viongozi wa idara zote za serikali huteuliwa na rais aliyeko madarakani.

2. Kwa serikali kama hiyo akitokea mtu mpinzani na ufisadi ni wazi atakuwa adui wa serikali nzima. Hivyo mbinu zote zitatumika kuhakikisha hapati nafasi yoyote. Kwani nani atakuwa tayari kupoteza kitumbua chake!

Hivyo hali ndiyo hiyo Tanzania, si rahisi kwa mtu mwadilifu kupata uongozi wa nchi hii kwani waliopo wanahofia kupoteza mali na heshima zao zinazo tokana na ufisadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom