Mambo yazidi kwenda ovyo TFF

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
TIMU za Geita Gold Sport na Polisi Tabora hazikubaliana na adhabu ya kushushwa daraja kwa tuhuma za kupanga matokeo ya mechi Daraja la Kwanza iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo vinajiandaa kukata rufaa.

Lakini wakati timu hizo zikijiandaa kuchukua hatua hiyo, habari kutoka ndani ya shirikisho hilo, zinadai kuwa hali mbaya ndani ya taasisi hiyo ya kusimamia soka ni ‘udhaifu’ wa kiushauri anaopewa Rais Jamal Malinzi.

Kiongozi mmoja ndani ya TFF (jina tunalihifadhi) amedai kuwa kashfa inayolitafuna shirikisho hilo kwa sasa ni madhara ya udhaifu wa ushauri anaopewa Malinzi katika mambo mbalimbali ya kiutendaji.

Mtoa habari huyo alidai kuwa, Malinzi amezungukwa na kundi la watu wasio na uwezo wa kumsaidia ndiyo maana kashfa ya rushwa na lawama haziishi ndani ya shirikisho hilo.

Alidai kuwa tangu bosi huyo aingie madaraka kurithi mikoba ya Leodger Tenga Oktoba 2013, Malinzi hana washauri wazuri wa kumsaidia kazi.

"Haya yanayoendelea sasa ni matunda ya kuwakumbatia watu ambao wanashindwa kumshauri vizuri. Hawamsaidii, wanamharibia ndiyo maana TFF ya chini yake haiaminiki tena na wadau,” alisema mtoa habari huyo.

Aliongeza kwamba viongozi wengi walioingia kwenye utawala wa Malinzi walionekana kutokuwa na uzoefu hali ambayo imechangia kurudisha nyuma maendeleo.

"Kuna baadhi ya mambo yanashangaza sana, utakuta kiongozi yuko pale na anakuuliza jambo ambalo alipaswa kulifahamu kabla ya kushika cheo alichonacho. Hawana uzoefu na uongozi," chanzo hicho kilieleza.

Nipashe jana kwa nyakati tofauti ilijaribu kufanya mawasiliano ya simu na Malinzi, katibu wake Selestine Mwesigwa kuhusiana madai hayo bila mafanikio.

"Niko kwenye kikao," Mwesigwa aliandika ujumbe mfupi baada ya kutopokea simu alipopigiwa.
Juzi jioni, TFF ilitoa taarifaya kujiuzulu kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha.

Chacha alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa ni Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano baada ya aliyekuwa anashikilia cheo hicho, Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ameachia ngazi kwa madai ya kubanwa na majukumu mengine mapya.

Chacha pia jana kupitia simu yake ya mkononi hakupatikana kutokana na muda mrefu kuwa imezimwa.

Wakati Chacha akijiuzulu, jana kwenye mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za sauti za mawasiliano kati ya baadhi ya viongozi wa TFF na viongozi wa moja ya timu zilizoandaliwa kupanda daraja.

Hata hivyo, TFF kupitia katibu wake, Mwesigwa ilitoa taarifa ikikana viongozi wake kuhusika katika sauti hizo na kuahidi kuwachukulia hatua kali wanaosambaza sauti hizo kwenye mitandao.

Hayo yametokea siku chache tu baada ya Kamati ya Nidhamu ya TFF kutoa adhabu ya kuzishusha daraja timu za Polisi Tabora, JKT Oljoro, Geita Gold Sports na JKT Kanembwa kutokana na kubainika kupanga matokeo kwenye mechi za kundi C Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Source: NIPASHE
 
Hawana lolote hao Mkuu watupishe tu na TFF yetu tuwape Viongozi wa mpito watuvushe hapa tulipo. Wanachokifanya ni kutapatapa tu ila tayari Watanzania wameshajua Dagaa ni nani, Papa ni nani na NYANGUMI ni nani.
 
Kaazi kwelikweli. Siamini kama Wahaya wote kwa umoja wao wameshindwa kuiongoza TFF.
 
Back
Top Bottom