Mambo Yanaanza Kufukuta Ndani ya CCM. Neema Kwa Upinzani Makini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo Yanaanza Kufukuta Ndani ya CCM. Neema Kwa Upinzani Makini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Mar 16, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ifuatayo imeripotiwa na Majira.
  UVCCM hawana mamlaka kutung'oa-Chiligati  *Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
  *Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?


  Na John Daniel

  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Maponduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema
  licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

  Wakati Bw. Chiligati akitoa kauli hiyo, wajumbe wenzake wa sekretarieti waliotakiwa kuachia ngazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa 'kumsaidia' mwenyekiti wametofautina kuhusu kauli hiyo huku wakishindwa kuzungumzia kwa uwazi wito huo wa vijana.

  Jana gazeti hili liliwakaririwa vuoa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ukiitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

  Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani Pwani, Bw. Abdallah Ulega wakati akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa humo, huku akisisitiza kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwa ndiyo imekuwa ikitoa siri kwa chama cha upinzani cha CHADEMA.

  Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

  Akizungumza na Majira jana Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

  "Ni haki yao kutoa maoni, sioni cha ajabu hapo, vijana wana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa.

  "Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

  Alipoulizwa changamoto waliyopata na iwapo wanajiandaa kuwasilisha mapendekezo yao kwenye vikao vya juu kutokana na wito wa UVCCM hakuwa tayari kutoa majibu ya moja kwa moja badala yake alisisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

  "Nimesema hayo ni maoni ya vijana na wana haki ya kuyatoa," alisistiza Bw. Chiligati bila kufafanua.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba alisema licha ya kuheshimu uhuru wa kutoa maoni lakini haamini kama yaliyoandikwa katika vyombo vya habari ndiyo yaliyozungumzwa na UVCCM mkoa wa Pwani.

  "Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema," alisema Bw. Makamba.

  Alipotakiwa kujibu iwapo katiba, kanuni na taratibu za CCM zinatoa nafasi kwa umoja huo kuondoa secretarieti iwapo imeshindwa kutimiza wajibu wake alisema;

  "Ni maoni yao, lakini pia sina hakika kama yaliyoandikwa yako sawa sawa," alisema Bw. Makamba bila kutoa ufafanuzi wa kina.

  Alipoulizwa hatua atakazochukua kama Mtendaji Mkuu wa CCM kuhusu wito huo wa UVCCM alisema yeye hawezi kujitetea kupitia magazeti na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

  "Siwezi kufanya kazi ya kujitetea kwenye magazeti, wao ni vijana wa CCM, wamekaa kwenye baraza lao wakasema, sasa unataka nisema nini? alihoji Bw. Makamba na kuongeza, "Nasema hivyo ndivyo walivyoona. wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo hawakupatikana kutoa maoni yao kwa simu zao zilikuwa zinaita bila majibu.

  Mbali na sekretarieti, vijana hao waliwashambulia mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye wakisema kauli zao za kukikosoa chama hazina lengo zuri bali ni njia tu ya kutafuta urais 2015

  Akizungumzia suala hilo, Bw. Lowassa ambaye pia alionywa na vijana hao kutoa maoni nje ya vikao wakati anayo nafasi ya kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete, alisema maoni yake kuhusu uchumi hayana sababu ya kusubiri vikao.

  "Nilikuwa vijijini kwenye ziara sijasoma magazeti, lakini wewe nikikuuliza hali ya uchumi utasema kuwa ni nzuri?Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imependa hilo nalo tusubiri vikao? alihoji Bw. Lowassa.

  Alisema kama mtu anataka kuwania urais mwaka 2015 hawezi kuanza kampeni kwa sasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kutoa nafasi ya kushughulikiwa na kuchafuliwa na maadui. Bw. Sumaye hakupatikana jana kwenye simu yake.

  Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kuzungumzia wito huo wa UVCCM, alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa hayo ni maoni ya vijana na kila mmoja anayo haki ya kutoa maoni yake.

  "Hayo ni maoni ya vijana, sasa unataka nitoe maoni gani?" alihoji Bw. Msekwa. (End of Quote)
  Nimei-red paragraph hiyo kwa kuwa inanipa maswali mengi. Hawa ndugu zetu kumbe wana siri ambazo zikitolewa kwa Chadema zinasababisha kupungukiwa kura? Siri gani hizo? Au jamaa kachemka? Mbona majibu ya mabingwa wa kuchonga kama Makamba yamekuwa mafupi kiasi hicho?
  CDM tukiweza kuondoa tishio au uwezekano wa surprise kutoka kwa Zitto na kudumisha umoja mambo yanaweza kuwa rahisi kwetu 2015.
   
 2. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siri zipo, za EPA, Meremeta etc. Ila wanaotoa sio Sekretariet pekee bali wote waliochoshwa na udhalimu wao.
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Kwa tetesi nilizozipata jana kunakutokuelewana kani ya mwenyekiti na sekretariet iliyopo hasa makamba. Sababu ni kuwa mwenyekiti anataka kuwatosa wakati wao ndiyo walimpigania kupata ushindi pia mwenyekiti analetewa umbea na watu kuwa sekretariet imechoka na inatakiwa waachie ngazi, pia kuna mnyukano wa mwenyekiti anawatu wake ambao angependa kuwapo kwenye sekretariet hiyo wakati wajumbe hao hawataki kutoka ama wanawatu wao ambao wangependa wachukuwe nafasi zao sasa hapo ndipo kazi inakuwa pevu.
  Bado ni tetesi zikiwa wazi tutahabarisha vizuri.
   
Loading...